Always, ukweli ni mchungu, lakini inabidi usemwe.
Lowassa ni fisadi, ni kweli, lakini watanzania wengi wanamkubali, huo nao ni ukweli hata kama hatuutaki.
Katika pita pita zangu kila sehemu ninayofika hata kama ni safari za mikoani huwa najaribu kuchokoza mada za siasa ili kupata mawazo yao. Wengi wanajua kuwa jamaa ana kashfa, ila wanasema ni mchapakazi. Wengi wanasema kama Lowassaa atapitishwa kuwa mgombea bila shaka watampa kura yao. Naomba msinishambulie mimi mgeni jukwaani bandugu:lock1:
kama mwizi mbona hawampeleki mahakamani bana, huwezi mwita mtu mwizi tu from no where...na kwa sabb wameshindwa kumpeleka mahakamani hiyo inathibitisha kuwa lowasa sio mwizi..na ndio mana watu tuna imani naye..
ukiangalia kwa mapana yake kunzia serikali hadi wapinzani wote wezi tu!!!!!! kwani hujasikia huyo mbowe anakopesha chama chake hela na baadae anajilipa mamilioni zaidi? anaununua vifaa bya chama mwenyewe na chenji anawekandani..anafanya hayo kwa kushirikiana na watu wake wachache ndani ya cdm..hapo hajapewa wizara au uraisi itakuwaje?
kwa kifupi watanzania wengi hawajui tu kwamba siasa ni ajira na kwamba wanasiasa hawako kwa ajili ya wananchi bali kwa maslahi yao..mpka uelewe haya ndio utaelewa kuwa hakuna mwanasiasa msafi kizazi hiki