LoveMeter - Airtel Jirekebisheni....

Domhome

JF-Expert Member
Jun 28, 2010
3,197
3,930
Kila siku napokea sms toka Aitel yenye ujumbe huu:

"Kupima kama unaendana na mpenzi wako kwa kutumia love meter, tuma love nafasi jina lako nafasi, jina la mpenzi wako kwenda 15334 kwa shs 250= tu"

USHAURI KWENU AIR TEL:
Sizitaki hizi sms zenu kwenye simu yangu, laa sivyo nitawashitaki!!
 
Hata mimi siutaki ujinga huu nawashangaa hawa airtel kunifanyia usumbufu.
 
Ndio hii ni kweli kabisa imekua shida na usumbufu maana
mi mwenyewe nashindwa kuwaelewa hawa jamaa waache mambo
ya kusumbua watu
 
wanapenda sana hela hawa...yaani wamekaba weeee wakaona bado. mpaka wameamua kuingia kwenye michezo tuliofanya sana tukiwa secondary...ujinga mtupu!
 
Kila siku napokea sms toka Aitel yenye ujumbe huu:

"Kupima kama unaendana na mpenzi wako kwa kutumia love meter, tuma love nafasi jina lako nafasi, jina la mpenzi wako kwenda 15334 kwa shs 250= tu"

USHAURI KWENU AIR TEL:

mi nakushangaa unalalamika wakati hili nis oko huria amua kama mimi vunja lain yao tupa kule tafuta mtandao mwingine
yaani mimi wameniudhi sana mpaka nimeamua kukatafuna haka kaline kama inavyoonekana hapa kwenye picha nikakatupilia mbali ndio wakome
airtel.jpg
 
By the way hii ni kuingilia uhusiano wa watu and it's totally not acceptable, sijui hao TCRA wanasimamia nini kama hata vitu kama hivi hawawezi kuviona. Huo ujumbe maana yake ni kuwa upime kama unaendena na mpenzi wako..... na kama hauendani then what next.... muachane?! Upime kama unaendana na mke wako...This is fu...y kabisa. and they are charging 250. Kututumia ujumbe wa hivi ni usumbuufu na wizi mkubwa, TCRA pls wake up.
 
Wadau huo ni wizi uliokubuhu. Kwa namna nyingine huo mchezo ni sawa na kupiga ramli kwa mganga wa kienyeji ili ujue mwanamke au mwanaume fulani anakupenda au hakupendi. Kimsingi hakuna logic yoyote zaidi ya kuvuna hela za watz kijinga maana ukituma hayo majina watakutumia kiwango cha mapenzi kati watu wawili ambao majina yametumwa. Percent inaweza kuwa kubwa au ndogo lakini hakuna justification ya kuwa kweli mtu anakupenda. mapenzi hayapimwi kwa mashine hata siku moja. Mbaya zaidi hata ukituma jina la dadako kakako, babako, babu, hata jina la mbuzi, ng'ombe gari nk lazima upate asilimia fulani ya upendo.
Kuthibitisha hilo fungua internet (eg google) andika love meter kwenye google unapata huo upuuzi. Nilitest Zali ya love meter kwenye internet kati ya Suzuki Swift na Toyota Hiace ikaja 99%. Can you imagine. Inasikitisha sana kuona kampuni kama hii inaamua kuwaibia watu kwa njia kama hii. Kweli tz shamba la bibi aisee. WIZI NA UPUZI MTUPU.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom