Sehemu ya 2
Aliendelea kunipigia simu usiku ghafla kama kawaida yake na mimi sikuwa naenda halafu nilikuwa namba yake hata sijai save
Kutokana na namna alivyokuwa anaongea kila akinipigia simu namuuliza wewe ni nani?
Akanijibu mimi ni fulani (jina lake silipendi kuliweka hapa) yeye akawa anadhani namjua sasa nikamuuliza cousin wangu Farida unamjua mtu fulani?
Akasema ndiyo.... ndiyo nikaamua sasa kuingia ktk profile yake nikaangalia picha zake....... ndiyo nikamjua na Farida akaniambia anampenda sana huyo, kiukweli sikuwa najua nyimbo zake lakini kuna nyimbo moja nilikuwa naijua ila sikuwa najua kama yeye ndiyo kaimba.
Farida akawa ananiambia nyimbo zake basi tukawa tuna tabasamu......
Tukajiona tuna bahati kumjua pia pia nilitamani kumuona live lakini nilijikaza sana kwa sababu sikupenda ambavyo alikuwa akiniita ghafla usiku ni mtu fulani ambae anatumia jina lake na mimi nikakaza kwa hiyo sikuwahi kwenda kabisa .
Basi nilimpotezea sana kwa muda mrefu kuna siku tulikutanana online akawa ananitongoza rasmi hapo sasa nilikuwa tayari namjua kama yeye ni msanii nikawa namwambia
Bwana mimi naomba tuwe marafiki wa kawaida tu
Nikamwambia mimi nina mpenzi wangu ba hapa nilipo na pete ni mchumba wa mtu.
Alisema ndiyo lama kutoka na mimi basi wewe kama hutaki kutoka na mimi basi tuwe marafiki, wewe kuwa rafiki yangu siwezi.
Mmmmh nilishangaa maana yeye alikuwa ni msanii na niliona kama ananinyima haki ya kuwa shabiki wake nikamtolea mfano wa huyo msanii mwingine.
Nikamuuliza kwani nyie mkoje? Mpaka mlale na mtu ndiyo mjione wanaume? Basi tukaishia hapo kuchat akiwa anasisitiza anataka kuni.... tena anataja lile neno gumu.
Alinistaajabisha yaani nilizoea kutongozwa kistaarabu kwa heshima lakini hapo heshima ilikuwa 0
Itaendelea.....