Love at first sight

Duh, kidume nasafiri mno mno ila sijawahi kupata hio bahati ya kukaa nna binti. Juzi kati natoka Mbeya kufika Igurusi akapanda binti ana rangi nzuri sana, nyeusi flani hivi, nilikua siti namba mbili, yeye akakaa pale, akanichangamkia mno. Dah, ghafla Agent kaja kumuondoa pale kamwambia siti INA MTU aiiseee nililaani dah
 
Good,enjoy your love baby. Nivizuri kutoa yamoyoni wengine humu wanakufa na emotion zao kimyakimya.
 
Hey guys

Imeshawahi kutokea ile hali umemuona mtu mara moja tu ukatamani awe wako?

Imenikuta stendi ya mabus mkoa fulani kuja Dar. Siku nafika pale nikamuona mkaka mmoja amazing,sijui kwanini alikuwa ananiangalia vizuri namna ile...kimoyo moyo nikaweka sala fupi "ee Mungu huyu kaka hata nisipokaa nae seat moja naomba nisafiri nae bus moja tu" halafu nikamalizia na Amen,nikaingia kwenye bus

Nimefika kwenye bus nikakaa nikiendelea kusali sala ile ile ya Mungu asaidie yule kaka kuwepo ndani ya bus nililopo,nikajisemea ngoja nitoke ndani ya bus nijifanye naenda washroom ili nimuone hata mara nyingine,nikatoka nikaenda washroom

Mungu ni mkuu jamani, nilivyotoka washroom nikaingia ndani ya bus nikamuona yule kaka ndani ya lile bus, mimi namba 9 yeye 10

Sikuwahi kuona safari fupi kama ile japo kiuhalisia ni safari ndefu mnoooo, masaa yalikimbia fasta kinyama huku tukiwa tumezoeana kama vile tulikuwa tunafahamiana kabla.

Hiyo ni mwaka mmoja uliopita tarehe kama ya leo,tumekamilisha mwaka with my man 😊😊 Japo haiwahusu wala haiwasaidii kitu lakini nawaambia tu...nampenda huyu mwanaume

Naona kila kitu changu kinampenda,macho yakimuona napata ile amani ambayo siipati kwa yoyote,mwili wangu umemkubali mana nina hisia kali sana juu yake,nikiisikia sauti yake napata ile hamasa ya kuendelea kumsikiliza akiongea hata kama haongei na mimi

Sijawahi kuwa mdau ya ngono lakini tangu nikutane naye nataka kila muda tuwe peke yetu chumbani

Cheers to many years with my man 🥂

Am so in love!

Hongera sana Joanah kwa kumpata wa kufanana nae
Kwa maelezo yako ni kwamba umempata mwenza yaa mwili, moyo, nafsi vyote vimebalance

Mungu awatunze
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom