Los angelitos: Je, siku ukiondoka dunia na watu watakukumbuka kwa lipi...?

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
35,697
106,861
Mates,Moja kati ya maswali ambayo hua najiuliza kila siku ni je ikitokea leo nikaondoka je jamii iliyonizungukai tanikumbuka kwa yapi? Je dunia itanikumbuka kwa lipi/jambo lipi nililoitendea? au ndio nikiondoka watanifukia tu na kunisahau au watabaki wananikumbuka kama mtu niliyefanya kitu fulani muhimu katika maisha yao na dunia kwa ujumla. Binafsi hua nawaonea wivu sana wale majamaa wawili kutoka midle East ambao ni Yesu na Muhamad, katibia robotatu ya wakazi wa dunia nzima wanaishi ndani ya miongozo ya falsafa zao kila siku. ndio maana ni miaka karibia 2000 na zaidi lakini bado hawa watu wanakumbukwa na kuheshimiwa kwa falsafa zao walizoaacha kwenye jamii, natumaini mpaka mwisho wa dahari majina yao hayatasahauliwa. Sio hawa tu pia kuna watu mbalimbali wameweza kujijengea heshima kwa matendo yao mbalimbali waliyotenda hapa duniani kama vile Nyerere,Karl Max,socrates,Davinci,Newton,tesla,Einstein Nk nk. -Respect yourself and who around you.

Legacy ni vitu ambavyo siku ambayo wewe ukifa watu waliobaki watabaki wanakumbuka kwa vitu hivyo. Baada ya wewe kufa tu utazikwa watu watapiga pilau na bia kwenye utanduzi wako wa msiba baadae ndugu wataanza kutoana macho kwa kugombania malina vitu ulivyoacha...punde watakusahau maana akili yao itakua bize kuwaza jinsi kupata mali zako ulizozichuma kwa jasho na damu baada ya kumaliza kutapanya mali zako watakusahau kabisa(kasoro mama yako tu na watoto) tena hata ulipozikwa watapasahau maana kwakua hukua na chochote cha kuOffer kwenye jamii hawawezi hata kutambika kwenye kaburi lako. Angalua ulipozikwa panaweza kupata bahati ya kupaliliwa na waumini wa jumuia wakifanya usafi au Waumini wa swala tano. Marafiki zako na wale waliokuita mkuu kwenye vikao vya baa hawana habari nawe tena. Sasa umeona kwamba ukifa hutakumbukwa kwa wingi wa mali ulizoacha, wanawake uliotembea nao, watoto ulionao bali watu na dunia itakukumbuka kwa lipi hasa ulichofanya kwenye jamii yako. -Be Humble, life is full of possibilities.

Moja kati ya utajiri mkubwa na wa thamani sana ambao binaadamu mimi na wewe tumepewa ni Choice au Free Will, yaani uhuru wa kuchagua kuishi vile ambavyo wewe mwanadamu unataka. Hivyo basi kila mtu anaweza kuitengeneza kesho yake iwe kutokana na vile yeye ambavyo ametaka iwe kwa kuzingatia chaguzi zake katika maisha...kutokana na chaguzi zako unaweza kuchagua jina lako liishi mioyoni mwa watu kama mtu mwema sana na wakutegemeka, msaidizi naa mshauri wa mambo mema nk...Au utapenda jina lakoli baki midomoni mwa watu kama kibaka mzuri sana, bishoo sana,tapeli mzuri,Mtia mimba na mkimbia mimba, mzee wa totoz, mtukanaji mzuri nk. -We have Granted the ability to choose what we want to be, We are determined by our choice we make. every choice we make it have its consequences...Choose wisely.

Dia de Muertos
Nchi za Latin Amerika hasa Mexico wanaamini kwamba mtu baada ya kufa anaenda kwenye ardhi/nchi ya wafu nakuwaacha waliohai katika nchi ya walio hai, hivyo basi nchini za latin America hasa mexico hua kila tarehe 2 ya mwezi wa kumi na moja hua wanaadhimisha siku ya wafu wenyewe wanaita Dia de Muertos. Kila familia nyumbani mwao wamejenga Alatare/ madhabahu ndogo ambazo wao wanaita Ofrenda, kwenye madhabahu hiyo hua wanaweka vitu mbalimbali ambavyo ndugu zao walikua wanavipenda wakati wakiwa hai hasa chakula na vinywaji kubwa zaidi wanaweka picha za wapendwa wao waliofariki pia madhabahu hiyo hupambwa na kwa petali za maua ya njano wenyewe wanayaita cempasúchil au Flor de Muerto (maua ya marehemu)...ukutani wanaweka msalaba au sanamu la Mama bikra maria.

Siku ya sherehe (November2) watu wa famili hunywa na kula pamoja watu wazima waliofariki huwekewa pombe za aina mbalimbali huku watoto wadogo waliofariki wenyewe wanawaita los angelitos (the little angels) huwekewa Toys...Sasa ili soul ya mtu aliyekufa iweze kuvuka kutoka kwenye Land of the dead hadi Land of the living kuungana na familia yake lazima picha yake iwe kwenye Ofrenda/madhabahu au watu wa familia yako/jamii wawe wanakukumbuka. Kwakutambua kwamba ili uje uungane na familia yako lazima watu ulioishi nao au familia wawe wanakukumbuka hivyo wengi hujitahidi kuishi vizuri na familia au jamii wanayoishi ili waache kitu kitachofanya wakumbukwe (kwenye jamii), kumbuka hakuna mtu kwenye familia au jamii anaweza kukukumbuka kama hukua mtu mwema kwenye familia au jamii. After you dead and rotting in the ground it is the Legacy that lives on, not your personal Groly,not your honor it is Legacy. -Tywin Lannister

Je, tufanyaje ili kuacha alama maishani?
Wanasema kwamba Dead man tells no tales lakini mimi nakuambia kua A dead man can leave a tale, a good tale that can last and been told for thousand years. Legacy ndio kitu pekee ambacho mtu anaweza kukiacha na kubaki mioyoni mwa watu,hivyo tuangalie ni kitu vitu gani hasa vinaweza kufanya tukaacha alama isiyofutika duniani. Kwawanaoamini katika Mungu tunaweza kuelewana.
  • You worth, and you are wonderful made

Katika harakati za kufanya mambo ambayo yanaweza kuacha alama duniani mtu anaweza kusema kwamba mimi ni mdogo, mimi sifai kwenye jamii, mimi sina uwezo wa kifedha na mambo mengi ambayo yanaweza kumfanya mtu ajidharau katika mambo anayotaka kutenda...Baada ya Mungu kumuumba mwanadamu alimpulizia pumzia ambayo ni nafsi ya uhai akampa mamlaka ya kutawala kila kitu kilichopo duniani, kama Nafsi ya uhai tuliyonayo mimi na wewe leo ilitoka kwa Mungu basi vivyo hivyo mimi nawe tuna uungu ndani yetu ndio maana mwanadamu ameweza kufanya maendeleo makubwa na gunduzi nyingi ambazo kiumbe mwingine hawezi. Watu wasioamini katika Mungu na wanaita Psychic power/abilities ambayo unaipata mpakabaada ya kuUnlock vitu fulani na vitu fulani lakini kiukweli ni uongo tu ni Nafsi hiyo ya uhai kutoka kwa Mungu inayotuwezesha kutenda mengi makubwa.

Mwanadamu ndio kiumbe pekee ambaye ana sifa zote mbili Imortal na Mortal, Anamwili ambao unakufa na roho ambayo haifi, vyote kwa pamoja vinaunda mwanadamu aliyeumbwa kwa jinsi ya ajabu..ndio maana malaika na viumbe wengine wote wanashindwa hadhi na malaika. mbele ya Mungu mwanadamu ni kiumbe first class, huko juu tumeona tumepewa uwezo wa kufanya chaguzi, ni mwandamu pekee ndio anaweza kuchagua kua immortalau mortal.

kwa lugha rahisi tunaweza kusema kwamba Mwanadamu ni Strong Artificial Intelligence maana anaweza wa kujifunza na kufanya lolote yeye alilotaka/alilopenda wakati malaika wao ni kama Weak Artifiacial Intelligence ambao wamekua programmed kuperfom special task. kama malaika kawekwa kua mlinzi basi ataishi maisha yake yote akilinda.

Maelezo yote hapo juu ni kuonyesha jinsi gani mwanadamu ameumbwa na uweza mkuu hivyokila chochote anachotaka kufanya anaweza kutimiza. Varys (GOT character) anasema kwamba A small man can cast a large shadow, akimaanisha kwamba mtu mdogo anaweza kutoa kivuli kikubwa, hivyo basi haijalishi wewe ni mdogo au mkubwa maskini au tajiri bado unaweza kufanya kitu kikubwa ambacho kitabaki mioyoni mwa watu kama tu ukiwa na imani thabiti juu ya uweza uliopewa na dhamira kuu juu ya upendalo kufanya.....wandamu tumeumbwa kwa mfumo wa kua compatible to each other au kama vidole vilivyo, kila baada ya kidole kimoja katikati kuna uwazi ambao vidole vya mkuno mwingine vinaweza kukaa pale na kutengeneza bond imara. hivyo ndivyo inavyotakiwa wanadamu wawe kuna watu wamepungukiwa vitu fulani inabidi mwingine aje aongezee alivyonavyo ili kumfanya mtu awe mtimilifu, ndio maana twatakiwa kusaidiana na kuishi kwa upendo.

Stan Lee ansema Great powers comes with great responsibilities, ukiona umepewa utajili basi usijidai na kuuficha ndani peke yako. unakua umepewa nyenzo za kuwatoa watu wanaokuzunguka katika matatizo yao mbalimbali, kama law of nature inavyotaka anayetoa ataongezewa aliye na uchoyo atalaaniwa na utajiriwake.hivyo kwa hicho hicho kidogo ulichonacho unaweza kuanza nacho kufanya mambo ambayo yatakua alama siku ukiondoka.-With tremendous Ambition everything is possible.
  • Fahamu wewe ni nani na kusudi lako ni lipi.
Huko juu nimewataja Muhamad na Yesu kama watu walifanikiwa kuacha legacy duniani karibia kila mtu anawajua, ukichunguza waliwezaje kwanza kabisa walijua kuna Mungu aliyeumba vyote na kujua kwanini Mungu huyo aliwaleta duniani. hivyo basi kama unahitaji kutenda kitu kitakachokufanya ukumbukwe kwanza lazima ukiri uwepo wa Mungu na kwamba wewe ni zao la uumbaji wake kwa kuzingatia imani yako -A hero can never exist in vaccum

Quinque viae; Hizi ni shahuda zinazoonyesha uwepo wa Mungu duniani hivyo tutazitumia kuangalia kwanini tumtegemee Mungu kutimiza matakwa yetu chanya.

The First Cause and The First Mover
Kwanza inabidi ukiri kwamba kila kitu kilichoko duniani kimeumbwa nae na kila kinachotokea kinatokea kwa matakwa yake, hivyo unaweza kutimiza lolote unalotaka maana yeye ndio muumba wa vyote.Maskini na tajiri, mrefu na mfupi, mweusi na mweupe wote wameumbwa nae na kila binaadamu anatakiwa kujali hali ya mwenzake. Ukimuomba takupatia, ukitoa atakubariki...Ni wewe kukiri kua huwezi bila ya msaadawake. "kwa maana Bwana amenitia mafuta na neema zake zinamiminika juu yangu"

Tambua kwamba ulitoka kwa Mungu, upo hapa kwa ajili ya Mungu na utarudi kwa Mungu hivyo kusudi lako linatoka kwa Mungu na kila mtu kaumbwa na kusudi lake...Muombe Mungu wako akuonyeshe kusudi lako kisha simama katika kusudi lako na kulitekeleza... Binaadamu mkamilifu ni asikiae shida na mateso ya wanadamu wenzake.Wanasema maneno hayavunji mfupa ila yanweza kuvunja au kujenga roho ya mtu hivyo hata kwa maneno yako yenye Uungu na heri ndani yake unaweza kuacha alama na kua mfano wa kuigwa kwenye jamii.

sio lazima utoe mamilioniau misaada mikubwa lakini maneno yako yenye faraja yanweza kuishi mioyoni mwa watu daima. Kuna watu wengi hawana furaha wala faraja wanatamani hata mtu wa kwenda kuwafariji kwa maneno tu hivyo unaweza kuanza kwa kufanya hivyo.PEnda kua malaika wa amani na upendo,mpatanishi na muunganishi baina ya watu na watu mapaka wanaokuzunguka wakuone kua kweli U mMungu pamaja nasi au Heaven Sent.

Note:
Wakati unatafuta jinsi ya kuacha alama duniani kumbuka kua pia dark Dimension can Help you, hapa watu wanakwama. Dark Dimensio pia imesaidia wengi kufanya vitu ambavyo vimeacha alama duniani lakini bado haistahili maana yafaa nini kupata mali na sifa zote duniani halafu ukakosa rehema za Mungu? Hivyo basi wakati unatenda mambo yako angalia unayafanya kwa kutegemea BackUp ya Nani. Genuine data zinatakiwa kutoka kwenye Server za Light Dimension ndiodata hizo zinakua hazina malware na Virus mbalimbali.
all the best on your Journey to achieve inner happiness and Ligh Dimmensions
-Vinchii
el maestro..
 
Kwa hiyo unajilinganisha na hao wana wa Mungu? Familia yako inatosha mkuu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom