Lori laparamia kibanda, laua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lori laparamia kibanda, laua

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Jan 26, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,439
  Likes Received: 22,355
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Baadhi ya wasamaria wakijaribu kutoa msaada kwa waathirika wa kibanda kilichoparamiwa na lori leo asubuhi na kusababisha kifo cha mtu mmoja katika ajali iliyotokea leo asubuhi Mbagala Rangi Tatu.

  MTU mmoja amekufa baada ya lori la mchanga kuvamia kibanda cha biashara katika ajali iliyotokea leo asubuhi Mbagala Rangi Tatu.

  Tukio hilo limetokea leo asubuhi Mbagala Rangi Tatu ambapo ajali hiyo imesababishwa na lori lenye namba T 872 AVS aina ya Fiat baada ya kumshinda dereva wake ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja.

  Kwa mujibu wa mashuhuda wetu waliongea na gazeti hili kwa nyakati tofauti wamedai kuwa dereva huyo wa lori, akiwa kwenye mwendo kasi, ghafla alivamia kibanda hicho kilichokuwa kando ya barabara na kusababisha kifo cha mwanamume mmoja aliyekuwa amesimama nje.

  Maiti imehifadhiwa chumba cha maiti Hospitali ya Temeke na polisi wanaendelea kumsaka dereva wa gari hilo.

  Pia, wakazi 36 wa jijini Dar es Salaam wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa na makosa mbalimbali.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga, amesema watuhumiwa hao walinaswa jana wakati polisi wakifanya msako mkali wa kuwasaka wahalifu.

  Amesema kuwa kati ya watuhumiwa hao watuhumiwa 12 walinaswa Kinondoni.

  Amewataja baadhi yao kuwa ni Asha Juma (42), Joseph Paulo (35), Juma Said (25), James Paulo (35), Ally Said (46), na wenzao.

  Pia, watuhumiwa wengine 14 walinaswa Temeke na Ilala wakiwa wanauza pombe haramu ya gongo na wengine walikutwa wakiwa na bangi.

  SORCE: DAR LEO
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  poleni jamani kwa maafa
   
Loading...