Look at Kenyans Murdering Each Other!

Jamani uko wapi utawala wa sheria?
Ohh Mungu awasamehe wote hao coz hawajui watendalo.
Sidhani kama wanakumbuka ONLY GOD CAN JUDGE US.
 
Last edited:
Jamani jamani hii desturi ya kuchukua sheria mikononi inasikitisha sana kupita maelezo.Halafu serikali ya Kenya inaangalia. walipashwa hawa watu waliofanya hiki kitendo wachukuliwe hatua hata kwa kupitia kitengo cha haki za binadamu.Najuta kwa nini nimeangalia. Hii ni kiasi gani mwanadamu amegeuka kuwa kama mnyama na zaidi ya mnyama.Its hard to believe kama a human being can do such a horrible and scary action. shame on us.
 
Jamani jamani hii desturi ya kuchukua sheria mikononi inasikitisha sana kupita maelezo.Halafu serikali ya Kenya inaangalia.

Sio suala la serikali ya Kenya. Hii ni sehemu ya mazoea, utamaduni wetu hata sisi Watanzania. Mtu akishukiwa kunyofoa kidani cha mkufu anapigwa mawe mpaka afe.

Mimi nimewahi kushuhudia mwizi anapigwa mawe kama chatu. Waliorusha mawe na wale tulioangalia yale mawe kama sindimba wote ni sawa na tulishiriki kwenye yale maovu. Tena tuliokodolea macho huu mdundiko ni wabaya kuliko waliorusha mawe (Martin Luther King Jr). Ni utamaduni wetu, na hata conception of justice ya Waziri Mkuu wetu Mizengo Pinda na yenyewe imetoa approbation to this heathen justice isokuwa na due process, wachawi na wanaodhaniwa kuua Albino, akasema, tuwaue hapo hapo!

Ushirikina unaathiri jamii, lakini due process inataka mtuhumiwa uchawi apate nafasi kupinga hakutenda uchawi.

Siyo suala la kabila la Kikenya au serikali ya Kenya. Utamaduni wetu, Tanzania na Kenya na kwingine kama kwetu, utamaduni wetu wa haki haujajengwa na due process.
 
Ok, Hapa lazima na mimi niongeze maoni yangu. Cha kwanza, tusisahau kwamba sisi ni binadamu. Binadamu, yani Humans, we have two sides: One, is the side of us that sits at a cafe with one leg over the other sippin coffee with ease in the company of a lovely lady or a man. The other is the side shown above "ogelea ogelea kwa moto". Sio unyama, ni ubinadamu, tusisahau hicho. The so called 'civilised' and 'uncivilised' part of man. It is the mere reality of man, let us not call it animal like.
And I want to ask the following questions.
Albino killings, and the beuracratic approach we have witnessed our government choose. How effective has it been? Go report suspects my fellow wananchi says Pinda, and while your at it you might as well throw in those you suspect of drug trafficking and armed robbery as well. Lack of evidence, lengthy trials, removal of business licenses.

How effective has the 'civilised' approach been to the albino slaughters, an 'uncivilised' problem?
 
Last edited:
inasikitisha sana, lakini kama alivyosema kuhani
tatizo ni kubwa zaidi kwani inaonyesha hata watazamaji
wameafiki na unyama huo na hili ndilo linatisha zaidi.
 
Hii video ni mbaya sana, lakini pengine ndio hali halisi ya kuua albinona iliyowakumba bibi wenye macho mekundu kule Shinyanga miaka ya karibuni huku Bongo ingawaje bado hatujapata live video yake kama hii. Sasa hii inatupa mwanga how serious matters can be.

Sasa nchi ina sheria, vijini na mitaa ina watawala watu watano wanachomwa moto live. Ajabu kabisa. Nashindwa hata cha kusema kwani uchawi ni imani tu.
 
Sio Kenya tu Hata Tanzania mbona vibaka wanachomwa na matairi? Mbona vibaka wanauwawa kwa matofali na mawe????? all are sad news. Kweli bado ni primitive practices.
 
Mh! no difference with Tz, havent you guys read LHRC Human Righs Reports on mob justice and the like? I saw similar actions which was aired by ITV when a mob in Tegeta burnt to death a mere kibaka whose mistake was snatching a woman's kipima baridi! and the police post is not even far! not only that it also happened around Mabibo!
 
Unbelivable!!

How can this happen at a time that an African has gone far enough to lead the Free World???

A disconnect somewhere??​
 
huu unyama sijawhai kuuona toka nizaliwa. Mungu anisaidia, nisianze kuwehuka kwenye ndoto usiku usingizini. mchana kweupeee, sijawahi kuona kabisa. watu kibao wanaangalia, jamani, jamani, hivi kuna selikali huko? pamoja na kwamba sisi wenyewe hapa tuna albino na vizee shinyaga, lakini inauma ati.

Serikali ipo lakini wamelala baada ya kulewa na hela za ufisadi.
 
dah. hii kali. binadam kumfanyia binadam mwenzie kama vile

majuzi hapa bongo vyombo vya habar vimeripot kuwa bibi mmoja na wajukuu wake shinyanga walifungiwa milango kwa nje usiku petrol ikamwagwa kwenye nyumba na wakapigwa keberit. mpaka majiran kuja kuwasevu walishaungua sana. yule bib alifia hospitali. mungu amlaze mahali pema peponi

mitaa ile tunasikia kila mara akina bib wanauawa - eti wachawi etc. na mara viungo vya albino. mitaa ya mbeya siku si nyingi tulikuwa tunasikia watu kuchunana ngozi. na mitaani kama dar vibaka kuuawa kwa matairi shingoni, kupigwa

jamii inajua wakosaji wanastahili kupelekwa polis/vyombo vya sheria. lakin jamii haifanyi hivyo. inaadhibu kwanza then polis labda baadae
 
kwa hapa kwetu

vibaka hawakabi 'kistaarabu'. kibaka haoni shida kukata sikio ili apate kidani. na hata mkimkamata si muda mrefu mtamuona mitaani. labda ushupalie sana

kwamfano kibaka unamwona akimkaba mtu na kumpiga kisu. jamaa anadondoka chin damu kibao na mara mnaanza kumfukuza. mnamkamata anawajeruhi kwa kisu. mtapata shida mumpeleka kishikaji polis. zaid zaid mtaanza kumshushia kipigo kwanza

au umewahi kusimuliwa au kuona majambaz kuvamia nyumba ya mtu na kuwakata kata mapanga watu wote waliokuwa ndani. hii ni pamoja na kubaka etc. wakakamatwa na kupelekwa polis. muda si mrefu tena mnasikia wameachiwa kwa sababu ya 'kukosekana ushahidi'. then siku si nyingi tena ukaona majambazi wanakurupushwa sehemu. mkawafukuza na mkawakamata. mkiwatia mikononi si rahis sana kuacha kuwaadhibu kabla ya mambo ya polis. mnapokuwa wengi mtakontrol vipi kias cha kupiga?

na wala sio rahis sana kumkuta mtu anamchuna ngozi binadam mwenzie mkamkamata na kumpeleka kituoni bila 'kumpa adhabu kwanza'

inahitaji moyo kuwapeleka polis kistaarabu jamaa mliowakuta wakitenganisha viungo vya binadamu mwenzao (albino) kwa kisu ili wapate utajir fasta fasta

ni vigumu mno kumfanyia ustaarabu jamaa mwenye maguvu mliemkuta akitoa roho ya bibi yake eti kwa sababu ni mchawi

hapo juu nimeongelea hali halisi ilivyo

cha muhimu zaid zaid si kulaumu jamii inapotoa adhabu. najua kuna kusingiziwa, au kukosea kweli

hao wenye courage ya kufungia watu kwa nje na kupiga kiberit nyumba, watafutaji viungo vya albino, ngozi za binadamu, majambaz ndio wakulaumiwa kwanza katka jamii. mambo wayafanyayo yanaambatana na ukatili usio kifani kwa binadamu. wasipokuwepo hakuta kuwa na 'ogelea kwa moto'. anyway. maisha ya binadamu yeyote ni very precious. na wala maisha ya mtu hayawez lipwa kwa maisha mengine kupotea
 
Back
Top Bottom