Watoto matumbo nje, na Kikwete kazi kucheka tu tangu asubuhi hadi jioni! Wewe ni baba, wewe ni mama, Tanzania ni familia yako - watoto matumbo nje, hawatoi haja kubwa, hawakojoi, hawana pa kujisitiri mvua, wewe unajiita raisi!
Kwanini mfanyakazi wa chama au serikali anayeishi Dar es salaamu, aendeshe gari kubwa la Shilingi za kitanzania Milioni 100 wakati angeweza kutumia KISUZUKI tu, kikafanya kazi ile ile ya kumpeleka kazini na nyumbani kwa shilingi milioni 25, na hizo 75 zilizobaki zikatumika kubadilisha hali ya hao watoto! Jamani! Watoto matumbo nje, lakini kazi ya Raisi ni nini - kuwacheka tu! Kama Uraisi ndiyo huo, mimi siutaki Baki nao Bwana kwani siku itafika, wewe na hoa mafidhuli wenzako mtawajibishwa na Maulana wa Utaala! Hayo mliyojilimbikizia hayatawafaa hata kwa mdhamani, kwani yote yatabaki hapa hapa! Hii inatia uchungu na huzuni sana!