LONGIDO: Mgombea wa CCM apokelewa kwa shangwe, vifijo na nderemo kwa msafara mkubwa wa magari

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
MJI wa Longido na vitongoji vyake juzi ulirindima kwa zaidi ya saa mbili kwa vishindo vya maandamano ya magari na waenda kwa miguu yaliyojaa shangwe na nderemo za honi za magari na maneno ya kejeli kutokana na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo, Dk Stephen Kirushwa kuwasili katika mji huo kwa msafara mkubwa wa magari.

Dk Kirushwa aliyembwaga aliyekuwa Mbunge wa Longido kwa tiketi ya Chadema, Onesmo Ole Nangole aliyepinga katika Mahakama Mahakama ya Rufaa kuvuliwa ubunge, aliwasili kwenye Uwanja Mdogo wa Ndege wa Arusha uliopo katika mji wa Kisongo saa 6.05 mchana, alipokewa na umati wa watu wa mji wa Longido wakiongozwa na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa wilaya hiyo.

Msafara wa magari zaidi ya 75 ulianza kuondoka uwanjani hapo saa 7.35 mchana kwenda Longido na kufunga barabara ya Arusha hadi Namanga kwa zaidi ya saa mbili hadi kufika mjini humo na kupokewa na maelfu ya watu wakiwemo wanaCCM waliokuwa tayari kumpokea kwa miguu na kuzunguka mji wote wa Longido.

Akizungumza na wananchi wa Longido, Dk Kiruswa alisema wananchi wa jimbo hilo walikosa mwakilishi kutokana na tamaa ya mtu ya kutaka madaraka kwa kupora na siyo kwa kuchaguliwa na wakazi wa jimbo hilo.
Alisema mahakama imeliona hilo na kuamua kutengua ushindi wake alioupata kwa njia haramu na kuwataka wakazi wa Longido kuwa wavumilivu hadi siku maalumu itakapotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Alisema, “tunataka kufanya uchaguzi wa Jimbo la Longido kwa ustaarabu mkubwa ikiwa ni pamoja na kutotukanana, kashfa, kubaguana na kutengana kwa dini ama rangi au kabila kwa kuwa wakazi wote wa Longido ni watu waelewa na makini watajua pumba na mchele na kuchagua kiongozi bora na siyo bora kiongozi.”

“Tusubiri filimbi tume ya uchaguzi ya kuanzishwa pambano la uchaguzi wa Jimbo hili la Longido ili tuoneshe umma kuwa wana longido walidhulumiwa kwa muda wa miaka miwili bila ya kosa kwa tamaa ya mtu ya kutaka madaraka kwa nguvu,” aliongeza Dk Kiruswa.

Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Juma Simba “Gaddafi” alisema wakati umefika wa kuwaumbua wasaliti wa chama kwa kujifanya wanaCCM mchana na usiku wako upinzani. Gaddafi alisema hilo halitavumiliwa kwa uongozi uliopo ndani ya chama katika wilaya hiyo na kuwataka wanaCCM wote kuwa wamoja na uchaguzi ukitangazwa kufanya kweli ikiwa ni pamoja na kuwabwaga wapinzani kwa kura nyingi na za kishindo ili wasipate kisingizio
 
Hao waliompokea ni Nazwazwa yanapelekwa kwa ushabiki hayajui kesho yao, nchi imekuwa mbaya haina muelekeo biashara zinafugwa,watu wamepoteza hata matumaini ya kujua kesho yao Leo unaifurahia ccm,kweli mapunguani hayaishi Tanzania yetu hii.
 
Hapa ndo huwa naungana na watu kuwachukia Polisi.

ACHA nikae KIMYA...!
 
Jimbo linarudi CCM
Hata Batlida Buriani na Monaban walikuwa na misafara ya magari hadi 150 ila siku ya matokeo hawakuamini huo ndio mkoa wa Arusha kesho kutwa msije lia lia hapa jukwaani maana msafara wa magari haupigi kura
 
MJI wa Longido na vitongoji vyake juzi ulirindima kwa zaidi ya saa mbili kwa vishindo vya maandamano ya magari na waenda kwa miguu yaliyojaa shangwe na nderemo za honi za magari na maneno ya kejeli kutokana na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo, Dk Stephen Kirushwa kuwasili katika mji huo kwa msafara mkubwa wa magari.

Dk Kirushwa aliyembwaga aliyekuwa Mbunge wa Longido kwa tiketi ya Chadema, Onesmo Ole Nangole aliyepinga katika Mahakama Mahakama ya Rufaa kuvuliwa ubunge, aliwasili kwenye Uwanja Mdogo wa Ndege wa Arusha uliopo katika mji wa Kisongo saa 6.05 mchana, alipokewa na umati wa watu wa mji wa Longido wakiongozwa na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa wilaya hiyo.

Msafara wa magari zaidi ya 75 ulianza kuondoka uwanjani hapo saa 7.35 mchana kwenda Longido na kufunga barabara ya Arusha hadi Namanga kwa zaidi ya saa mbili hadi kufika mjini humo na kupokewa na maelfu ya watu wakiwemo wanaCCM waliokuwa tayari kumpokea kwa miguu na kuzunguka mji wote wa Longido.

Akizungumza na wananchi wa Longido, Dk Kiruswa alisema wananchi wa jimbo hilo walikosa mwakilishi kutokana na tamaa ya mtu ya kutaka madaraka kwa kupora na siyo kwa kuchaguliwa na wakazi wa jimbo hilo.
Alisema mahakama imeliona hilo na kuamua kutengua ushindi wake alioupata kwa njia haramu na kuwataka wakazi wa Longido kuwa wavumilivu hadi siku maalumu itakapotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Alisema, “tunataka kufanya uchaguzi wa Jimbo la Longido kwa ustaarabu mkubwa ikiwa ni pamoja na kutotukanana, kashfa, kubaguana na kutengana kwa dini ama rangi au kabila kwa kuwa wakazi wote wa Longido ni watu waelewa na makini watajua pumba na mchele na kuchagua kiongozi bora na siyo bora kiongozi.”

“Tusubiri filimbi tume ya uchaguzi ya kuanzishwa pambano la uchaguzi wa Jimbo hili la Longido ili tuoneshe umma kuwa wana longido walidhulumiwa kwa muda wa miaka miwili bila ya kosa kwa tamaa ya mtu ya kutaka madaraka kwa nguvu,” aliongeza Dk Kiruswa.

Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Juma Simba “Gaddafi” alisema wakati umefika wa kuwaumbua wasaliti wa chama kwa kujifanya wanaCCM mchana na usiku wako upinzani. Gaddafi alisema hilo halitavumiliwa kwa uongozi uliopo ndani ya chama katika wilaya hiyo na kuwataka wanaCCM wote kuwa wamoja na uchaguzi ukitangazwa kufanya kweli ikiwa ni pamoja na kuwabwaga wapinzani kwa kura nyingi na za kishindo ili wasipate kisingizio
maandano yanaruhusiwi kwa chama tawala tuu hao wengine ni hawarusiwi?
 
Back
Top Bottom