Loliondo, OBC, Dowans: The disturbing connection and secrets

Loliondo, OBC, Dowans: The disturbing connection and secrets

Hili bandiko sio geni hapa jamvini...

Mimi nasema "Loliondo iliuzwa mwaka 1992".

Kuna jamaa juzi kwenye Tanzania Daima Jumapili alisema kwenye makala kwamba na Mzee Ruksa alifanya madudu wakati wa awamu yake mojawapo ni hili la Loliondo! Nchi hii inamwitaji "Rawlimgs" wa kusafisha uoza kabla atujampata "Nyerere" mwingine. OOh lalal!
 
Hakuna cha ajbu, hayo ni mambo ambayo yalikuwepo, yapo na yanakuja, ndani ya nchi yetu kuna sehemu ambazo tutakuwa hatuwezi kuzigusa kwa sababu wageni wamepakalia.

Siasa chafu, uongozi mbaya na ubinafsi ndo vinatuangamiza.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
 
mbona sio mara ya kwanza kusikia haya,inamaana rais hajasikia au ndo ile imani tuliyonayo ya kuwa tuna rais kivuli asiyeweza kuchukua hatua katika mambo mazito.Lakini mbona hili jepesi?Hivi unaweza kuingia eneo lolote falme za kiarabu ukakuta unakaribishwa united states of america au nchi nyingine yoyote? Hizi dharau za nchi wawekezaji ambao wamegeuka wachukuaji zitaisha lini?Huu upumbavu mpaka lini?
 
Kama ni laana basi aliyetulaani kafa. leo nasoma gazeti moja nashitushwa na habari hii ya ajabu mwarabu eti anahamishia majina ya kwao na kuleta kwenye inchi yetu. hata mtandao unakukaribisha Eti karibu kwenye jumuiya ya kiarabu jamani haya si matusi? tena ya nguoni baba gani bora atakubali adhalilishwe nyumbani kwake mbele ya mke wake? serikali inauza nchi kwa kisingizio eti uwekezaji.

Tukumbuke mwaka fulani jamaa mmoja mfaransa alianika maovu ya serikali ya tanzani kupitia filamu ya Darwins nightmare alikemewa vibaya huyu aliianika tanzania nje ya nchi ila anachofanya muarabu huyu ni kutudhalilisha tuwamo ndani mwetu wenyewe serikali gani inaweka maslai ya wawekezaji kuliko sisi tuliowapigia kura? mbona mnatusaliti hivi?

Je wamasai sio watanzania au Mwarabu huyo wa emirates ni wa muhimu kuzidi mmasai mtanzania? Na hao walinzi wanaowauwa watanzania wenzao sio wazalendo unatumwa uue mtanzania mwenzio kwa pesa umelaaniwa wewe umtegemeae mwarabu huyo muuaji akifukuzwa tanzania ukaolewe naye uarabuni huko! mi nashauri kuwa huyo mwekezaji mnunua nchi afukuzwe mara moja kama mtashindwa kumtoa mmekwisha!serikali gani haijali wale waliowapigia kura na kuanza kujali misala ipitayo au hao mtawapa uraia mwakani?

Sijui ili wawachangie vizuri fedha za kampeni baadaye muwalipe fadhila kwa kuwasamehe kodi ili nchi ipate hasara ya mamilioi jifunzeni Japan ona wachina kibao wanafanya biashara feki mabalozi wao wapo tuu viongozi wetu wako kimya hivi mnajisikiaje misaada ya uwanja tumejenga kwa fedha yetu au mkapa unasemaje? Ifike muda viongozi mjue kua tutakapo uza nchi nyie mtaishi wapi au sauzi mlikojenga makasri yenu nihayo tuu

Nakiamini ninachosema niko tayari kukifia hata kwenda msituni kwa ajili ya hicho
 
Li nchi halina mwenyewe, kwa nini ameruhusiwa kuwa na network yake ndani ya nchi nyingine?? kwa hiyo hata wanan usalama wetu ni mbumbumbu au kwa kuwa ni mradi wao basi??

Tanzania haina muda mrefu tutapigana, hivi hata wanajeshi wetu!, sijui yameridhika??
 
hivi kikwete kweli hujui kwamba mwarabu anamtandao wake wa mawasiliano ya mija kwa moja hadi dubai?? Na kama umemruhusu unaona ni sahihi?? Ndege za uwezo wa kubeba tani 200 zinatua pale liliondo zinabeba wanyama hivi wakiisha mtabeba makalio yenu??
 
hivi kikwete kweli hujui kwamba mwarabu anamtandao wake wa mawasiliano ya mija kwa moja hadi dubai?? Na kama umemruhusu unaona ni sahihi?? Ndege za uwezo wa kubeba tani 200 zinatua pale liliondo zinabeba wanyama hivi wakiisha mtabeba makalio yenu??

Mkuu Magezi nimemkandamizia hili swali muungwana sasa sijui kama kutakuwa na mchujo siunajua tena wale viherehere wa pale magogoni wanavyopenda kujikomba kwa Muungwana.

Nimetwanga na maswali matatu mazuri sana kuhusiana na General Tyre.Tatizo hakuna umeme labda ni mkakati wa watu wa usalama kuhakikisha muungwana hapati wakati mgumu.Anyway nina kajenerata kangu hapa nyumbani nitakuwa nina waupdate wapiganaji wote through Jamiiforums.

G Kabonde.
Mpiganaji asiyechoka
 
Wazungu wakejeli Serikali ya Kikwete

- Wasema posho zawapofua watendaji
- Wasema inajali wawekezaji kuliko raia

Waandishi Wetu
Raia Mwema
Septemba 9, 2009


SURA ya Tanzania katika duru za kimataifa imeanza kuchafuka na sasa vyombo vya habari, hususan magazeti barani Ulaya, yameanza kuielezea Tanzania katika tafsiri ambayo ni kinyume cha juhudi za maofisa wa serikali kuinadi kwa madhumuni ya kuvutia zaidi wawekezaji.

Miongoni mwa mambo yanayoandikwa na vyombo hivyo yakiwamo magazeti ya The Guardian, Economist na Financial Times, ni pamoja na urasimu unaokwaza wawekezaji, maofisa wa serikali kupenda posho, serikali kukumbatia wawekezaji dhidi ya wananchi katika baadhi ya maeneo na kusuasua kuingia katika Shirikisho la Afrika Mashariki.

Magazeti hayo yamechapisha taarifa kuhusu Tanzania katika matoleo yake ya hivi karibuni kati ya Julai na Septemba mwaka huu likiwamo gazeti la Financial Times lililonukuu maofisa wa kampuni moja ya uwekezaji iliyokusudia kujenga kiwanda cha dawa jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa habari iliyoandikwa na gazeti hilo, inaelezwa kuwa wakati Kamal Kotecha alipoanza mazungumzo ya kujenga kiwanda cha dawa mjini Dar es Salaam ambacho kingezalisha dawa bora na kukuza uchumi, mamlaka zilimhakikishia kwamba dawa hizo zingeidhinishwa ndani ya miezi mitatu.

Leo, zaidi ya mwaka mmoja na nusu na uwekezaji wa dola za Marekani milioni 13, Kotecha bado anasubiri kibali hicho kutoka.

"Huwezi kuwaona maofisa au kupata uamuzi. Siku zote wako katika mikutano," analalama Kotecha, mfanyabisahara Mhindi ambaye amepata kuishi Jamhuri ya Kongo (DRC) mmiliki wa Zenufa Pharmaceuticals.

Anaongeza: "Unaweza kusema ofisi zetu ziko kwa msajili, kwa kuwa kila siku tuna mtu kati yetu anayekwenda katika ofisi yake (kufuatilia).

"Katika Tanzania, moja ya nchi ya Afrika yenye afueni kidogo katika muundo wa sekta ya utendaji, tatizo si rushwa pekee. Ni aina ya mfumo ambao umekuwa kama taasisi, yaani taratibu za kisheria ambazo huchelewesha muda, ambao umehalalishwa na wafadhili na mashirika ya kimataifa. Lakini pengine chimbuko la hali hii ni utamaduni wa malipo ya posho (per diem)".

Malipo ya kila siku kwa maofisa wanaohudhuria mikutano na warsha yanayolenga kulipia gharama za safari, chakula na malazi.

Mtumishi mmoja wa Serikali aliimbia kampuni ya Zenufa kisa cha kampuni hiyo kusubiri kibali kwa mwaka na nusu.

Alisema, ya kuwa msajili wa cheo cha chini hupata mshahara wa dola za Marekani 600 (takriban shs 72,000) kwa mwezi lakini akisafiri au akiwa mkutanoni hupata dola 50 (sh zaidi ya 50,000) za Marekani. Msajili mwandamizi hupata mshahara wa dola za Marekani 2,000 au posho ya siku ya dola 200 za Marekani akiwa katika mikutano na kuongeza;

"Ndiyo maana hawashikiki ofisini. Hali hii ni habari ya kawaida. Msomi mmoja alilipwa posho ya kikao kilichofanyika mita chache kutoka ofisini kwake. Alipohoji ni za nini aliambiwa za mafuta, aliposema kwake ni jirani, akaambiwa wasipolipa hakuna atakayehudhuria. "

Kwa mujibu wa gazeti hilo, mdudu huyu wa posho haishii serikalini tu bali mashirika yasiyo ya kiserikali nayo yanachangia na hayo hualika wataalamu kutoka serikalini na kuwapa posho nono huku wakwavunja moyo wanaobaki ofisini.

Klaus Leisinger, mkuu wa Novartis Foundation, shirika la misaada la Uswizi alipata mara kadhaa kuomba kufadhili kituo cha mafunzo ya afya (Tanzanian Training Centre for International Health) akajikuta akiambulia patupu.

Anasema: " Ilikuwa vigumu kuanzisha malengo makubwa kwa kuwa wafanyakazi walikuwa wakilipwa mishahara ambayo ilikuwa lazima ichangiwe na posho za vikao na safari".

Nalo gazeti la Economist, Septemba 3, mwaka 2009, limeripoti kuhusu kusuasua kwa Tanzania kuingia katika Shirikisho la Afrika Mashariki kwamba, Uganda imepata kupitia mapinduzi na hata wakati mgumu wakati wa utawala wa Milton Obote, yote yakijidhihirisha katika umwagaji mkubwa wa damu wakati wa utawala wa Idi Amin, na vipindi virefu vya ukiukwaji wa haki za raia.

Gazeti hilo limeeleza kwamba chini ya Baba wa Taifa, Julius Nyerere, Tanzania ilichukua siasa ya ujamaa iliyowafanya watu wake wajikokote katika umasikini lakini wakabaki na mshikamano na amani na Kenya ilishamiri kuendana na dunia, lakini yenyewe ikijidhihirisha kwa matendo ya ukosaji amani na rushwa. Sasa Kenya inaweza kuwa isiyo na utulivu kulinganisha na majirani zake.

Kwa mujibu Economist mwaka 1967 Kenya, Tanzania na Uganda ziliunda Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa nia kuanzisha shirikisho lakini hakukuwa na maendeleo ya maana kabla ya jumuiya hiyo kuvunjika mwaka 1977, huku baadhi ya Wakenya wakishangilia, wakifurahi kwamba nchi yao ilikuwa ikiwabeba sana wanachama wengine wa jumuiya.

Hata hivyo, mwaka 1999, mpango huo ulifufuliwa na mwaka 2007 ulipanuka kuzijumuisha Burundi na Rwanda na sasa linaeleza gazeti hilo kwamba wengi wana shaka kama Umoja wa aina ya ule wa Ulaya unaweza kufikiwa katika eneo hili hata kama kuna ahadi ya kuwa na sarafu moja ifikapo mwaka 2015 ili kuwezesha muungano wa forodha kufanya kazi.

Hata hivyo linaeleza kwamba matukio ya hivi karibuni yanaashiria kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kuwa na shirikisho lakini Tanzania ndiyo ambayo mara nyingi imekuwa ikikwamisha mambo yasiende katika EAC, ikihofia kufunikwa na Wakenya na Waganda watafuta ardhi na ambao wanaaminika kuwa na elimu zaidi kulinganisha na Watanzania.

Lakini Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete, sasa anasema hakuna sababu kwa Watanzanua kuendelea kulialia, bali wajiandae kuingia katika soko la pamoja.

Soko la Mitaji Tanzania, ambalo ni dogo, linaamini katika miaka michache ijayo patakuwa na soko la pamoja la Afrika Mashariki. Kazi si mbioni ya kuanzisha mfumo wa biashara ya pamoja.

Kama Tanzania imekuwa ikibaki nyuma, Uganda imekuwa ikichangamkia sana wazo la kuwa na shirikisho, pamoja na mambo mengine, kwa kuwa Rais Yoweri Museveni ana ndoto ya muda mrefu ya kuustafu akiwa rais wa kwanza wa Shirikisho la Afrika Mashariki.

Hata Paul Kagame, Rais wa Rwanda, anaelezwa kwamba anafurahia wazo la kuwa na EAC. Ushirikiano wake wa hivi majuzi na Jamhuri ya Kongo (DRC) unalenga kukuza biashara baina ya nchi hizo kwa kutumia soko kubwa la Afrika Mashariki. Anataka kuwa anasafirisha bidhaa za Kongo, zilizoongezewa thamani Rwanda kupita katika mianya ndani ya EAC.

Na Kongo haina tatizo na maono hayo ya Kagame. China ambayo ndiye mwekezaji mkubwa katika DRC inataka mbao, chuma na madini mengine yasafirishwe kupitia bandari za Afrika Mashariki.

Kwa sababu hiyo, na sababu nyingine, Kenya, kwa upande wake inataka kujenga bandari mpya ya kina kirefu karibu na kisiwa cha Lamu, karibu na mpaka wa Somalia. Kwa ajili hiyo baadhi ya maofisa wa Kenya wanasema mikoko na mazalia ya samaki jirani na mahali itakapojengwa bandari hiyo si masuala ya kuzuia kujengwa kwake.

Wanasema bandari hiyo, kiwanda cha kusafisha mafuta na mji mpya vitawekwa mahali ambako havitavuruga urithi na biashara ya utalii ya Lamu. Matarajio ya baadaye ni kuwa na barabara na reli kwenda Mogadishu, Addis Ababa na Kigali bomba la mafuta likileta mafuta ya Uganda na Sudan Kusini.

Fedha za uwekezaji zitakuja kutoka Kuwait na matajiri wengine kutoka katika nchi za Ghuba, kwa njia hii Afrika Mashariki itaunganishwa kuliko ilivyopata kuwa na soko la pamoja litakuwa na maana zaidi.

Na hakika kwa nini shirikisho la Afrika Mashariki lisipanuke nje ya nchi wanachama wa sasa? Likitazamwa kwa maana ya lugha ya maeneo haya, yaani Kiswahili, malori ya bidhaa yatayokuwa yakitoka katika bandari ya Mombasa na mvutano wa kisumaku unaoufanya mji mkuu Nairobi kuwa kitovu cha shughuli nyingi, Afrika Mashariki inasambaa hadi Ethiopia, inahusisha sehemu za Somalia, sehemu ya mashariki mwa DRC na ukanda kaskazini mwa Msumbiji na na eneo lote la kusini mwa Sudan ambayo inatarajiwa kuwa huru ifikapo mwaka 2011 kama kura za maoni za raia wa eneo hilo zitaamua hivyo.

Kuna watu wapatao milioni 126 katika EAC. Likipanuka watu zaidi ya milioni 120 wataongezeka hiyo ikifanya idadi ya watu zaidi ya mara mbili ya nchi kadhaa ndogondogo katika maeneo mengine ya Afrika, idadi inayotosha kulifanya eneo hilo kuvutia zaidi kwa wawekezaji wa nje na kulifanya kuwa na nguvu zaidi katika majadiliano na dunia nyingine.

Lakini wafanyabiashara wakazi bado wana wasiwasi. Kwao shirikisho linaweza kukwazwa na mgogoro wa kibiashara, mapigano ya kikabila au likabanwa tangu mwanzo na wanasiasa wafanyabiashara wenye uchu na urasimu wa watendaji. Hakika kuna maoni m changanyiko.

Nalo gazeti la The Guardian na The Obsever yote ya Uingereza, yalieleza kuhusu uwekezaji katika mbuga ya Loliondo, kaskazini mwa Tanzania kuwa ni kati ya mifano ya Serikali ya Tanzania kutokana na kuwa na njaa ya "dola za Marekani" inakumbatia zaidi wawekezaji kuliko wananchi wake, na inathamini wanyama wanaovutia watalii wengi kuliko kuthamini wananchi.

Katika machapisho hayo yaliyoandikwa na waandishi waliofika eneo la Loliondo, imewekwa bayana kuwa licha ya malengo ya serikali kujiongezea mapato kutokana na sekta ya utalii, lakini maisha ya wenyeji katika maeneo ya uwekezaji ni duni, na hakuna uhusiano mzuri kati ya wawekezaji na wenyeji.

Kwa mujibu wa habari hizo, wamasai ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakiendeleza utamaduni wao wa ufugaji kwenye ardhi yao, kwa vizazi na vizazi, sasa wanatakiwa kuhama maeneo hayo ili kuwapisha wawekezaji mamilionea, kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao za kitalii.

"Nikiwa katika eneo la umasaini, simu yangu inasoma ujumbe unaonikaribisha katika Jamhuri ya Kiarabu (United Arab Emirates).

"Ni ujumbe unaosema furahia mtandao bora zaidi wa simu na huduma nyingine wa Etisalat," "Furahia uwapo wako hapa Jamhuri ya Uarabuni!"

Ni eneo ambalo wenyeji wamelipachika jina la Uarabuni. Ni eneo yalipo makao makuu ya Shirika la Biashara la Ortelo (OBC), kampuni inayohusika na masuala ya utalii ambayo haijawekwa katika matangazo ya tovuti.

Ilianzishwa mwaka 1993 na Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Uarabuni (UAE) yenye uhusiano wa karibu na familia ya kifalme, Dubai.

Ni kampuni ambayo pamoja na mambo mengine ni mahsusi kwa ajili ya kuwapokea masheikh na mamilionea wa kiarabu ambao hufika Kaskazini mwa Tanzania kupumzika, eneo la Loliondo.

Katika habari iliyoandikwa na gazeti la The Obsever la Uingereza, Loliondo inaelezwa kama eneo la kuvutia ambalo "kutokana na njaa ya dola (fedha) kwa serikali ya Tanzania limetolewa kwa wawekezaji wa kigeni.

"Mkakati wa maendeleo wa Tanzania unaeleza kuwa ni lazima idadi ya watalii wanaotembelea nchi hiyo ifikie watalii milioni moja mwaka 2010.

"Ni dhahiri kuwa maofisa wa serikali wanafanya chochote ili kuhakikisha malengo hayo yanatimia. Takriban robo ya eneo la nchi limetengwa kwa ajili ya kile kinachoitwa hifadhi.

Maili chake kutoka kilima kilichopewa jina la "Uarabuni" kuna shughuli nyingine za kijasiriamali zinazoendelea zikihusisha wajasiriamali wa kiarabu.

Kuna eneo la hekari 12,000 lililotengwa kwa ajili ya hoteli na kupiga kambi kwa watalii. Eneo hilo limetolewa kwa mwekezaji ambaye shughuli zake zinaunganishwa kwa jina la kikampuni la Thomson Family Adventures.

Utoaji wa maeneo hayo umekuwa ukilalamikiwa na wenyeji ambao ni wamasai wakidai hawana maeneo ya kulisha na kunywesha mifugo yao.

Lakini mwekezaji huyo amekuwa akikanusha madai ya wenyeji hao akisema; "Wamekuwa wakipewa huduma ya maji ya visima wakati wa kiangazi." Imeripotiwa kuwa kwa miaka miwili sasa, kumekuwapo na mashambulizi hata ya kutumia risasi kati ya walinzi wa mwekezaji huyo na polisi dhidi ya wenyeji.

Liz McKee, ambaye ni Meneja Mkuu wa shughuli za mwekezaji huyo amenukuliwa akimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa mradi unaokusudiwa kuanzishwa utahifadhi ardhi na wanyama.

Haamini kwamba ni busara kuwaacha wafugaji kuendelea na mfumo wao mkongwe wa maisha uliodumu kwa karne kadhaa.

Hakuna ardhi ya kutosha, sidhani kama wamasai wataendelea na maisha haya ya kufuga kwa kuhama hadi mwisho wa dunia." Anasema mwanamama huyo mwenye asili ya Uingereza.

McKee ni mtu ambaye aheshimu kwa asilimia 100 utamaduni wa kimasadi na hasa unaohusu tabia dhidi ya wanawake ikiwamo ya kuoa watoto wadogo hata wenye umri wa miaka 12.
Ni wazi kuwa sasa utamaduni imara wa wamasai unaanza kunyongwa kisayansi. Serikali ya Tanzania imekuwa karibu zaidi na wawekezaji wa kitalii, huku wamasai wakilalamika kuhamishwa kwa nguvu kwenye makazi yao ya asili.

Taarifa hizi zinanukuu matamko ya wanaharakati nchini kwamba kati ya miezi ya Julai na Agosti, mamia ya wamasai walichomewa nyumba zao za polisi ikiwa ni majibu dhidi ya kile kinachodaiwa kuwa baadhi ya wamasai kuingiza mifugo yao eneo la mwekezaji wa kiarabu.

"Wamasai wanaonekana kuwa wanahitaji katika kupigwa picha na watalii, kubeba mabegi ya watalii, au hata kuwalinda," anasema Moringe ole Parkipuny, ambaye ni mzee wa kimasai aliyewahi kuwa mbunge na kuongeza kuwa; "Siku hizi wanyama wanakuwa na thamani zaidi kuliko watu."

Hapa, wamasai wanatakiwa kuhama kwa amri ya serikali ili kupisha nyati 25 ambao ni kivutio kwa mamia ya watalii ndani ya mbuga ya Ngorongoro.

Ololosokwan ni mkazi wa umasaini ambaye alituhadithia kuhusu uvumi kuwa Sheikh kutoka Dubai atawasili hivi karibuni katika Shirika la Ortelo.

Kumekuwapo na maelezo kutoka kwa wenyeji kuwa kila wanapokuja wageni maarufu kutoka Uarabuni hutandikiwa zulia jekundu. Mwandishi aliyekuwapo huko alitaka kujua kama anaweza kupiga picha na alipowaeleza nia yake hiyo, alijibiwa; "Watu hukamatwa wanapokaribia eneo hilo."

Inaelezwa kuwa kampuni ya OBC imepewa leseni ya kuua simba watano kwa msimu. Lakini swali linakuja nani anayehakikisha idadi hiyo? Anahoji mkazi mmoja wa kijiji jirani na Jamhuri ya Kiarabu, Loliondo.

Waandishi wa habari na watu kutoka Mashirika yasiyo ya Serikali (NGOs) wamekuwa wakipigwa marufuku kufika eneo hilo na hata wenyeji wamekuwa wakionywa na polisi kuwa hata kuzungumzia kwa ubaya kuhusu OBC kutawatia kwenye matatizo.

Mfugaji mmoja wa kimasai alieleza kuwa amekwishawahi kuona mtego wa kutega chui wakiwa hai, ikielezwa kuwa wamepewa kibali hicho na serikali.

Inadaiwa kuwa msimu uliopita wa kiangazi, kijana wa kimasai mwenye umri wa miaka 29 alikufa kutokana na ajali, lakini ilidaiwa kuwa kijana huyo alipigwa risasi na baadaye kugongwa kwa gari ili kuzima joto la vurugu ambalo lingeweza kuibuka kutoka kwa wenyeji.

Hata hivyo, kampuni ya OBC imekuwa ikitoa misaada ikiwamo ya mahindi ili kukabili tatizo la njaa lililokuwa likiwakabili wenyeji. Inaelezwa pia kwamba kampuni iliwahi kutoa shilingi milioni 25 lakini baadhi ya wanavijiji walikataa fedha hizo.

"Hatukushirikishwa wakati waarabu wanapewa maeneo haya," anasema Kirando ole Lukeine, mmoja wa wazee wa kimila na kuongeza kuwa; "Kwa hiyo, kijiji chetu hakitaji msaada wowote kutoka kwao."

Mzee mwingine wa kimasai anasema; "Tunaeleza ni lazima tuitii serikali lakini hizi ni mbinu tu za kutaka kuchukua sehemu nyingine ya ardhi yetu."

Kumekuwapo na madai kuwa maofisa wa serikali wakiwamo baadhi wanaoshughulikia masuala haya wamekuwa na ukwasi wa kupindukia. Takwimu za rushwa zinaonyesha kuwa Tanzania ambayo mwaka 2008 ilikuwa nchi ya 102 kati ya 180 zilizokithiri kwa rushwa, iliambulia dola za Marekani milioni 9.3 mwaka 2002, kutokana na masuala ya uwindaji kwa leseni.

Hata hivyo, taarifa za waandishi wa kigeni zinaeleza kuwa licha ya mapato hayo hali ya umasikini miongoni mwa wenyeji ni duni.

Mchakato wa kuhamisha wafugaji una historia ndefu nchini Tanzania, ikiwa ni mpango ulioanza mwaka 1959, wakati huo mpango huo ukiendeshwa na serikali ya kikoloni kutoka Uingereza.

Baada ya uhuru, mwaka 1961 hifadhi nyingi za taifa zilianzishwa, uanzishwaji ulioambatana na kuhamisha wenyeji kwenye maeneo husika.

Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 70 ya wananchi ni masikini wa kutupwa, na asilimia 15 ya watoto wamekuwa wakipoteza maisha wakiwa na umri chini ya miaka mitano.

Hata hivyo, licha ya takwimu hizo mbaya inaelezwa kuwa idadi ya watalii imekuwa ikiongezeka na hivyo kuongeza mapato ya serikali.

Liz McKee, amekuwa akielezea matarajio yake kama mwekezaji kuwa wenyeji watapata ajira kutokana na kuanza shughuli kwa kampuni anayosimamia, ambayo inatarajiwa kuanza kazi mwakani.

McKee ndiye aliyemwalika mwandishi wa jarida la The Observer kutembelea kampuni yake na kumhoji meneja mwenyeji, Daniel Yamat.

Hata hivyo, kutokana na maelezo hayo ya kupatiwa ajira, mwandishi kabla ya kufuatilia mwaliko huo alitaka kujua maoni ya mwenyeji, Lesingo Ole Nanyoi, kama yuko tayari kupewa ajira, naye alimjibu; hapa, hilo haliwezekani.

Lesingo ambaye ni baba wa watoto wanne akiwa na wake wawili, wakati mwingine amekuwa akilazimika kuuza ng'ombe wake ili kupata fedha za kuendesha familia yake ikiwa ni pamoja na kulipia gharama za matibabu.
 
Mimi naona tumerogwa...Kuna haja ya kubinafisisha hata IKULU

Nyingine hii hapa.....

============================
Associated Press

Loliondo GAME CONTROL AREA, Tanzania - At a dirt airstrip in rural Tanzania, a desert camouflaged cargo plane from the United Arab Emirates air force taxis up to pallets stacked with large coolers full of game meat, the harvest of a successful Hunting season.

As Tanzanian immigration and customs officials fill out documents under a thatched shelter, brand-new, four-wheel-drive trucks and dune buggies drive to and from a nearby luxury campsite, the base for one of Tanzania's most expensive - and secretive - game Hunting operations, Otterlo Business Corp.

Hundreds of members of Arab royalty and high-flying businessmen spend weeks in the Loliondo Game Control Area each year Hunting antelope, lion, leopard and other wild animals. The area is leased under the Otterlo name by a member of an emirate royal family who is a senior officer in the UAE defense ministry.


While neighboring Kenya outlawed big game Hunting in 1978, the Tanzanian government says Hunting is the best use of the land and wildlife. But villagers and herders say big money has led government officials to break all the Hunting rules, resulting in the destruction of most of the area's non-migratory animals and putting East Africa's most famous national parks under threat.

Loliondo is on the main migratory route for wildlife north of Ngorongoro Crater, east of Serengeti National Park and south of Kenya's Masai Mara National Reserve. The summer Hunting season coincides with the migration of wildebeest and zebra through the area, where they eventually cross into the Serengeti and the Masai Mara. Predatory animals follow the migration.

During the colonial era, Loliondo was set aside for European royalty as a Hunting area.
Since independence, Loliondo has remained a Hunting reserve, but it is supposed to be managed by area residents for their benefit.

Local leaders, who refuse to speak publicly because they fear retribution, say they have not been consulted about the lease that was granted in 1995 by national officials in Tanzania's political capital, Dodoma. They say government officials have tried to silence criticism.

"The lease was given by the government and the Maasai landowners were not involved," said one Maasai leader. "All the resident animals have been killed ... (now) they carry out Hunting raids in the Serengeti National Park, but the government closes its eyes."

Maasai warriors told The Associated Press that hunters give cash to anyone who can lead them to big game, especially leopards. They also said that Otterlo officials have begun pumping water into some areas to attract more animals and that what the warriors call suspicious fires in the Serengeti have caused animals to move into Loliondo.


An Otterlo manager, who gave his name only as Khamis, initially agreed to an interview with AP but later did not return repeated phone calls.

In an interview with the newspaper, The East African, Otterlo managing director Juma Akida Zodikheri said his company adheres to Tanzanian law, and he denied hunters killed animals indiscriminately. He said the owner of the company is Maj. Gen. Mohammed Abdulrahim al Ali, deputy defense minister of the UAE.


While Tanzania has strict rules on game Hunting, Maasai who have worked at the lodge say guests are never told of the limits and hunt as much as they want. Tanzanian officials deny that.

Col. A.G.N. Msangi, district commissioner for Ngorongoro District, said all applicable rules are enforced. He accused the Maasai of rumor-mongering in an effort to discredit Otterlo.

The company "is following the system the government wants," Msangi said. "OBC has invested more money here than any other company in the district."


Msangi said Hunting companies request permission to kill a certain number of animals. Once the request is approved by wildlife experts at the Ministry of the Environment, the company pays a fee based on that number whether they actually kill the animals or not, he said.

"We have police and ministry people making sure they don't exceed what they have paid for," Msangi said. The tourists are also required to employ professional hunters to ensure no female or young animals are killed, he added.

Compared to the numbers in Serengeti National Park, very few large animals were seen during a three-hour drive through Loliondo. But without any independent survey of the animal population, it is impossible to know whether Msangi's conservation efforts are working.


Msangi described his main duty as balancing the needs of people, animals and conservation. He said not only does Hunting revenue finance wildlife conservation, but Otterlo, like most tourism companies, also makes charitable donations to help pay for schools and development projects and it provides badly need jobs.

Also appeared in Washington Times, 1 Aug 2002
 
Karibu jamhuri ya kiarabU-Tanzania. what a joke? only in Tanzania, not even Africa
 
Karibu jamhuri ya kiarabU-Tanzania. what a joke? only in Tanzania, not even Africa

in his session yesterday Kikwete mentioned Abudhabi Group financing one the roads.... they must be connected I guess?? Shame.
 
"Wafugaji warudi kwao"- Mhe. Pinda (PM)

Hii kauli mnaionaje ndugu zangu?

Sasa huku wanakowachomea moto si ndio kwao. Hivi serikali ina maana gani mbona kuna uzembe wa hali ya juu sana.
 
Baada ya Kusoma hii story yote, nawapa respect sana wale waasi wa Kule OGONI land Nigeria, hii iliwatesa na sasa wanapigania haki yao, utajiri upo ktk ardhi yao wanaonufaika ni wengine.

Na LOLIONDO wanaonufaika ni waarabu na viongozi wetu. Nakumbuka sana enzi za gazeti la motomoto na hii scandal TOKA leo MZEE Ruksa kwangu ni KIBARAKA kauza nchi na uhuru wa ndugu zetu wamasai NA SASA WANATESEKA katika ardhi yao ya urithi. Niambieni ile SNIPER (AU AK47) inauzwa bei gani nikanunue nataka niwe mfano wa wapigania haki duniani ntamtungua mmoja baada ya mwingine, km wamasai hawako huru basi hata wewe mfipa, mhehe, mmakonde hauko huru, hili Nyerere alilisema hatuwezi kujiita tuko huru wakati nchi nyingine bado zinaendeleza mapambano dhidi ya ukoloni.

Kama kwenye hizo picha za waarabu zinavyoonekana mmoja kashika sniper anauwa mnyama ndivyo mimi ntakavyo CHINJA hawa dhalimu WAARABU. Wote waliosaini mikataba feki hii, sniper lazima iwanuse, kwa nini tudhalilike ktk ardhi yetu wenyewe? watanzania tuache UOGA, nchi inafilisiwa hii tutabaki na mashimo tuu, jangwa na wanyamapori wote watatoweka.

Nawaachia wenyewe muamue, tuendelee kuwa WADANGANYIKA? WATANGA NA NYIKA? AU WEREVU. If there is any rebel group being formed, list my name number ONE!
 
"Wafugaji warudi kwao"- Mhe. Pinda (PM)

Hii kauli mnaionaje ndugu zangu?

Sasa huku wanakowachomea moto si ndio kwao. Hivi serikali ina maana gani mbona kuna uzembe wa hali ya juu sana.


Mhhhhhhh!!!!!!!!!!
Si unajua uchaguzi ni mwakani? Kwama EPA mmeikomalia hivyo wewe unafikiri watapata wapi pesa za kampeni tofauti na kuuza hao wamaasai? Ukoloni ulitoka kwa mlango wa mbele, sasa umerudi kwa mlango wa nyuma (UWEKEZAJI). Viongozi wa nchi hii hawana tofauti kabisa na viongozi wa zamani waliokuwa wanawauza watu kwa shanga na vipande vya nguo. naona shuluhisho la jambo hili ni watu wote wa loliondo wajipange na ktoichagua tena Serekali inayowauza na kwanyanyasa katika ardhi yao.
 
Iliuzwa na kibaraka wa waarabu, Mwinyi, na ndiye aliyejaribu kwa nguvu zote kipindi kile kusilimisha tz, akashindwa. wakiona waarabu tu wanainama wanawaramba miguu,hivi kuna mtu alishawahi kuwaamini waarabu kweli, dunia nzima wanaogopwa.
 
Nasikitika siku hao wanyama wanaowindwa na wengine kusafirisha wakiisha, basi itakuwa zamu ya hao ndugu zotu kuwindwa na kusafirishwa kama watumwa.
 
Baada ya Kusoma hii story yote, nawapa respect sana wale waasi wa Kule OGONI land Nigeria, hii iliwatesa na sasa wanapigania haki yao, utajiri upo ktk ardhi yao wanaonufaika ni wengine. Na LOLIONDO wanaonufaika ni waarabu na viongozi wetu. Nakumbuka sana enzi za gazeti la motomoto na hii scandal TOKA leo MZEE Ruksa kwangu ni KIBARAKA kauza nchi na uhuru wa ndugu zetu wamasai NA SASA WANATESEKA katika ardhi yao ya urithi. Niambieni ile SNIPER (AU AK47) inauzwa bei gani nikanunue nataka niwe mfano wa wapigania haki duniani ntamtungua mmoja baada ya mwingine, km wamasai hawako huru basi hata wewe mfipa, mhehe, mmakonde hauko huru, hili Nyerere alilisema hatuwezi kujiita tuko huru wakati nchi nyingine bado zinaendeleza mapambano dhidi ya ukoloni. Kama kwenye hizo picha za waarabu zinavyoonekana mmoja kashika sniper anauwa mnyama ndivyo mimi ntakavyo CHINJA hawa dhalimu WAARABU. Wote waliosaini mikataba feki hii, sniper lazima iwanuse, kwa nini tudhalilike ktk ardhi yetu wenyewe? watanzania tuache UOGA, nchi inafilisiwa hii tutabaki na mashimo tuu, jangwa na wanyamapori wote watatoweka. Nawaachia wenyewe muamue, tuendelee kuwa WADANGANYIKA? WATANGA NA NYIKA? AU WEREVU. If there is any rebel group being formed, list my name number ONE!


umenena, hili sio jambo la wamasai tu, wachaga wahaya wote by any means necessary lazima tuuonoe huu ufisadi hata kama ni kwa mtutu wa bunduki !Better die a free man rather than live as a slave!
 
Kuna mhusika katuma hii:

Loliondogate 2- become a police project

[...]


The eviction of pastoralist from their home which was conducted by Tanzania police {field force unit} with assistance of private guards anti poachers Otterllo Business Cooperation OBC from 14th July to date, get into another face. The eviction become source of income for police, those who are contacting the operation and those at Loliondo headquqter.
Communities are still suffering, violation of human rights is still going on, Maasai bomas and houses burnt still going on, sticking of innocent people, communities began to become poorer because of the loss of their livestock/cattle due to lack of water and grass, the woman who was raped and his husband are worried of their life, this is because the have been told by the government people to never witness any person if they want survival, and two day ago she refuse to say anything to me and she never went any person to ask that "(tung'wayioki mayieu madamu, kayiew altau lai, emeekure akata ayie oltungani laitadamu, netero orkiyioi, Niache sitaki kukumbuka, nataka niishi, sitaki mtu yoyote tena aniulise, akaanza kulia) leave me along, I don't want to remember, i need my survival, i don't need any person to asked me ever, then start crying"

Since mid August to date, the eviction of pastoralists turn into new face of which one to two people are taken every day to lock up followed by jailed. You can only get released by the police or told no case to answer if you give money to them, most people are giving money to police not because they have done mistake but they are not seeing secured while spending time on lock up or jailed.

The eviction and harassment of the Maasai people is still going on with three vehicles of both Government and Otterlo Business Cooperation guards is now a big income to police who are contacting the operation.
People are courted while grazing their cattle and taken to lock up in loliondo police headquarter and can only released or win if they have money to pay policeman.

Two people courted while walking but released after pay 70,000 T.sh to police.
The numbers of people arrested from 11th August to 17th August are twenty seven as follow.
On August 11th, 2009 at Olorien/Magaiduru village seven people courted in which 5 of them jailed for six month and one released and one penalties 50.000 T.sh.
1.Leken Olosereka
2.Simat Parkisuaa
3.Kiaro Senet
4.Tiambati Mbario
5.saitoti Morise
(all five prisoned for six month but after several weeks of prison they got a legal help from Legal and Human Right Center to appeal and they won the case.)
6.Mosongo orminis (released)
7.shaangwa Lilash (charged penalties of Tsh 50,000)

On 16th August 2009, the at Olorien/ Magaiduru eleven people courted and judgments was as follow.

1.Oldapash Merika
2.Leng'oone Oliaripu
3.Looseli Ledidi
4.Otumoi Morinde
5.Oloomu Seneti
6.Oloomoni Ngoile
7.Ritei Parshuku
8.Mosolwa Kokoi
9.Meikang'a mbeyo (all released at loliondo police station after paying money)

10.Lemao Morise
11. Ole Koipa (the case were continuo listening)

On 17th August 2009 at Soitsambu village nine people were arrested.

1. Kinyanjui Kimeriai
2..Noonyuat Soit
3.Oloning'o Sung'e
4.Nengoone Piando
5.Lemama Yaile
6.Seretui Olorkijape
7.Tumate Rotiken
8..Ngoriaki Kaura
9.Nooliat koipa ( all nine released by police after two day lock up, they paid the police T.sh 600,000 so that they are not taken to court or jailed.


The number of people arrested for first week of September (that is 1st -8th September) are eleven as follow.

On 1st September 2009 two people arrested at Arash village. The case postponed and they are attending the court
1.Loeku Moti
2.Ngoitorito Ngelea

On 4th September, 2009 four people arrested at Ololosokwan village, The police release them after giving money.
1.Kerimas Siololo
2.Sanaet Rotiken
3.Ngidash Parmwat
4.Mangoe Rotiken.

On 6th September, 2009 three people courted at Soitsambu village, they are still attending the court.
1.Munga Rotiken
2.Lengai/Sayadi Mbusia
3.Meipuki Rotiken

On 8th September 2009, two people courted at Soitsambu village and they are still at police lock up since 8th to 10th morning.
1. Karatina Mbusia- an elder of 70yrs old, he was walking on the way to his home
2. Ole Kaigil boy.
The young boys of Olesadera 7 year old run and lose for two days in the bush on the same date of August 8th.

[...]
 
Kama ni laana basi aliyetulaani kafa. leo nasoma gazeti moja nashitushwa na habari hii ya ajabu mwarabu eti anahamishia majina ya kwao na kuleta kwenye inchi yetu. hata mtandao unakukaribisha Eti karibu kwenye jumuiya ya kiarabu jamani haya si matusi? tena ya nguoni baba gani bora atakubali adhalilishwe nyumbani kwake mbele ya mke wake? serikali inauza nchi kwa kisingizio eti uwekezaji.

Tukumbuke mwaka fulani jamaa mmoja mfaransa alianika maovu ya serikali ya tanzani kupitia filamu ya Darwins nightmare alikemewa vibaya huyu aliianika tanzania nje ya nchi ila anachofanya muarabu huyu ni kutudhalilisha tuwamo ndani mwetu wenyewe serikali gani inaweka maslai ya wawekezaji kuliko sisi tuliowapigia kura? mbona mnatusaliti hivi?

Je wamasai sio watanzania au Mwarabu huyo wa emirates ni wa muhimu kuzidi mmasai mtanzania? Na hao walinzi wanaowauwa watanzania wenzao sio wazalendo unatumwa uue mtanzania mwenzio kwa pesa umelaaniwa wewe umtegemeae mwarabu huyo muuaji akifukuzwa tanzania ukaolewe naye uarabuni huko! mi nashauri kuwa huyo mwekezaji mnunua nchi afukuzwe mara moja kama mtashindwa kumtoa mmekwisha!serikali gani haijali wale waliowapigia kura na kuanza kujali misala ipitayo au hao mtawapa uraia mwakani?

Sijui ili wawachangie vizuri fedha za kampeni baadaye muwalipe fadhila kwa kuwasamehe kodi ili nchi ipate hasara ya mamilioi jifunzeni Japan ona wachina kibao wanafanya biashara feki mabalozi wao wapo tuu viongozi wetu wako kimya hivi mnajisikiaje misaada ya uwanja tumejenga kwa fedha yetu au mkapa unasemaje? Ifike muda viongozi mjue kua tutakapo uza nchi nyie mtaishi wapi au sauzi mlikojenga makasri yenu nihayo tuu

Nakiamini ninachosema niko tayari kukifia hata kwenda msituni kwa ajili ya hicho

Manawapigia kura wenyewe, na cha ajabu mtaendelea kuwapigia.

Si unaona hao wamasai wanalalamika sas hivi?
Kaangalie matokeo ya uchaguzi mwakani na utashangaa kuona wamempigia nani.

We nenda kaangalie matokea ya uchaguzi katika sehemu ambazo watu wanalia shida kuliko sehemu zote, maeneo waliovunjiwa nyumba zao, maeneo yenye wizi na ujambazi wa kupindukia, maeneo watu wanalia maji miaka nenda rudi, etc.

Ndio watanzania walivyo.
 
Back
Top Bottom