Loliondo: Kama ni Lowassa tumeliwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Loliondo: Kama ni Lowassa tumeliwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Arafat, Mar 7, 2011.

 1. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Kama ikiwa huyo Mzee wa Umasaaini huko Lolindo ni Mganga wa EL na kuwa kila atakaye kunywa hayo maji yake 2015 huta mwambia lolote juu ya EL, basi tumeliwa tena tuhesabu 2025.

  Napata mashaka makubwa juu ya taarifa zake, napata shida kwanini wizara ya afya haitoi tamko lolote. Kwanini wizara ya afya wasipereke wataalam wao na wagonjwa ili kupata sample za wagonjwa waliopona kwa ajili ya kutoa taarifa elekezi? kwanini serikali imelala!

  Niliwai kusoma kitabu cha Prof.Gabriel Ruhumbuka; Janga kuu la Wazawa, ambaye hajakisoma akitafute, ni riwaya ilitumika sana katika Vyuo vikuu mbali mbali Amerika na nadhani pia ni miongoni mwa vitabu teule Tanzania. Mambo yote yanayofanyika hapa Tanzania mengi yake Ruhumbuka alikwisha yaona katika riwaya. mtunzi anaongelea Ushirikina na madhara yake akitumia Tanzania kama jukwaa la kufikisha ujumbe, utakuta mauhaji kwa imani za kishirikina kama yale ya Albino yalikwisha andikwa na huyu mwana falsafa wa kitanzania, alikuwa UDSM 1970 hadi 1985 kabla ya kuamia USA.

  Siyo kwamba napinga kuwa huyo mzee hana dawa, hapana na uliza kwanini serikali haitoi tamko elekezi kutoka wizara husika ya Afya? ilitujue watu wetu wanaomiminika huko Loliondo kupewa maji wapo salama!

  Hili swala linavyotolewa maelezo si la kiimani tena, maana ukisha kuvuka kuponyesha kwa maombi ukaanza kutoa dozi iwe ya maji au vidonge tayari hiyo siyo Kuponyesha kwa imani ni kuponyesha kwa tiba asilia, kwa kweli hapo siyo imani peke yake.

  Hisije ikawa kama 2005; Kama dawa inatibu lazima itaonyesha katika vipimo vya kitaalam na kama haionyeshi maana yake haitibu huo ndio ukweli. hizi dini sasa zinaweza kutupereka katika uchawi nasi tukatumbukia bila kujua, Mwaka 2005 Askofu wa Katoliki ndie aliyekuwa wa Kwanza kutangaza kuwa Kikwete ni chaguo la Mungu, leo hii imedhiirika ni kazi ya Uchawi na Majini, watanzania kama tumelala hivi mbona tuta-tawaliwa hadi 2105!.

  Kumbukeni ya Kibwetele na ya Makanisa yalioibuka kama uyoga na baade kushiriki biashara ya unga hasa mikoa ya Mbeya, Iringa na Dar es Salaam.
   
 2. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Serkali nayo imekata tamaa kama wananchi wake ndiyo jibu!!:rain:
   
 3. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Kama wamekata tamaa kwanini wasiondoke badala ya kuacha mambo yanafanyika kichwa chini miguu juu kiasi hiki
   
 4. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #4
  Mar 7, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tanzania kama nchi iko ICU ikitoka huko ndio tutaongea vizuri.
   
 5. birungi

  birungi JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kama ingekua ni mipango ya lowassa isingekuja kidizain hii.maana inawalenga wagonjwa tu.
  kweli ruhumbuka alisema mengi ila hili la loliondo wala halijatabiliwa na mwanafalsafa. ni nyakati tu kama zilivyokua za nuhu,luthu na hata kipindi cha farao.
   
 6. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #6
  Mar 7, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  nashindwa kujizuia. Tatizo la serikali yetu ni kutokuwa wabunifu na kuenzi innovations za watu wao. Hapo walitakiwa kutuma jopo la madakitari kuchukuwa sample za dawa, na kutest wagonjwa wanaopewa dawa before na baada ya matubabu ili kujiridhisha scientifically hali ikoje. na kama ni ugunduzi then, kuweza kuu-advance zaidi na mzee mgunduzi kulinda hati milki yake kwa faida ya mgundunzi na nchi. Mwaka mmoja Iringa mtu aligundua namna ya kuzalisha umeme kijijini badala ya tanesco kujifunza, wakamshitaki kuwa anataka kuua watu. Kigoma kijiji cha mgombe na Nyachenda (kasulu) kulikuwa na wazee waliokuwa wanatengeneza bunduki aina mbalimbali za kusasa (siyo magobole); wakamatwa kuwa wataeneza majambazi. Hivyo, bado umuhimu wa kuendeleza local innovations hakuna tanzania, tunaamni katika importations. Lakini localization of innovations na defusion of external inovations ndo imeinyanyua china kiuchumi hadi kuwa hivi ilivyo-ya pili duniani.
   
 7. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #7
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Kumbuka kuwa wanasema huyo mzee anatoa dawa siyo maombi peke yake, ikishakuwa swala la dawa lazima wafuatilie na kutoa Tamko. Nchni kwetu antibiotics zimejaa kila kona watu wanameza hovyo, ebu nenda hata London tafuta prescription ya antibiotics kama utapata? Mpaka Daktari akupime na aridhike sawasawa ndiyo utapewa hiyo dawa.

  Tamko ni muhimu sana ili tuepushe kutokea mambo ya Ushirikina hapa.
   
 8. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #8
  Mar 7, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Mkuu Umenena vyema. Tatizo ni kwamba Serikali yetu imekaa kishabiki shabiki kwenye kila jambo. Usishangae ukienda Ofisini kwa Waziri husika ukaambiwa kuwa naye amefuata dawa Loliondo. Isitoshe nimesikia kuwa kuna hata wakubwa wa Serikali wanaenda huko. Nao wanafuata dawa eti!! Binafsi nimekuwa najiuliza swali kama lako, kwa nini Serikali, kupitia wizara ya AFya isifuatilie na kisha kuweka utaratibu mzuri wa watu kupata hiyo huduma na wakati huo huo kufanya mpango wa kuepusha tabu wanazozipata wagonjwa wanaoenda Loliondo? Manake kwa jinsi nilivyouona msururu unaoelekea kule ni dhairi kuwa kunakuwepo na scrambling kubwa sana ili kuweza "Kupata dawa".

  Kwa mfano, kama wangeweza kufuatilia na kufanya uchunguzi kama ulivyoshauri, wakiridhishwa na matokeo yake wanaweza kumleta huyo mganga Arusha mjini na akajengewa mazingira ya kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na akihitaji kuzifuata dawa zake basi anapewa usafiri maalum kwenda Porini na kurudi Arusha ambako ingewawia rahisi na salama "wateja" wake kumpata.

  Anyway, Serikali yetu ina mapungufu mengi sana yanayochangiwa na uzembe,, hii ni sehemu ndogo tu ya mapungufu yao....
   
 9. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #9
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 974
  Trophy Points: 280
  Nadhani yule babu akihama kule Loliondo basi ile dawa haitafanya kazi. Kuhusu kuifanyia uchunguzi, wanasema hiyo dawa ukiondoka nayo mbali ya maeneo yake inakuwa haifanyi kazi inayotakiwa.
   
 10. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #10
  Mar 7, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna jamaa zangu walienda huko mmoja alikuwa vidonda vya tumbo baada ya kunywa hiyo dawa ndani ya nusu saa akawa amepona pia kuna mwingine mguu na Nkomo vilikufa ganzi akiwa njiani kutoka huko alishangaa mkona ukaanza kupona kesho yake mguu na mkono vikapona mwingine alipeleka watu yeye ni dereva wa tours aliamua kunywa alishangaa alikuwa anavaa miwani akawa haoni vizuri Alivua anaona ameacha kabisa kivas miwani hao nimeona kwa macho yangu.
   
 11. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #11
  Mar 7, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  The best CRAP 2011 from the Best CRAPER 2011!
   
 12. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #12
  Mar 7, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  [​IMG]

  Vipi na wanaochekacheka kama huyu wanatibiwa? Maana anachekacheka kama leader flani hapa nchini. Loh!!
   
 13. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #13
  Mar 7, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hahaaaaaaaaa haiwahitokea.
   
 14. A

  Adaha Member

  #14
  Mar 7, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Viongozi wa Serikali hawawezi kuchukua hatua ya kuichunguza dawa hii kwa sababu wengi wametumia. Pia dawa hii ukitoka nayo nje ya eneo la babu inageuka kuwa maji ya kawaida na ukiiba inageuka kuwasumu, ukijihudumia mwenyewe inakuwa maji ya kawaida.
  Miujiza haiwezi kufanyiwa utafiti wa kimaabara. Siku babu atapokosea masharti ya dawa hii basi ndiyo itakuwa mwisho wa tiba. hata akifa basi na tiba hii itakuwa mwisho wake. Nabii Mussa alipiga bahari na fimbo maji yakaachia njia, alipiga mwamba maji yakatoka. uwezo huu alipewa yeye peke yake na mungu kwa wakati ule.
   
 15. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #15
  Mar 7, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Kaka raisi ameenda huko na mawaziri wake wewe unategemea nini???
   
 16. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #16
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hoja ni EL, huyo mchungaji au uraisi 2015 ?

  Naomba nikueleze huyu EL ni wa pale monduli,nje kidogo tu ya arusha town! Ni umbali wa km 350 mpaka loliondo;kwaio kwangu sioni uhusiano wa huyu mchungaji na EL.

  Kwa wale wanaoamini,hili jambo la huyu mtu kuponya ni kweli kabisa. Sioni sababu ya serkali kuzuia watu kuponywa? Labda kama wewe mwenye hoja ni kakobe ambae kanisa lake waumini wamepungua baada ya wengi kumiminika huko loliondo!

  Kama unaamini mashetani,nakupa pole na ushindwe.
   
 17. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #17
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Kwanini Mkuu?
   
 18. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #18
  Mar 7, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,274
  Trophy Points: 280
  mzee mwenyewe anaeponya huyu hapa.

  198708_205145842829764_100000030499659_818565_2519222_n.jpg
   
 19. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #19
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Nashukuru sana Mkuu kama nawe umeona tatizo maana nilidhani nipo peke yangu!! Je umemsikia hata mmoja katika nafsi yake? wote wana toa taarifa ni wale walioona aliye pona kabisa sijamsikia hata mmoja kujitokeza kutujuza tunaomba pia ajitokeze basi
   
 20. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #20
  Mar 7, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280

  Tusiwe na hofu kiasi hiki cha kuogopa kila kitu kwa kuhisi ni mbinu ya mafisadi kwani itafika mahali tutaogopa hata kula hotelini au kupanda mabasi tukihisi ni ya akina EL na RA
   
Loading...