Lol yamenikuta

Lol yamenikuta

Kwa hali ilivo Anza kuzoe maumivu utakua muhanga muda wote wa maisha yako hauwezi kujiamini!! Kuanza upya si ujinga! Bora Angekua rafiki ila ndugu kabisa utakosa Amani'
 
dah pole kijana ukajua umepata kumbe umepatikana!! But kaa nae ujaribu kumueleza ukweli na ana msimamamo gani kwako maana unaweza ukasema anakupenda kumbe anaempenda zaidi ni uncle
hapo ni kutoka nduki tu ....maana cha kale dhahabu...
 
hapo unatafuta kufa kwa presha bora utafute mtu mwingine x wake ndo awe mkwe wake loh hapo ni kukaribisha majaribu ya kukumbushia zilipendwa.
 
Bwana mtaraji kuoa kama unampenda mchumba wako mwelezee ukweli na endelea na mipango yenu ya kuoana. Mimi imani yangu ni kuwa kila mtu ana PAST yake; sio wote tulioa/kuolewa tumekutana bila kuwa na mahusiano sehemu nyingine. Kwani hawa wake/waumme zetu hawana ex wao??? Na hiyo bado haijazuia watu kuoana.

Mkiamua kuoana mwambie na uncle wako AACHE MAWAZO YAKE YA KUENDELEA na uhusiano na huyo mdada kwakuwa sasa ni MCHUMBA WAKO!!!!
 
hapo ni kutoka nduki tu ....maana cha kale dhahabu...

ni kweli kabisa af kikianza kuwa dhahabu kwa uncle huku kwa mhusika kinafifia guess what...................kujilipua,kulipuliwa,tindikali,kukatana makoromeo,makorodani,kuchinjana ndivyo vitakavyo husika kwa wakati huo,huyu kaka bora amteme tu huyu demu maana huko mbele ni majanga zaidi ya majanga
 
Yaani nauonea huruma huo uhusiano ulio kuwa mzuri kuingia doa. Halafu hakuna mwenye kosa kati ya hao wawili, yaani FATE pekee ndio ya kulaumiwa.

Ila ningekuwa mimi mkaka ningefight for my love n happiness. But you are not me, so go ahead!
 
Kwanza nampongeza huyu dada ni mwaminifu na muwazi sana ila sidhani kama ndoa yako itakuwa na HESHMA mbele ya nduguzo jamaa hata marafiki pale mahusiano waliyokuwa nayo mpenzi wako na uncle wako yatakapobainika!
Cha kufanya ni kumuita uncle wako ukiwa na bibie humfahamishe huyo ndiyo mkeo na upime mwenyewe kwa mda kama atamuheshimu na kukaa mbali naye, na je nduguzo watalichukuliaje kama watafahamu!! maana unaweza kumchukua dada wa watu baadae akafanyiwa vurugu na NDUGUZO.

TAFAKARI SANA KABLA YA MAAMUZI
 
Kaka, upe uhusiano wako muda kidogo, atleast miezi 3-5 uone muenendo wa mkeo mtarajiwa Na huyo mjomba wako, ndio uamue,

Ila for Now just relax,...
 
Back
Top Bottom