'Lockdown' yapendekezwa nchini

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,905
6,691
WAKAZI wa maeneo yaliyo na kiwango cha juu cha maambukizi ya virusi vya corona nchini Tanzania huenda wakafungiwa ndani iwapo serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan itatekeleza kikamilifu mapendekezo ya ripoti ya kamati iliyobuniwa kutathmini ugonjwa wa Covid-19 humo nchini.

Kamati hiyo iliyoongozwa na Prof Said Aboud, inasema kuwa Tanzania tayari imekumbwa na mawimbi mawili na nchi hiyo ya Afrika Mashariki inakabiliwa na hatari ya kuyumbishwa na wimbi la tatu.

Ripoti hiyo, hata hivyo, inaonya kwamba iwapo serikali itafanya uamuzi wa kuwashurutisha watu kutoondoka nyumbani kwa lengo la kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona, ihakikishe kwamba shughuli za kiuchumi hazitatiziki.

“Serikali iendelee kuzingatia mazingira ya Kitanzania katika udhibiti wa ugonjwa wa Covid-19 katika kuamua kuweka au kutokuweka shuruti ya kujifungia na kuwa na ubunifu ili kuruhusu ukuaji wa uchumi na kuimarisha sekta zinazochangia katika uchumi,” inasema ripoti hiyo.

Ripoti hiyo pia inaitaka serikali kutoa takwimu kuhusu uwepo wa ugonjwa wa Covid-19 na kuchukua hatua madhubuti kuimarisha hatua zote za afya za kinga katika ngazi zote ili kuepusha wimbi la tatu la ugonjwa huo.

Ripoti ya kamati hiyo pia inapendekeza kuwa serikali iagize chanjo ya corona kupitia mpango wa kutoa chanjo nafuu kwa nchi maskini (Covax).

Kuhusu tiba za kiasili, kamati hiyo inapendekeza kuwa dawa hizo zitumike lakini sharti ziwe zimethibitishwa kisayansi.

“Kamati inashauri serikali kwa kutumia vyombo vyake iendelee na hatua kuelekea kuruhusu matumizi huru ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 kwa kutumia chanjo zilizoorodheshwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) ili kuwapa fursa ya kinga wananchi wake kwa kuwa kupitia uchambuzi wa Kamati, chanjo hizo zina ufanisi na usalama unaokubalika kisayansi,” inasema ripoti hiyo.

Kamati hiyo inashauri kwamba makundi ya watu walio katika hatari kubwa ya kuambukizwa na corona yapewe kipaumbele chanjo itakapowasili nchini.

“Kipaumbele cha utoaji wa chanjo dhidi ya Covid-19 nchini kwa kuanzia kiwe kwa wahudumu katika vituo vya kutolea huduma za afya na watumishi walio katika mstari wa mbele wa utoaji wa huduma mathalani watumishi sekta ya utalii, hoteli, mipakani, viongozi wa dini na mahujaji.

“Wazee na watu wazima kuanzia umri wa miaka zaidi ya 50 na watu wazima wenye maradhi sugu mengine mathalani kisukari, shinikizo la damu, maradhi ya mfumo wa upumuaji, magonjwa ya figo pia wapewe kipaumbele,” inasema ripoti hiyo.

Iwapo, Rais Suluhu ataamua kutoa agizo la kufunga baadhi ya maeneo ya nchi, atakuwa ameenda kinyume na msimamo wa mtangulizi wake John Pombe Magufuli aliyeaga dunia Machi 17, 2021.

Magufuli alikuwa ameapa kuwa hatafunga nchi na wala hataagiza chanjo ya corona kutoka mataifa ya kigeni.

Chanzo: Taifa leo
 
Tangu kuzuka kwa Corona nchini China mwaka 2019, mataifa mengi duniani yaliamua kuja na mbinu za kupambana na Corona kwa kufungia watu ndani(lockdown) kuvaa barakoa, social distance na mengine mengi ikiwemo Chanjo.

Tanzania tuliamua kuishi na Corona kwa kukataa kujifungia (lockdown) na shughuli ziliendelea kama kawaida na watu wakisafiri huku na huko, hata watalii kipindi cha Corona walikuwa wengi sana Tanzania.

Baada ya miaka miwili kupita tangu Corona izuke mataifa yaliyoongoza kwa vifo ni Marekani, China, India Brazil etc hayo mataifa ni tajiri yana mitungi ya oxygen mingi ,wana barakoa, na walijifungia.

Tanzania chini ya hayati rais Magufuli tuliamua kutumia njia za asili kama kunywa juice ya Tangawizi na malimao, kupiga nyungu na kumtanguliza Mungu mbele etc na matokeo yake impact ya Corona ni ndogo sana na tuliweza kuingia uchumi wa kati.

Cha kusikitisha baada ya miaka 2 ya Corona kupita ,tume iloyoundwa na rais Samia Suluhu licha ya hiyo kamati kujaa maprofesa wa afya inataka kutuaminisha kwamba watanzania si lolote si chochote na tunatakiwa tujifunze kwa waliofanya lockdown huko nchi za nje.!!!
Lakini ukweli ni kwamba ukipima impact ya Corona Tanzania inaonyesha tumefanikiwa sana na tulitakiwa tujivunie haya mafanikio hadharani na kuitaka dunia ije ijifunze Tanzania mbinu tulizotumia.

Hivi sisi watanzania nani aliyeturoga? Pamoja na ushahidi wote uliotuzunguka ukionyesha tumefaulu vita ya Corona bado maprofesa wetu wanataka tufanye kama walivyofanya India, Marekani, Rwanda?

Na Chadema nao wanashangilia?
 
Unaemsifia na safu yake wako wapi akili ya ulozi hii..
Mungu hadhihakiwi Corona haina mkubwa ..

Corona haina Chama
 
Tume iliyoundwa viongozi wa Dini hakuna, huu utawala tumekwisha. Viongozi wa Dini hawakubaliki
 
Hebu tuanze Kutaja hapa chini Majina ya Wajumbe wa Kamati Maaalum ya COVID 19 ili lolote Likitokea tujue chanzo ni wao Naomba mnaowajua muweke orodha hapa;
1.
2.
3.
4........
 
Tangu kuzuka kwa Corona nchini China mwaka 2019, mataifa mengi duniani yaliamua kuja na mbinu za kupambana na Corona kwa kufungia watu ndani(lockdown) kuvaa barakoa, social distance na mengine mengi ikiwemo Chanjo.

Tanzania tuliamua kuishi na Corona kwa kukataa kujifungia (lockdown) na shughuli ziliendelea kama kawaida na watu wakisafiri huku na huko, hata watalii kipindi cha Corona walikuwa wengi sana Tanzania.

Baada ya miaka miwili kupita tangu Corona izuke mataifa yaliyoongoza kwa vifo ni Marekani, China, India Brazil etc hayo mataifa ni tajiri yana mitungi ya oxygen mingi ,wana barakoa, na walijifungia.

Tanzania chini ya hayati rais Magufuli tuliamua kutumia njia za asili kama kunywa juice ya Tangawizi na malimao, kupiga nyungu na kumtanguliza Mungu mbele etc na matokeo yake impact ya Corona ni ndogo sana na tuliweza kuingia uchumi wa kati.

Cha kusikitisha baada ya miaka 2 ya Corona kupita ,tume iloyoundwa na rais Samia Suluhu licha ya hiyo kamati kujaa maprofesa wa afya inataka kutuaminisha kwamba watanzania si lolote si chochote na tunatakiwa tujifunze kwa waliofanya lockdown huko nchi za nje.!!!
Lakini ukweli ni kwamba ukipima impact ya Corona Tanzania inaonyesha tumefanikiwa sana na tulitakiwa tujivunie haya mafanikio hadharani na kuitaka dunia ije ijifunze Tanzania mbinu tulizotumia.

Hivi sisi watanzania nani aliyeturoga? Pamoja na ushahidi wote uliotuzunguka ukionyesha tumefaulu vita ya Corona bado maprofesa wetu wanataka tufanye kama walivyofanya India, Marekani, Rwanda?

Na Chadema nao wanashangilia?
Daaah naona picha mbaya sana ya vifo inakuja tuombe sana Mungu abatilishe hili
 
Bora tutumie njia nyingine kwenye udhibiti wa kuenea kwa ugonjwa, lockdown italeta majanga mengine hapo baadae, italeta janga la njaa maana wananchi walio wengi wanategemea biashara wanazofanya kila siku na pia nchi kuingia kwenye madeni makubwa kutoka kwenye makampuni yalioingia nayo mikataba ya miradi ya kimaendeleo.
 
Loki dauni ni ndoano moja hatari sana hasa kwa nchi kama yetu ambapo familia nyingi hazina hifadhi ya chakula hata cha siku tano n.k

Unapowafungia watu ndani unatengeneza Matatizo makuu mawili moja ni kushusha kinga za mwili ambapo watakuwa wanashambuliwa na magonjwa kirahisi huku taifa litahitaji kununua madawa ilikuwapa/kuwauzia raia.
Pili utawatengenezea hali ya kuhitaji kutoka nje kwa mkupuo endapo shida zita zidi.

Binafsi siungi mkono hoja ya kuwafungia watu ndani....

Tuendelee kuishi kwa taadhari tu na kufuata taratibu za awali....
Hizo chanjo wanazopendekeza sio za kuzikurupukia chanjo inaugumu wake hasa kwenye kwenye ufanyaji kazi wake inategemea jotoridi husika mfano 20c endapo itasafirishwa na jotoridi kubadilika jua umeshatengeneza kitu kingine kabisa ambacho mtu akichanjwa yaweza kutengeneza kitu kingine tofauti na kinga kusudiwa....
 
WAKAZI wa maeneo yaliyo na kiwango cha juu cha maambukizi ya virusi vya corona nchini Tanzania huenda wakafungiwa ndani iwapo serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan itatekeleza kikamilifu mapendekezo ya ripoti ya kamati iliyobuniwa kutathmini ugonjwa wa Covid-19 humo nchini.

Kamati hiyo iliyoongozwa na Prof Said Aboud, inasema kuwa Tanzania tayari imekumbwa na mawimbi mawili na nchi hiyo ya Afrika Mashariki inakabiliwa na hatari ya kuyumbishwa na wimbi la tatu.

Ripoti hiyo, hata hivyo, inaonya kwamba iwapo serikali itafanya uamuzi wa kuwashurutisha watu kutoondoka nyumbani kwa lengo la kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona, ihakikishe kwamba shughuli za kiuchumi hazitatiziki.

“Serikali iendelee kuzingatia mazingira ya Kitanzania katika udhibiti wa ugonjwa wa Covid-19 katika kuamua kuweka au kutokuweka shuruti ya kujifungia na kuwa na ubunifu ili kuruhusu ukuaji wa uchumi na kuimarisha sekta zinazochangia katika uchumi,” inasema ripoti hiyo.

Ripoti hiyo pia inaitaka serikali kutoa takwimu kuhusu uwepo wa ugonjwa wa Covid-19 na kuchukua hatua madhubuti kuimarisha hatua zote za afya za kinga katika ngazi zote ili kuepusha wimbi la tatu la ugonjwa huo.

Ripoti ya kamati hiyo pia inapendekeza kuwa serikali iagize chanjo ya corona kupitia mpango wa kutoa chanjo nafuu kwa nchi maskini (Covax).

Kuhusu tiba za kiasili, kamati hiyo inapendekeza kuwa dawa hizo zitumike lakini sharti ziwe zimethibitishwa kisayansi.

“Kamati inashauri serikali kwa kutumia vyombo vyake iendelee na hatua kuelekea kuruhusu matumizi huru ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 kwa kutumia chanjo zilizoorodheshwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) ili kuwapa fursa ya kinga wananchi wake kwa kuwa kupitia uchambuzi wa Kamati, chanjo hizo zina ufanisi na usalama unaokubalika kisayansi,” inasema ripoti hiyo.

Kamati hiyo inashauri kwamba makundi ya watu walio katika hatari kubwa ya kuambukizwa na corona yapewe kipaumbele chanjo itakapowasili nchini.

“Kipaumbele cha utoaji wa chanjo dhidi ya Covid-19 nchini kwa kuanzia kiwe kwa wahudumu katika vituo vya kutolea huduma za afya na watumishi walio katika mstari wa mbele wa utoaji wa huduma mathalani watumishi sekta ya utalii, hoteli, mipakani, viongozi wa dini na mahujaji.

“Wazee na watu wazima kuanzia umri wa miaka zaidi ya 50 na watu wazima wenye maradhi sugu mengine mathalani kisukari, shinikizo la damu, maradhi ya mfumo wa upumuaji, magonjwa ya figo pia wapewe kipaumbele,” inasema ripoti hiyo.

Iwapo, Rais Suluhu ataamua kutoa agizo la kufunga baadhi ya maeneo ya nchi, atakuwa ameenda kinyume na msimamo wa mtangulizi wake John Pombe Magufuli aliyeaga dunia Machi 17, 2021.

Magufuli alikuwa ameapa kuwa hatafunga nchi na wala hataagiza chanjo ya corona kutoka mataifa ya kigeni.

Chanzo: Taifa leo
Ila Jiwe lilikuwa na misimamo mikali kwelikweli,lilikuwa linawazidi mpaka ISIS & Alquider combined
 
Tangu kuzuka kwa Corona nchini China mwaka 2019, mataifa mengi duniani yaliamua kuja na mbinu za kupambana na Corona kwa kufungia watu ndani(lockdown) kuvaa barakoa, social distance na mengine mengi ikiwemo Chanjo.

Tanzania tuliamua kuishi na Corona kwa kukataa kujifungia (lockdown) na shughuli ziliendelea kama kawaida na watu wakisafiri huku na huko, hata watalii kipindi cha Corona walikuwa wengi sana Tanzania.

Baada ya miaka miwili kupita tangu Corona izuke mataifa yaliyoongoza kwa vifo ni Marekani, China, India Brazil etc hayo mataifa ni tajiri yana mitungi ya oxygen mingi ,wana barakoa, na walijifungia.

Tanzania chini ya hayati rais Magufuli tuliamua kutumia njia za asili kama kunywa juice ya Tangawizi na malimao, kupiga nyungu na kumtanguliza Mungu mbele etc na matokeo yake impact ya Corona ni ndogo sana na tuliweza kuingia uchumi wa kati.

Cha kusikitisha baada ya miaka 2 ya Corona kupita ,tume iloyoundwa na rais Samia Suluhu licha ya hiyo kamati kujaa maprofesa wa afya inataka kutuaminisha kwamba watanzania si lolote si chochote na tunatakiwa tujifunze kwa waliofanya lockdown huko nchi za nje.!!!
Lakini ukweli ni kwamba ukipima impact ya Corona Tanzania inaonyesha tumefanikiwa sana na tulitakiwa tujivunie haya mafanikio hadharani na kuitaka dunia ije ijifunze Tanzania mbinu tulizotumia.

Hivi sisi watanzania nani aliyeturoga? Pamoja na ushahidi wote uliotuzunguka ukionyesha tumefaulu vita ya Corona bado maprofesa wetu wanataka tufanye kama walivyofanya India, Marekani, Rwanda?

Na Chadema nao wanashangilia?
Hoja yako ina mashiko na inahitaji tafakuri na kujihadhari na kuigaiga. Ni muhimu kuzingatia mazingira na hali halisi ya maisha yetu.

Tusiipinge sana ripoti na pia tusidharau njia zetu zilizotufikisha hapa, ikiwemo kumtumaini Mungu.
 
Mapendekezo tu haya wakuu, ila kwa lock down tutazaliana sana tena sanaa
Fafanua hapa kwenye 'kuzaliana Sana'

me nijuavyo kitakwimu Tanzania ina vijana na watoto wengi zaidi kuliko watu wazima na wazee.sasa km vijana ni wengi,vijana haohao wengi wetu hatujaoa na hatukai na wanawake,haya tuambie tunazaliana vipi sasa kukiwa na lock down..labda iseme kutakuwa na ongezeko la upingaji wa punyeto
 
Back
Top Bottom