Mkandaara umenena, maana utafutaji unaozungumzwa si kama ule "rasmi" wao wanachofanya ni kuweka mazingira "ikiwa watamhitaji" iwe kazi rahisi. Hiyo ni kama wanataka kutenda haki, lakini jambo baya kuliko yote ni kwamba HAWAMTAFUTI kwa kheir wala kwa MASLAHI YA WATANZANIA... Hilo ni zito kulizungumza lakini kwa kawaida kama walitaka, MArekani hata kama haikusema, kuna utaratibu wa kawaida kwa kutumia mikataba ya kimataifa kubadilishana watuhumiwa/washitakiwa.
Mikataba hiyo inatengenezewa sheria na kwa kawaida ni lazima kuwapo kesi katika mahakama za nyumbani (Mfano Kisutu) ambayo itatoa ombi la kutaka kurudishwa kwa mtuhumiwa na ombi hilo lazima lionyeshe maelezo ya mahakamani yanayoonyesha dhahiri kuwapo kwa kesi inayoweza kusikilizwa kwa maana kuwepo kwa ushahidi wa kutosha, ili nchi aliko mtuhumiwa (Marekani) iridhike kwamba huko kuna kesi. Baadaye kesi hiyo tena ifunguliwe katika mahakama ya mahali alipo (DC/Boston) na huko sasa tena mtuhumiwa/mawakili wake ajitete kupinga kurudishwa, hadi hukumu itolewe ndipo sasa anaweza kurudishwa.
Sasa hapo ndipo tunasema HAWAWEZI kwenda RASMI, na ni kweli kama alivyosema Salva bado hawamhitaji (rasmi) bali sasa wanazunguka mbuyu kutaka kufuatilia, yuko karibu na nani na kwa maslahi gani. Je, watu wa nyumbani nani yuko karibu naye na je, amewaachia ujumbe wowote unaoweza kuwaharibia?
KUNA SIRI NZITO. PAMOJA NA KUWA WALIELEZWA KUTAMANI AFE, SASA INAWEZA KUWA KINYUME KWANI HAWAJUI MPAKA SASA ANA SIRI GANI. NADHANI WANATAMANI WAMUONE KWA SIRI KABLA HAJAFA AMA KABLA YA KURUDI NYUMBANI, AMA KABLA HAJAMWAGA RADHI