Liyumba matatani tena, akutwa na simu gerezani

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Liyumba matatani tena, akutwa na simu gerezani
Send to a friend
Friday, 02 September 2011 21:04

liyumba2yrs.jpg
Amatus Liyumba

James Magai
ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi (DPA) wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Amatus Liyumba ambaye anatumikia kifungo cha miaka miwili jela, ameingia matatani tena akidaiwa kukutwa na simu gerezani aliyoitumia kuwasiliana na Rais Jakaya Kikwete.

Liyumba kwa sasa anatumikia adhabu ya kifungo cha miaka miwili katika Gereza la Ukonga, baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka katika ofisi ya umma wakati wa akifanya kazi BoT.

Wakati bado akiwa anaendelea na adhabu hiyo, taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile zilisema Liyumba alifikishwa katika Kituo cha Polisi cha Stakishari kilichopo Ukonga na kuhojiwa kwa kosa la kukutwa na simu gerezani.

Habari hizo zilifafanua kwamba Liyumba alifikishwa kituoni hapo saa 3:00 asubuhi kwa gari la Magereza lenye vioo vyeusi na kuhojiwa kwa muda wa takribani dakika 30 kuhusu tuhuma hizo.

Vyanzo hivyo vya habari vilifafanua kwamba, Liyumba anadaiwa kukutwa na simu ambayo ilibaki kituoni hapo kwa ushahidi.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, Julai mwaka huu Liyumba alimpigia simu Rais Kikwete kwa kutumia simu hiyo. Hata hivyo, bado haijafahamika ni nini hasa alichomweleza Rais lakini habari zaidi zinadai kuwa kitendo hicho kilimfanya mkuu huyo wa nchi kuhoji iweje Liyumba amiliki simu wakati ni mfungwa?
Kutokana na tukio hilo, inadaiwa kuwa maofisa usalama walimwekea mtego na juzi usiku walimdaka akiwa na simu hiyo na asubuhi yake walimpeleka kituoni hapo kwa mahojiano.

“Sasa hivi kinachofanyika ni uchunguzi katika Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) ili kujua alichokuwa akikifanya kwenye hiyo simu na uchunguzi huo ukikamilika basi anaweza kupandishwa kizimbani wakati wowote,” kilidokeza chanzo chetu.

Kifungo cha sasa
Liyumba alihukumiwa kwenda jela miaka miwili na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Mei 24, 2010 na hadi sasa ameshakaa gerezani kwa muda wa miezi 15 na siku 10 (mwaka mmoja, miezi mitatu).

Kabla ya hukumu hiyo, alikuwa amekaa mahabusu kwa muda wa miezi 15 na siku 26 tangu siku aliyopandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza, kisha kupelekwa mahabusu kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Januari 27, 2009 akiwa na mshirika wake, Deogratias Kweka wakikabiliwa na mashtaka mawili ya kuisababishia Serikali hasara ya Sh.221bilioni na matumizi mabaya ya ofisi za umma.

Walikuwa wakidaiwa kutenda makosa hayo kwa kuidhinisha upanuzi wa mradi wa majengo pacha ya BoT, bila idhini ya Bodi ya Wakurugenzi na hivyo kuongeza gharama za mradi tofauti na zilizoidhinishwa na bodi.

Hata hivyo, baadaye Kweka alifutiwa mashtaka na kubakia Liyumba peke yake ambaye naye alishinda kosa kubwa la kuisababishia Serikali hasara ya Sh.221bilioni na kubaki na kosa la matumizi mabaya ya madaraka ambalo lilimtia hatiani.

Mei 28 mwaka huohuo, kwa kutumia jopo la mawakili walioongozwa na Majura Magafu, Liyumba alikata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam akitoa sababu 12 za kupinga hukumu hiyo pamoja na adhabu.
Katika sababu zake za kupinga hukumu hiyo jopo la mawakili wa Liyumba pamoja na mambo mengine, lilisema Mahakama ya Kisutu ilikosea kisheria na kiukweli katika kutathmini ushahidi na utetezi.

Hata hivyo, Desemba 21, 2010, Mahakama Kuu ilitupilia mbali rufaa yake na kukubaliana na hukumu iliyotolewa Mahakama ya Kisutu.

[h=4]Comments [/h]

#4 rutashubanyuma 2011-09-03 06:51 nionavyo sheria yabidi zibadilishwe ili muda wote ambao mtu yupo rumande uhesabike kama sehemu ya kifungo...................na kama sheria hii ingelikuwa yatumika basi Liyumba hivi sasa angelikuwa mtu huru na pengine haya yote yasingelimkuta akiwa ndani.............ninachoshangazw a sana na hukumu ya Liyumba yawaje au hahusiki na matumizi mabaya ya bilioni 221......lakini akutwe na kosa la matumizi mabaya ya madaraka kuhusiana na kosa ambalo tayari alionekana hana hatia..................nchi hii rushwa kwenye mahakama hii yazidi kushamiri.........it makes no logic at, all..........

Quote

+2 #3 Kakomya 2011-09-03 06:11 Aha! Kumbe Liyumba naye alikuwa swahiba wa Rais? Ama kweli tumekwisha. Watanzania inatubidi tufanye juhudi za ziada kuirudisha hadhi yetu iliyopotea. Maana kumtoa Nyerere marais woote tuliowapata baadae ni vibaka! Huyu wa sasa ametia fora kwa maana hana hata chembe ya uoga wala aibu katika utekelezaji wa uhalifu wake.
Mungu ibariki Tanzania.
Quote

+2 #2 Ralph 2011-09-03 05:34 Safari hii tumempata rais Kibaka! Liyumba ni kondoo tu wa Kafara na kufungwa kwake ni geresha tu! Hilo dili la pesa za wizi Kikwete ndiye mwenyekiti!
Quote

+1 #1 ahmed00 2011-09-03 02:53 Rais ni mchafu, anakumbatia wachafu, wengi wa washikaji wake ni wachafu. Haiwezekani kuwa msafi wakati umezungukwa na uchafu.
Quote

Refresh comments list
 
watu hawajagundua kuwa Kikwete yule waliomzoea siye huyu, Awaulize watu wa dini yake ambao walidhani kwa kuwa nimwenzao" atawapatia mahakama ya kadhi, kikwete sio yule wanayesema anacheka na watu, kweli atacheka huku anakushughulikia, hilo la Lyumba liwe onyo na fundisho kwa watu wote ambao hawaamini kuwa ni binadamu, na wanaweza wakapata matatizo kama watu wengine, hiyo simu ni moja ila serikali iende mbali kuona kama hata sehemu anayolala ni sawa na wahalifu wengine, mahitaji anayopata gerezani ni sawa na wezi wa kuku?
 
Simu mkononi kumpandisha tena Liyumba kizimbani
Send to a friend
Wednesday, 07 September 2011 21:36

liyumba2yrs.jpg
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba

James Magai
BAADA ya kukutwa na simu akiwa jela, aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba sasa anatarajiwa kupandishwa kizimbani kwa tuhuma za kukutwa na nyenzo hiyo ya mawasiliano gerezani.

Liyumba ambaye kwa sasa anatumikia adhabu katika Gereza la Ukonga kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka katika ofisi ya umma wakati wa akifanya kazi BoT, anatuhumiwa kukutwa na simu hiyo gerezani na Septemba 2, alifikishwa katika kituo cha Polisi Stakishari kwa mahojiano na polisi.

Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Jeshi la Magereza, Naibu Kamishna wa Magereza (DCP), John Minja alisema Dar es Salaam jana kwamba kitendo alichokifanya Liyumba kilivunja sheria za nchi na kanuni za jeshi la Magereza.

Hatua hiyo ya Magereza imekuja baada ya polisi kutangaza kwamba haina kanuni inayoweza kutumiwa na jeshi hilo kumtia mtuhumiwa hatiani. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alikaririwa mara baada ya Liyumba kuhojiwa akitoa wito kwa Jeshi la Magereza kutoa kanuni zinazoonesha kuwa hilo ni kosa.

Minja alisema Liyumba atapandishwa kizimbani kujibu tuhuma hizo wakati wowote mara baada ya polisi kukamilisha upelelezi wake.

DCP Minja alisema Liyumba alivunja Sheria ya Magereza Namba 34 ya mwaka 1967, Sura ya 58 kifungu cha 85 pamoja na Kanuni za Magereza Tangazo la Serikali (GN) Namba 13 la mwaka 1968.

Kifungu hicho kinaeleza kuwa mtu yeyote ambaye hana mamlaka ya kisheria atakayeingiza au kutoa kitu chochote gerezani kilichopigwa marufuku atakuwa na hatia. Kanuni hiyo ya Magereza inabainisha kuwa ni kosa kwa mfungwa yeyote kumiliki kitu chochote asichoruhusiwa kuwa nacho gerezani.

"Simu ni miongoni mwa vitu vilivyopigwa marufuku gerezani. Si mfungwa wala mahabusu tu lakini hata askari wa kawaida haruhusiwi kuingia na simu gerezani isipokuwa mkuu wa gereza na wasaidizi wake tu," alisema.

Kwa mujibu wa kifungu hicho cha 85 (1) adhabu ya kukutwa gerezani na kitu chochote kilichopigwa marufuku, ni faini isiyozidi Sh1,000 au kifungo kisichozidi miezi sita au vyote viwili kwa pamoja.

Alisema athari za mahabusu au mfungwa kuwa na simu gerezani ni uwezekano wa kuathiri usalama wa gereza kwa kuwa mhusika anaweza kuitumia kupanga njama za uhalifu au hata kuvuruga ushahidi kwa kuwatishia mashahidi, hakimu au jaji.

"Kwa hiyo Liyumba alipokamatwa na alifikishwa katika kituo cha Polisi Stakishari kuhojiwa na alifunguliwa jalada namba STR/IR/8661/2011 na baada ya uchunguzi wa polisi kukamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo," alisema DCP Minja na kuongeza;

"Wapo wengi tu ambao tulishawakamata na kuwapeleka mahakamani ambao walipatikana na hatia ya kosa na wakatumikia adhabu".

Akizungumzia suala hilo wakili mmoja wa Serikali ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini alisema: "Hili ni kosa la jinai. Ni hatari sana kwa usalama wa gereza kwani mfungwa au mahabusu akiwa na simu anaweza kushirikiana na watu wa nje kupanga njama dhidi ya gereza."

Wakili huyo aliongeza: "Kwa kuwa anakuwamo ndani, basi anakuwa ameyajua mazingira yote ya gereza na udhaifu wake. Hivyo anaweza kutoa kwa watu wa nje ambao wanaweza kufanikisha kuvamia au kuingia na kuwatorosha wafungwa na mahabusu gerezani."

Alisema kutokana na kosa hilo, mfungwa au mahabusu anayekamatwa na simu gerezani anafunguliwa mashtaka mahakamani na akipatikana na hatia adhabu yake huwa ni faini au kifungo jela au vyote viwili.

Siku alivyodakwa

Baada ya kubainika alikuwa na simu gerezani anayodaiwa kumpigia Rais Jakaya Kikwete, Liyumba alifikishwa kituo hicho cha Stakishari saa 3:00 asubuhi na kuhojiwa kwa muda wa takriban dakika 30.

Ili kukamilisha uchunguzi wake, Polisi inatarajiwa kushirikiana na kampuni ya simu iliyotumiwa kumwezesha mtuhumiwa kuwasiliana pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), ili kujua alichokuwa akikifanya kwenye hiyo simu.

Liyumba alihukumiwa kwenda jela miaka miwili na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mei 24, 2010 baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya ofisi. Hadi sasa Liyumba amekaa gerezani kwa muda wa miezi 15 tangu alipohukumiwa.

watu hawajagundua kuwa Kikwete yule waliomzoea siye huyu, Awaulize watu wa dini yake ambao walidhani kwa kuwa nimwenzao" atawapatia mahakama ya kadhi, kikwete sio yule wanayesema anacheka na watu, kweli atacheka huku anakushughulikia, hilo la Lyumba liwe onyo na fundisho kwa watu wote ambao hawaamini kuwa ni binadamu, na wanaweza wakapata matatizo kama watu wengine, hiyo simu ni moja ila serikali iende mbali kuona kama hata sehemu anayolala ni sawa na wahalifu wengine, mahitaji anayopata gerezani ni sawa na wezi wa kuku?

JK ni yuleyule na hakuna alichobadilika............................kuwageuka waislamu ni baada ya kuona upepo wa kisiasa umemgeuka....................na hata Bunge halina imani naye na lipo kwenye mikakati ya kumtema......................Lipumba alifikiri yuko karibu na JK..............lakini asichokijua ni kuwa JK ana wenyewe.......................akina Rostam Aziz,Manji.......................Kempinsky.........................Msekwa........................na wengineo................hata Lowassa alifikiri anamfahamu JK.............sasa amemfahamu kuwa ni mnafiki wa kutupwa................
 
Liyumba matatani tena, akutwa na simu gerezani Send to a friend

Friday, 02 September 2011 21:04

liyumba2yrs.jpg
Amatus Liyumba

James Magai
ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi (DPA) wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Amatus Liyumba ambaye anatumikia kifungo cha miaka miwili jela, ameingia matatani tena akidaiwa kukutwa na simu gerezani aliyoitumia kuwasiliana na Rais Jakaya Kikwete.

Liyumba kwa sasa anatumikia adhabu ya kifungo cha miaka miwili katika Gereza la Ukonga, baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka katika ofisi ya umma wakati wa akifanya kazi BoT.

Wakati bado akiwa anaendelea na adhabu hiyo, taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile zilisema Liyumba alifikishwa katika Kituo cha Polisi cha Stakishari kilichopo Ukonga na kuhojiwa kwa kosa la kukutwa na simu gerezani.

Habari hizo zilifafanua kwamba Liyumba alifikishwa kituoni hapo saa 3:00 asubuhi kwa gari la Magereza lenye vioo vyeusi na kuhojiwa kwa muda wa takribani dakika 30 kuhusu tuhuma hizo.

Vyanzo hivyo vya habari vilifafanua kwamba, Liyumba anadaiwa kukutwa na simu ambayo ilibaki kituoni hapo kwa ushahidi.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, Julai mwaka huu Liyumba alimpigia simu Rais Kikwete kwa kutumia simu hiyo. Hata hivyo, bado haijafahamika ni nini hasa alichomweleza Rais lakini habari zaidi zinadai kuwa kitendo hicho kilimfanya mkuu huyo wa nchi kuhoji iweje Liyumba amiliki simu wakati ni mfungwa?
Kutokana na tukio hilo, inadaiwa kuwa maofisa usalama walimwekea mtego na juzi usiku walimdaka akiwa na simu hiyo na asubuhi yake walimpeleka kituoni hapo kwa mahojiano.

"Sasa hivi kinachofanyika ni uchunguzi katika Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) ili kujua alichokuwa akikifanya kwenye hiyo simu na uchunguzi huo ukikamilika basi anaweza kupandishwa kizimbani wakati wowote," kilidokeza chanzo chetu.

Kifungo cha sasa
Liyumba alihukumiwa kwenda jela miaka miwili na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Mei 24, 2010 na hadi sasa ameshakaa gerezani kwa muda wa miezi 15 na siku 10 (mwaka mmoja, miezi mitatu).

Kabla ya hukumu hiyo, alikuwa amekaa mahabusu kwa muda wa miezi 15 na siku 26 tangu siku aliyopandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza, kisha kupelekwa mahabusu kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Januari 27, 2009 akiwa na mshirika wake, Deogratias Kweka wakikabiliwa na mashtaka mawili ya kuisababishia Serikali hasara ya Sh.221bilioni na matumizi mabaya ya ofisi za umma.

Walikuwa wakidaiwa kutenda makosa hayo kwa kuidhinisha upanuzi wa mradi wa majengo pacha ya BoT, bila idhini ya Bodi ya Wakurugenzi na hivyo kuongeza gharama za mradi tofauti na zilizoidhinishwa na bodi.

Hata hivyo, baadaye Kweka alifutiwa mashtaka na kubakia Liyumba peke yake ambaye naye alishinda kosa kubwa la kuisababishia Serikali hasara ya Sh.221bilioni na kubaki na kosa la matumizi mabaya ya madaraka ambalo lilimtia hatiani.

Mei 28 mwaka huohuo, kwa kutumia jopo la mawakili walioongozwa na Majura Magafu, Liyumba alikata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam akitoa sababu 12 za kupinga hukumu hiyo pamoja na adhabu.
Katika sababu zake za kupinga hukumu hiyo jopo la mawakili wa Liyumba pamoja na mambo mengine, lilisema Mahakama ya Kisutu ilikosea kisheria na kiukweli katika kutathmini ushahidi na utetezi.

Hata hivyo, Desemba 21, 2010, Mahakama Kuu ilitupilia mbali rufaa yake na kukubaliana na hukumu iliyotolewa Mahakama ya Kisutu.

Liyumba anaonewa buure kwa mtizamo wangu mimi namuona ni shujaa hata kama alikwiba lakini kaacha ukumbusho wa kuongeza ghorofa pacha za Benki Kuu ambayo bila yeye ingekuwa mbilikimo,na je wale wanaopewa kusimamia miradi na hakuna kinachoonekana,asvali Liyumba bana kaiba lakini kuna kitu tunakiona alichokifanya,wengine wanaiba hatuoni kilichofanywa zaidi ya tumboni street
 
Back
Top Bottom