Liyumba kuwasilisha rufaa leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Liyumba kuwasilisha rufaa leo

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, May 30, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280


  [​IMG]
  ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba
  ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba, leo anatarajiwa kukata rufaa na kuiwasilisha mahakama kuu, kupinga hukumu ya miaka miwili jela. Wakili aliyekuwa akimtetea Liyumba, Majura Magafu amesema kuwa, watawasilisha rufaa hiyo leo kutokana na kutoridhishwa na maamuzi wa mahakama ya Kisutu dhidi ya hukumu hiyo.


  Liyumba alihukumiwa Mei 24 mwaka huu, baada ya kukutwa na hatia ya matumizi mabaya ya ofisi akiwa mkurugenzi katika mradi wa majengo pacha ya benki hiyo hali aliyoisababishia serikali kupata hasara ya shilingi bilioni 221.
   
Loading...