Liyumba ajikita Mahakama ya Rufaa.......... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Liyumba ajikita Mahakama ya Rufaa..........

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Dec 25, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,313
  Likes Received: 418,600
  Trophy Points: 280
  Liyumba aendeleza mapambano
  Friday, 24 December 2010 20:27

  James Magai na Tausi Ally
  KIGOGO wa zamani katika Benki Kuu ya Tanzania, Amatus Liyumba, ameamua kuendelea kupinga adhabu ya kifungo cha miaka miwili anayoendelea kuitumikia.

  Hatua hiyo imekuja baada ya kugonga ukuta katika rufaa yake ya kwanza ya kupinga hukumu hiyo iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Mei 24 mwaka huu.

  Katika hukumu hiyo ya rufaa hiyo iliyosomwa Jumanne wiki hii,Jaji Emilian Mushi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, alitupilia mbali rufaa hiyo na kwamba hukumu na adhabu ya Mahakama ya Kisutu ni sahihi.

  Uamuzi umemfanya Liyumba kuzidi kusota gerezani akitumikia adhabu hiyo.

  Hata hivyo tayari Liyumba kupitia kwa jopo la mawakili wake, linaloongwa na Majura Magafu akisadina na Jaji mstaafu Hilary Mkate, Hudson Ndusyepo na Onesmo Kyauke wameshawasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa katika Mahakama ya Rufani.

  Wakili Magafu alilithibitishia Mwananchi jana kuwa waliwasilisha taarifa hiyo Jumatano ya wiki hii.

  Liyumba aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Benki Kuu (BoT) alihukumiwa kifungo hicho baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya Ofisi za umma.

  Lakini Mei 28 mwaka huu, Liyumba kupitia kwa jopo la mawakili wake, alipinga adhabu hiyo huku akitoa sababu 12 za kufanya hivyo.

  Sababu hizo ni pamoja na madai kuwa Mahakama ya Kisutu ilikosea kisheria na kiukweli katika kutathmini ushahidi na utetezi na kwamba ilkiuka kanuni zilizowekwa na mahakama za juu katika kutoa adhabu.


  Lakini katika hukumu ya rufaa hiyo Jaji Mushi alitupilia mbali utetezi wa Liyumba na mawakili wake, na kuunga mkono hoja za upande wa mashtaka na hukumu ya Mahakama ya Kisutu.

  Katika hukumu hiyo yenye kurasa 60 aliyoisoma kwa muda wa saa mbili dakika na nne, Jaji Mushi alisema hukumu na adhabu hiyo ilikuwa ni sahihi.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,313
  Likes Received: 418,600
  Trophy Points: 280
  Hiki ni kikosi cha kazi tuone kitazaa matunda gani............................ingawje hoja za muhimu za kumnusuru Liyumba mpaka sasa hawajazitaja.......................................

  Hivi yawezekana mtu mmoja akaongeza mapesa kwenye mradi na mkandarasi akalipwa bila ya Bodi na Wizara mama kuruhusu kweli kiwango ambacho Megji akiwa Waziri wa Fedha likwenda Bungeni kutetea kazi hizo za ziada kuwa zilikuwa ni muhimu kwa sababu ya kupambana na tishio la ugaidi?

  Hayo ni maswali ambayo tungependa yaulizwe na Mahakama ya rufaa itutolee majibu................Yasipoulizwa Liyumba aandike maumivu tu..................
   
 3. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #3
  Dec 25, 2010
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  .....hii ni namna ya akina Magafu Majura na wenzake kutafuna pesa iliyobaki ya Liyumba pasipo kuwa na tumaini la kutoka Jela. Waache. i tell u Liyumba hatatoka Jela b`se ana makosa makubwa kuliko hayo ya kisheria. anafanya mchezo na mkwere eeh
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Atashangaa kesi yake ya rufaa itakuwa bado kusikilizwa hadi atatokaa akiwa amemaliza...kifungo!!*nataka kujisafishaa
   
 5. m

  maarufu Member

  #5
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Liyumbaaa oyeeee
   
 6. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #6
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  He'll be free on 02/05/2011
   
Loading...