Live updates: Kilele cha mbio za Mwenge mkoani Iringa

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
4,582
2,783
Wadau,

Kweli Mwenge umechosha watu. Nilikuwa najaribu kuangalia sherehe hizi kupitia TBC. Maajabu karibu uwanja mzima hauna watu pamoja na taarifa ya kukusanya idadi kubwa ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hapo Iringa.

Nimetambua kuwa, hasira zinaweza kwenda kirahisi kwa Kamanda Msigwa.
 
Wadau,

Kweli Mwenge umechosha watu. Nilikuwa najaribu kuangalia sherehe hizi kupitia TBC. Maajabu karibu uwanja mzima hauna watu pamoja na taarifa ya kukusanya idadi kubwa ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hapo Iringa.

Nimetambua kuwa, hasira zinaweza kwenda kirahisi kwa Kamanda Msigwa.

Waalimu wametishiwa kuwa watafukuzwa kaz kwa kutohudhuria na kutosimamia wanafunz,nipo na mwalimu mmoja hapa kwenye kihiace (daladala) alipanga kutoenda lakin anasema amepigiwa simu na mwalimu wake mkuu kuwa kuna daftari la mahudhurio limewekwa na ole wake ambaye hata kuwepo ,so imebid tu aende.
 
sasa naona wameongezeka, kikwete alikuwa anacheza bhana kuna kamziki kanapigwa..... But
 
huyo mwalimu aisipoenda hawezi kufukuzwa kazi kwa sababu ya mwenge
itakuwa ni kituko
 
Kwa nini wawalazimishe hao walimu na wanafunzi kwenda kujaza uwanja?kwa nini wasiwaache huru ili wapime kama huo mwenge unakubalika kwa asilimia ngapi?
 
kwani sakata la kupandisha bendera za ccm liliishaje kwetu huku mikoani mwenge ulikuiwa ni kwa watumishi wote na wala si wananchi wakati mwingine kama kawa magari kufuata wananchi vijijini. vipi hapo iringa suala hilo halikufanyika?
 
kwa sasa vikundi mbalimbali vinaendelea kutumbuiza,wananchi ni wengi xana,tutaendelea kuwapa updates hasa mh.rais atakapoanza kutoa hutuba.
 
wakati wakimbiza mwenge wakielekea mbele kumkabidhi mwenge mh.rais kuna jamaa alienda kuwapokonya mwenge huo bahati nzuri maaskari walimuwahi Wakamtoa.
 
Acha uongo wewe. Watu wengi sana wapo uwanjani sasa. Wakati huo walikuwa barabarani wanamsubiri mhe rais na msafara wake upite. Wana iringa wamejitokeza kwa wingi sana na uwanja umetapika. Acha kusema vitu ambavyo havina uhakika....popompo mkubwa wewe
 
Jamani tuwe waungwana mbona naangalia live kupitia Tbc 1 na naona jinsi watu walivosheheni na Mc anasema huko nje nako watu kibao wanaendelea kuingia uwanjani,!!! Kusema sherehe zimedorora ni unafiki. Mwenge Oyeeeeeeeeeeee!!
 
Vipi kaka we mdau wa maandalizi?? Mbona wawa mkali sana yaheeeeeeee.

Unaangalia viti vya walala hai au walala hoi?
 
We unaangalia kichama inaonyesha. usidanganywe na jukwaa kuu! We unafikiri MC aseme wamesusia mkuu?
 
wkt wakimbinza mwenge wakielekea mbele kumkabidhi mwenge mh.rais kuna kijana alitaka kuwapokonya mwenge bahati nzuri maaskari walimuwahi na kumbeba.
 
Naona kijana anataka kuupeleka Ismani Mkumbusho kuonesha mara ya mwisho kukimbizwa ilikuwa umefanyika Iringa!
 
Haha haaa!kuonyesha watu walivyouchoka mwenge,kuna jamaa kajitokeza na kutaka kuupora mwenge na kutokomea nao kusikojulikana.bahati police wamemuwahi.angefanikiwa angeandika historia ya kusitisha mbio za mwenge moja kwa moja.
 
waalimu wametishiwa kuwa watafukuzwa kaz kwa kutohudhuria na kutosimamia wanafunz,nipo na mwalimu mmoja hapa kwenye kihiace (daladala) alipanga kutoenda lakin anasema amepigiwa simu na mwalimu wake mkuu kuwa kuna daftari la mahudhurio limewekwa na ole wake ambaye hata kuwepo ,so imebid tu aende.

kiherehere chake alishawaambia hawahitaji hao mbayuwayu kweli mara siendi mara kwa sababu...nimeamua niende.
 
Back
Top Bottom