mwenge unasababisha mimba zisizotarajiwa na maambukizi ya ukimwi.
Wadau,
Kweli Mwenge umechosha watu. Nilikuwa najaribu kuangalia sherehe hizi kupitia TBC. Maajabu karibu uwanja mzima hauna watu pamoja na taarifa ya kukusanya idadi kubwa ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hapo Iringa.
Nimetambua kuwa, hasira zinaweza kwenda kirahisi kwa Kamanda Msigwa.
Walioshiliki hawajafunguka kiutashi! mbona CDM hawashiliki?
Kwa nini wawalazimishe hao walimu na wanafunzi kwenda kujaza uwanja?kwa nini wasiwaache huru ili wapime kama huo mwenge unakubalika kwa asilimia ngapi?
Wanalazimishwa tu mkuu ila kwa hiari unadhani ungemkuta mtu na akili zake timamu amekaa chini kuangalia moto. Labda awe mchawina kwanini kila siku iwe ni walimu tu? Na sio wafanyakazi wengine kama mapolisi nk?
huku kwetu Mwenge shughuli za mwenge ziligharimu zaid ya Tsh.180,000,000/=, na ulitembelea vijiji 3 na Kuzindua nyumba 3 vijijini vyenye jumla ya Tsh,22,000,000/= jamani tueleweni mwenge ni kudhalilishana.Jamani tuwe waungwana mbona naangalia live kupitia Tbc 1 na naona jinsi watu walivosheheni na Mc anasema huko nje nako watu kibao wanaendelea kuingia uwanjani,!!! Kusema sherehe zimedorora ni unafiki. Mwenge Oyeeeeeeeeeeee!!
Mkuu kuna yeyote ndani ya familia yako amefanywa hivyo? Hebu tuweke wazi mkuu