Live Updates: Azam & Simba Matches

Hao wagonga nyundo nasikia ni n.y.oko sana wanapokua kwao!

mkuu wale jamaa hawafai, mie mara ya kwanza nimeona mechi yao uwanja wa taifa siku ile wanacheza na Yanga, sio siri wale jamaa ni hatari sana, beki za yanga zilikuwa hazipandi mbele kama walivyozoea kucheza na timu nyingine
 
Mgambo wazuie kabisa wasifanye makosa kama ya Mtibwa pale Jamhuri Morogoro.
 
Simba wakipoteza hii mechi natangaza kuwa shabiki mfu wa simba kuanzia jioni pale mpira utakapoisha na sitakaa niende uwanjani tena kuangalia mechi yoyote ya Simba wala kukaa kwenye TV kuangalia wakati Simba inacheza.
 
Mnyama ni mnyama tuu, simba hata kama ni Mzee usije ukadhani mbwa utaumia MKUU, nawatakia simba ushindi MNONO.
 
Halafu jamaa hawafungiki mpaka wawepungufu. Ukibisha waulize magalasa wa Uturuki.

mkuu ile mechi name nilishuhudia live, wale jamaa kiukweli hawafai kabisa, ukiwa nje utaona kama wanafanya mzaa ila waulize wachezaji wa timu pinzani watakwambia shughuli ya wale jamaa
 
Goli liliingia baada ya jamaa kutolewa au?
Sasa we unafikiri wangetimia wangeshindwa kurudisha? Mshukuruni mwamuzi wa mchezo la sivyo na nyinyi mungevunja viti kama hao wenzenu wa mtaa wa pili.
 
Simba wakipoteza hii mechi natangaza kuwa shabiki mfu wa simba kuanzia jioni pale mpira utakapoisha na sitakaa niende uwanjani tena kuangalia mechi yoyote ya Simba wala kukaa kwenye TV kuangalia wakati Simba inacheza.

Hahahahaha!si tutakua wote hapa JF au ndio ata hapa JF sport utapasusa?
Maana hii mechi lazima simba apigwe.
Yani ni sawa na uji na mgonjwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…