Live Updates: Azam & Simba Matches

Live Updates: Azam & Simba Matches

Tukumbushane analysis hii hapa chini nilikuwa nimeiweka humu jamvini about a week ago. Nadhani sasa tunaelewana....

Tisha-TOTO
Mkuu, ni ukweli usiopingika (na mchungu kumeza kwa wana Simba) kuwa Yanga ndiyo timu iliyosheheni vipaji bora kuliko timu yo yote hapa Tanzania kwa sasa ukilinganisha one vs one. Hilo halina ubishi.

Ni kwa vile tu Yanga wamejichanganya siku za hivi karibuni kwa kitendo cha kubadili benchi la ufundi ambalo lilikuwa linafanya kazi vizuri bado (ubingwa msimu uliopita na kuiweka timu kileleni mwa ligi msimu huu). Hii ni moja ya oversight kubwa sana ya uongozi na ndicho kitu kimeifanya timu ianze kwa kusuasua round hii ya pili.

Hata hivyo, pamoja na yote haya, nina uhakika wa 110% Yanga ataibuka bingwa come end of the season. Hii ni kwa sababu ya uzoefu wa kikosi ambao unaowawezesha kuhimili pressure ambayo huwapo kwenye run-in stage ya ligi yoyote and the fact kuwa hata historia inawa-back Yanga kuwa huwa ni wazuri sana kwenye run-in stage. Azam bado sana uwezo wa ku-handle aina hii ya pressure. Simba ni jina kubwa lakini wachezaji wake bado wachanga ku-handle pressure kubwa. Mbeya City ni kama Simba.

Haya mambo maamuzi yenye utata wa marefa ni jambo lisilokwepeka (inevitable) kwenye ligi yoyote duniani. Nadhani mmesikia jana Mourinho akilalamika kuwa ManCity huwa wanabebwa, lakini anasahau kuwa Chelsea alikuwa apoteze mechi pale darajani msimu huu dhidi ya West Brom kama si maamuzi tata ya refa yaliyowaokoa.

Yanga mwenyewe ni victim mara kadhaa wa maamuzi tata ya marefa, ingawa ni ukweli usiopingika kuwa kuna mengine amenufaika nayo pia. Hii hutokea si kwa Yanga tu bali pia kwa Simba, Azam, Coastal, nk. At the end of the season, things tend to even themselves out!
 
Yaani weekend hii imekuwa tamu sana kwangu mimi mwenzenu.....

Liverpool 5 Arsenal 1
Yanga 7 Wakomoro 0
Mgambo 1 Simba 0.

It can't get better than this, can it?

Mliofurahi kama mimi kwa matokeo hayo yote matatu tuungane kufurahi pamoja!!

Tuko identical twins katika hili!
 
Tatizo la mikia ni kelele nyingi, ile timu kwa mtu anayechambua mpira haina lolote. Bahati mbaya sana hata kocha wao sijui ameletwa kwa ajili ya Yanga mie sielewi manake kutwa kucha yeye anaongelea Yanga tu. Juzi wakati wnakwenda Mtibwa yeye akabaki Dar eti kuisoma Yanga, halafu anatamba eti dawa ya Yanga anayo, wakati anaenda kupambana na Mtibwa ni akili hiyo? Huyu amekwisha cheza na Yanga si bora Mholanzi ndo angekuwa anawahangaikia Simba manake hajacheza nao? dah! kipondo kingine mbeya, lazima mkalishwe tuuuuuuu!
 
Inategemea na timu, Mgambo inashika mkia halafu ndani ya dakika 90 mnakubali kipigo, wachezaji wetu wana matatizo hawajui maumivu wanayotusababishia, jiulize kuna watu wanatumia hela zao kusafiri kwenda kuwashangilia halafu wanaishia kupata maumivu hiyo ni haki kweli.

Dondosha chozi bro
 
Kuna watu tulikuwa tiGO tukahamia Airtel kwa sababu ya mauzauza mengi, kwa nini wewe usihamie Yanga, Azam au hata Mbeya City; timu zinazofanya vizuri? Kwa nini uendelee kuumia kila siku. Ukiwa mbishi utaendelea kupata dhoruba. Kuna kipigo kingine cha nguvu kinawasubiri pale Mbeya, jifunge kiume usije ukaanguka.

Wasukuma tunasema 'kwibata' yaani unajifunga nguo (normally khanga) na kuipitisha katika mapaja yote ili kuhakikisha kuwa sehemu nyeti ziko salama, huku ukiwa kifua wazi ndipo uingie vitani. Mkuu Masuke mnatakiwa 'kwibata' kabla ya kukipiga na Mbeya City, vinginevyo MCC watagonga sehemu nyeti mapema na ndipo mtakapolegea na kutandikwa goli nyingi tu.
 
Mkuu ushabiki wa mpira ni kama kabila huwezi kubadilisha sana sana utaacha baadhi ya mila za kabila lenu lakini huwezi kufanya total change ya kabila na mpira ni hivyo hivyo, ushabiki utafifia tu kushabikia timu yako kutokana na uzembe wanaofanya lakini huwezi kuihama kabisa.
 
Sasa mjiandae 'kwibata' mnapokutana na Mbeya City.
 
tichaa said:
Many teacher have to work not only for many hrs but also for a very small salary.
By TIE (english bk2 pg8)
What is ua commen?

Sent from my GT-B5512 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom