Live TBC1: Mawaziri wanaapishwa

Live TBC1: Mawaziri wanaapishwa

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,148
Reaction score
162,558
Muda huu ndio Raisi Kikwete amewasili katika viwanja vya Ikulu na zoezi la kuapishwa mawaziri ndio limeanza ambapo wanakula kiapo hicho mbele ya Raisi Kikwete.

Dr.Husseim Mwinyi ndio amekuwa wa kwanza akifuatiwa na Mathias Chikawe.
 
Waziri husein Mwinyi ameshaapishwa amefuata Mathias Chikawe sasa anafuata Asharose Migiro,Charles kitwanga naiau waziri nishati na madini,Amos Makalla naibu waziri wa maji,Janeth Mbene naibu waziri viwanda na biashara,Jenista Mhagama naibu waziri elimu...
 
JK Mbona Leo anhasira sana,Hana tabasam hata kidogo
 
Mungu awatangulie na kuwaongoza katika kutekeleza majukumu ya nafasi zao mpya. Wafanye kazi na kutimiza yale yote yanayotakiwa kutoka kwao kwa mujibu wa sheria za nchi. Ni kwa kufanya hivyo ndipo wataweza kuliponya taifa hili kutokana na uovu unaoendelea sehemu mbalimbali hasa unaohusiana na maliasili za taifa letu
 
Natamani hizi biblia takatifu na quruan tukufu zingekuwa zinawaunguza wizi uzandiki, na uchawiuchawi ndio siasa za afrika walaaniwe wote wanaovitia vitabu vya mungu unajisi.
 
Wakuu naendelea kufuatilia kuapishwa kwa mawaziri na manaibu wao wapya ikulu muda huu,kila anaeapa anasema sitatoa SIRI za baraza la mawaziri 'Mungu nisaidie' wakuu anaejua SIRI hizo atusaidie ni nini huwa wanatuficha watanzania kwenye hilo baraza la mawaziri.
 
Back
Top Bottom