LIVE feeds: Taifa Stars Tanzania VS Indomitable Lions (Cameroon)

LIVE feeds: Taifa Stars Tanzania VS Indomitable Lions (Cameroon)

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2011
Posts
4,225
Reaction score
869
Heshima kwenu wakuu.

Kwa wale tulioko ndani ya uwanja wa Taifa tujaribu kuwajuza wenzetu kile kinachoendelea ndani ya uwanja wa Taifa kwenye mechi kati ya Taifa Stars na Cameroon.

attachment.php

FULL TIME RESULTS:

Tanzania 1 - 0 Cameroon

attachment.php

​
 

Attachments

  • vplresults[1].jpg
    vplresults[1].jpg
    33.5 KB · Views: 2,365
  • full-time.jpg
    full-time.jpg
    18.5 KB · Views: 2,438
Picha:

1.jpg


Mbwana Samatta wa Tanzania akifunga bao baada ya kumlamba chenga kipa wa Cameroon, Efalla Komguep katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa baina ya timu hizo jioni ya leo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Tanzania, Taifa Stars ilishinda 1-0.

10.jpg

Beki wa Stars, Erasto Nyoni akimtoka beki wa Cameroon, Assou Ekotto

11.jpg

Thomas Ulimwengu akiwa ameruka juu na kipa wa Cameroon, Efalla Komguep kuwania mpira wa juu

12.jpg

Mbwana Samatta akipambana na mabeki na kipa wa Cameroon

13.jpg

Kiungo Frank Domayo wa Tanzania kulia akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Cameroon, Nyom Allan

14.jpg

Wachezaji wa Tanzania wakishangilia bao lao lililofungwa na Samatta waliyemdandia

0.jpg

Wa Mazembe, si wazembe; Thomas Ulimwengu akimpongeza mshambuliaji mwenzake wa TP Mazembe ya DRC, Mbwana Samatta kuifungia Stars leo

16.jpg

Kikosi cha Cameroon leo

15.jpg

Kikosi cha Stars leo

3.jpg

Samatta akimfunga tela Ashu Clovis

2.jpg

Thomas Ulimwengu akiwalamba chenga mabeki wa Cameroon

5.jpg

Beki Shomary Kapombe akitia krosi huku beki wa Cameroon, Nyom Allan akiipisha

7.jpg

Beki wa Cameroon, Aminou Bouba akimiliki mpira mbele ya kiungo wa Tanzania, Mwinyi Kazimoto

8.jpg

Hapa ndipo Stars ilipopata penalti, beki Ngoula aliupitia mpira miguuni mwa Samatta akitokea nyuma ndani ya eneo la hatari
 
jamano wqdau ni tv gani inaonesha huo mpira wa taifa star vs cameroon
 
Jamani ehee mbona kimyaa? au ndiyo tumeisha chinjwa!
 
naombeni mwenye link ya hii mechi kwenye internet anipe manake nipo nchi za watu!
 
Ila kiss Fm na TBC Taifa wanatangaza moja kwa moja..........Star TV wamejiunga wadau...mpira bado bila bila dk ya 18.....kaseja yupo chini kwa maumivu baada ya kugongana na Mchezaji wa Cameroon....
 
king'amuzi kinazingua tu kinastak hata cd star tv wanaonesha..
 
Back
Top Bottom