Live Band nyingi sio Halisi!

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
36,970
45,849
Ukitaka kujua kua hawa jamaa wanapiga play back na sio live;

1. Sauti ya mwimbaji mkuu " solo artist" ni ile ile, kila unakokwenda.

2. Idadi ya vyombo eneo husika haiendani na vyombo vinavyosikika kwenye mziki unaopigwa, mfano; unaweza sikia saksafoni kwenye mziki lakini live haipo.

3. Mapigo ya mziki live ni tofauti na Yale yanayoskika; mfano; angalia kwa makini mpiga drums; mapigo yake hayaendani na Yale ya mziki unaosikika!

4.mziki unaweza anza ghafla kwa ala ambazo hazipo live! Mfano mziki husika unaweza anza kwa kusikika saksafoni wakati haipo.

5. Wanamuziki wakiwa wanaongea wenyewe kwa wenyewe, hawasikiki ila wakiimba utawasikia!

6. Jamaa wamekariri nyimbo zote ila hawaimbi live! Wanaigiza tu!

7. Hayo yote ni maigizo! Hakuna live Band!
 
Duuh, hebu ngoja niangalie kwa makini hapa kama vipi nikawaumbue npo sehemu flan hivi hapa kuna hiyo live band!!!
 
Iko hivi, Vibendi vidogo vinavyopiga live huwa wanatumia mchanganyiko wa live na playback kwa hiyo anakuwa na zile nyimbo kwenye keyboard zikiwa na baadhi ya vyombo (kama trumpet) vyombo vilivyobaki pamoja na sauti zinatoka live. Hivyo kama kuna waimbaji, keyboard na magitaa mawili basi hao unaowaona ndio wanapiga live vyombo vingine vilishaingizwa/kurekodiwa kabla.
 
Back
Top Bottom