Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,846
- 43,318
Wasalaam wana jamvi.
Bila shaka kila mmoja wetu anajua fika muziki wa live unavyo vutia na kufurahisha na bila shaka kama kweli msanii atajiandaa na ataishi maisha ya kuimba live atapiga pesa sana tena sana maana hakuna kitu kina kera unapo kwenda kwenye show ya msanii halafu unasikia sauti ya CD badala ya kumsikia yeye.
Hapa Tanzania kuna band zinaimba live nyingi mfano Twanga pepeta, Yamoto band bila kuwasahau malaika band...na bila shaka hakuna ambaye amewai toa pesa yake kwenda kuwasikiliza hawa watu na hakajuta kwanini hakuigawa tuu au kuinunua sukari ikakaa nyumbani.
Binafsi kwa wasanii wa bongo fleva kwa sasa mtu ambaye anaweza kunishawishi nitoe pesa yangu kwenda kumuangalia akiimba live ni Christian Bella maana huyu mtu si wa mchezo kabisa na anaweza imba wimbo mmoja watu wakataka auimbe mara kumi huku unasikia ushirikiano wa mpiga kinanda,gita ,ngoma na kila chombo. Kama kuna aliyewai kuhudhuria show yeyote ya christian Bella akiimba bila shaka atanielewa nasema nini.... uzuri wa huyu mtu ana uwezo kabisa wa kujua gita sauti imepanda sana, au kinanda kiko chini, mpiga ngoma anapitiliza na huwa anarekebisha papo hapo na mambo yanakwenda sawa.
Ni ngumu sana tena sana kumpata msanii wa bongo fleva anayeimba live ukapenda arudie wimbo mmoja hata mara nne kama Christian Bella hakika kwa Christian Bella hatupunjwi na wala hatuibiwi ndio maana nataka wasanii wetu wajaribu kujifunza kwakwe au waache kuwadanganya watu wanataimba live maana baadhi ya wasanii sio wanaimba live bali hutapika live.
Halafu kuna tatizo wanalo wasanii wetu kama sio wao bali wanao waandaa kwani wao hudhani kuimba live ni kubadilisha melody, beat na sauti ya wimbo kiasi kwamba unaweza kujiuliza huyu anaimba wimbo gani? Watu wanapo kwenda kumsikia msanii akiimba live wanatarajia kusikia sauti yake halisi, ushirikiano wake na gita,kinanda na ngoma si vinginevyo na ndio maana nasisitiza wasanii wetu wanapaswa kwenda kuchukua shule kwa Christian Bella.
Kuna wasanii baadhi nimesha washuhudia kwenye luninga wakiimba live nitawataja na kuawachambua kidogo
1. Barnaba 2. Rubby 3. Ditto 4.Mwasiti 5.Marrlow 6.Baraka 7.Jux.8.Diamond
Barnaba na Ruby
Barnaba ana uwezo mkubwa sana wa kuimba live lakini bado ana tatizo la kuweka madoido mengi hadi ana kera sana tena sana na hili tatizo amesha muambukiza Ruby na analo sana tena sana...Hawa wanafikiri kuimba live ni kuweka manjonjo mengi hadi mantiki ya wimbo na melody inapotea... Lakini ukweli ni kwamba Barnaba muziki wa live anaujua bali anatakiwa kurekebisha madhaifu madogo aliyo nayo na kuongeza mazoezi hasa kwenye sauti. Ruby safari bado anayo ndefu maana bado hawezi kwenda sambamba na vyombo lakini anapaswa kujifunza na kufanya mazoezi.
Ditto
Kama ningepewa nafasi ya kumuambia mtu fulani aache kuimba live akiwa stageni basi ninge mwambia Ditto maana kwakweli ana madhaifu mengi sana na haya niliyashuhudia kwenye luninga akiimba wimbo wake wa moyo sukuma damu kwa kila aliye angalia ataamini kuwa alikuwa aimba vibaya sana au bora angeweka cd maana alibadilisha melody pia alishindwa kwenye sambamba na vyombo vya muziki na ukumbi ulikuwa umepoa na hata wasanii wenzie walio kuwa nyuma yake walikuwa wanapishana sana tena sana...itoshe kusema tuu kuwa Ditto anza upya mazoezi ya kuimba live ukiwa tayari anza kuimba.
Mwasiti na Marllow.
Ukweli ni kwamba hawa wawili wanacho kosa tuu ni mazoezi na kuwa serious maana macho yanaona kabisa wana uwezo sana tena sana. Marllow anajua sana kwenda sambamba na vyombo bila kumsahau Mwasiti pia ana sauti iliyoshiba na ina mvuto sana wanaweza kushawishi kuwasikiliza.
Baraka Da price na Jux.
Baraka ana sauti nzuri sana lakini swala la kuimba live bado hajaliweza na ni wazi huwa hafanyi mazoezi ya kutosha ndio maana hujikuta sauti ina mkauka kabisa na wala huwa hajui kuwa anapaswa kwenda sambamba na vyombo vya muziki na pia swala la kuongeza madoido mengi humuathiri sana. Jux ni msanii ambaye ana sauti yenye nguvu sana akiwa anaimba hata kupitia cd sauti yake husikika vyema anachotakiwa kwenye live ni kuongeza mazoezi ya kuimba live na kuachana na madoido kama wenzie lakini yeye ana fundishika ana paswa kumtazama Christian Bella anavyo fanya.
Diamond
Diamond alipoanza kufanya live ameanza kwa hatua kubwa maana ambacho nimegundua alicho fanikiwa ni kuweza kucontrol mwenda wa vyombo na sauti yake na ni wazi alifanya mazoezi kwa muda kidogo lakini pia anatakiwa kufanya mzoezi ili kuongeza pumza zaidi na kuondokana na kuchoka haraka, na kwa upande wa madoido kwake sijaliona sana lakini anapaswa kuepuka.
Hao ni mfano wa wasanii ambao wamewai kuimba live na nikawaangalia kwakweli itoshe kusema wasanii wengi wa bongo fleva wana kurupuka au kupushwa kwa uroho wa pesa mwisho wanaishi kuropoka live badala ya kuimba live ndio maana show zao nyingi zinakuwa zimepooza maana wanatumia wiki moja kujiandaa kuimba live wakati wanatakiwa kuishi wakiimba live.
Bila shaka wasanii wetu wanapaswa kuwa wanahudhuria show za Christian Bella ili wajifunze utofauti wa kuimba live na kuboronga live..watu wengi wamekuwa wakiliwa hela zao kwa kisingizio cha muziki wa live kumbe ni utumbo mtupu na uzuri waandaaji hujua fika show za live zina wateja wenye pesa wako radhi kutoa laki moja kwenda kushuhudia lakini huishia kujuta.
Wasalaaam.
N:B wale wana blog mnao nakili makala humu na kuzifanya za kwenu Mungu anawaona. basi msisite kusema mmezipata wapi.