Lita moja ya mafuta imefika 2,200, serikali ipo wapi?

Madcheda

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
422
69
jamani naomba nilete kilio changu kidogo! hivi huu ugumu wa maisha ni mimi mwenyewe ndo nnao u feel au ni watanzania wote???mbona kila mtu yupo kimya?
yan nimetoka kuweka mafuta saiv nimekuta lita moja ni 2,200 (yes elf mbili na mia mbili) hapo nilipo nasikia hazina haina hela na watu hawajalipwa mishahara. jaman hakuna anaye umia na hii hali mbona kimya???

Naomba msaada jamani hakuna lolote tunawezakufanya ili tubadili hii hali hata bei ya mafuta ipungue?mbona kenya wameandamana imeshuka sisi mbona tunaumia kimya kimya jaman????
 
wewe unajua bei ya mafuta kitika soko la dunia? au ndio kuropoka, kama mafuta yamepanda bei kwa wanaochimba je unategemea nini kwa nchi kama Tanzania.
 
Think BIG, kwani kuna hivi karibuni umesikia serikali imeongoza kodi kwenye mafuta? The rest serikali ya Tanzania haimiliki visima vya mafuta....
 
hajaongeza lakini kwa wenzetu kama kenya imebidi waondoe baadhi ya kodi ili bei ishuke maana kama mafuta yakipanda automatically na bidhaa zinapanda pia,use ur common sense
 
wewe unajua bei ya mafuta kitika soko la dunia? au ndio kuropoka, kama mafuta yamepanda bei kwa wanaochimba je unategemea nini kwa nchi kama Tanzania.

Kwani Kenya haipo kwenye soko la duni?
 
wewe unajua bei ya mafuta kitika soko la dunia? au ndio kuropoka, kama mafuta yamepanda bei kwa wanaochimba je unategemea nini kwa nchi kama Tanzania.

nategemea wapunguze baadhi ya kodi kwenye mafuta ili bei zishuke kaka
 
Think BIG, kwani kuna hivi karibuni umesikia serikali imeongoza kodi kwenye mafuta? The rest serikali ya Tanzania haimiliki visima vya mafuta....

hajaongeza lakini kwa wenzetu kama kenya imebidi waondoe baadhi ya kodi ili bei ishuke maana kama mafuta yakipanda automatically na bidhaa zinapanda pia,use ur common sense
 
wewe unajua bei ya mafuta kitika soko la dunia? au ndio kuropoka, kama mafuta yamepanda bei kwa wanaochimba je unategemea nini kwa nchi kama Tanzania.

Kama majibu ni hayo hakuna haja ya kuwa na Serikali! Hata yakitokea mafuriko tutaambiwa kwamba tusidai msaada nna kwmba si mnaona mvua nyingi sasa hivi?
 
Mvua inanyesha na mafuta yanachibwa ni vitu viwili tofauti.
 
wewe unajua bei ya mafuta kitika soko la dunia? au ndio kuropoka, kama mafuta yamepanda bei kwa wanaochimba je unategemea nini kwa nchi kama Tanzania.

Jaribu kufikiri japo kidogo basi,kuna sababu gani ya kuwa na serikali kama haiwezi kujali raia wake kwa kisingizio cha soko la Dunia

Hakuna sababu ya kuwa na hao sumatra sababu hawana msaada zaidi ya kuongeza ugumu wa maisha maana katika kila nishati utakayonunua iwe Umeme/mafuta wana asilimia yao pale

Wakati serikali za wenzetu wanajaribu kupunguza matumizi ya mafuta kwa kubadili magari yenye kutumia kiwango kikubwa cha mafuta na yenye matumizi madogo sisi ndio tunabadili kwa kununua V8 utafikiri tunachimba mafuta

Halafu mtu anasema Serikali ipo nina mashaka kidogo
 
wewe unajua bei ya mafuta kitika soko la dunia? au ndio kuropoka, kama mafuta yamepanda bei kwa wanaochimba je unategemea nini kwa nchi kama Tanzania.

busara basi! Unajua kodi kwa lita ni sh ngapi? Mbona landlocked countries jirani na sisi bei chini?
 
Sasa mtt wa rais anasema tunaishi kimjini mjini kweli tutaendelea na maamuzi ya maana kweli kwenye hii nchi??hawa watu inabidi tuwashinikize mana hv hv hatutabadili kitu
 
wewe unajua bei ya mafuta kitika soko la dunia? au ndio kuropoka, kama mafuta yamepanda bei kwa wanaochimba je unategemea nini kwa nchi kama Tanzania.
Kwani kenya wamefanya nini kupunguza bei ya mafuta?sisi kwa nini hatuwezi?maana hata hiyo kodi hapa tanzania hatuoni faida yake zaidi ya kulipa kesi serikali ilizoshindwa katika mikataba ya hovyo?pia baada ya kuuwawa osama bei soko la dunia imeshuka sana chini ya $100 per barell.
 
Sio petroli na diesel tu kila nyanja ya maisha hali ni mbaya sana.Aheri wewe unaye nunua Sh. 2200,mimi hapa nilipo nanunua Sh.2300!Nakubaliana na wewe,we must do something,sio kwa ajili yetu tu,lakini hata kwa ajili ya vizazi vijavyo.Ifike mahali tuseme enough is enough.
jamani naomba nilete kilio changu kidogo! hivi huu ugumu wa maisha ni mimi mwenyewe ndo nnao u feel au ni watanzania wote???mbona kila mtu yupo kimya?
yan nimetoka kuweka mafuta saiv nimekuta lita moja ni 2,200 (yes elf mbili na mia mbili) hapo nilipo nasikia hazina haina hela na watu hawajalipwa mishahara. jaman hakuna anaye umia na hii hali mbona kimya???

Naomba msaada jamani hakuna lolote tunawezakufanya ili tubadili hii hali hata bei ya mafuta ipungue?mbona kenya wameandamana imeshuka sisi mbona tunaumia kimya kimya jaman????
 
Tatizo tulilonalo watanzania ni kwamba hatuna sera yoyote ya kupambana na mfumuko wa bei. Hivyo tunajiendea hovyo hovyo tu tofauti na nchi nyingine. Chombo kikuu serikalini cha kupambana na inflation ni benki kuu ambayo maelezo yote inapewa kutoka wizara ya fedha.
Tatizo tulilonalo watanzania ni kwamba tunapenda sana bidhaa za nje kuliko za nyumbani, bic ya kuandikia, chaki za kuandikia na madaftari vyote hutoka nje ya nchi na vikifika nyumbani bei yake huwa juu sana kulingana na ushuru wa forodha na kodi kadhaa baadaye. Nakubali bidhaa zetu za ndani wakati mwingine hazina ubora wowote wa kushindana na bidhaa za nje, hivyo basi mwathirika mkuu wa mfumuko wa bei ni end user (mtumiaji wa bidhaa) ambapo kimsingi ni mtanzania. Madhara mengine kwa ufupi ni pamoja na kushuka thamani ya pesa yetu, wafanyakazi kuhaha na kutokidhi mahitaji yao kwa kuwa inflation haiendani na nyongeza katika mishahara yao na hii ni indication kwamba uchumi wetu ni wa hovyo.
Nini kifanyike? Tuandae sera mahsusi na maalum kwa ajili ya tatizo hili na ifanyike control ya kila wiki 6 kufanya tathmini kuona kama sera imefanikiwa au lah!. Rais anaweza kuteau tume maalum kushughulikia zoezo hili na uzuri ni kwamba tunao wasomi wengi ambao wanaufahamu uchumi. Hapa akina Lipumba wana maoni ya kuliokoa taifa letu na matatizo haya. Vinginevyo tutaendelea na inflation itapanda na mwishowe tutakuwa na taifa kama lile la Zaire wakati wa Mobutu au uchumi kama wa zimbambwe, mimi nadhani keshokutwa tutachapisha noti mpya za elfu 20 na elfu 50 kupunguza circulation ya fedha mikononi mwa wananchi. Ni hayo niliyonayo ila naomba wana JF tuchangie maada hii kwa kina...
 
Think BIG, kwani kuna hivi karibuni umesikia serikali imeongoza kodi kwenye mafuta? The rest serikali ya Tanzania haimiliki visima vya mafuta....

pamoja na hayo yote serikali inakosa maujanja ya ku cntrol bei ya mafuta...wamwombe ushauri bwana mkapa awape maujanja....
 
Majirani zetu Kenya wamepunguza kodi katika mafuta ili kuwasaidia wanunuzi na pia kupunguza ongezeko la mfumo wa bei (Inflation) lakini hii Serikali yetu ya kisanii hadi hii leo haijatoa tamko lolote lile kama itapunguza kodi katika bei za mafuta ili kuwasaidia watumiaji na kupunguza inflation. EWURA ni mzigo mwingine kwa Watanzania ambao hauna manufaa yoyote yale.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom