List ya nyimbo zilizopewa majina mazuri lakini zikaimbwa hovyo hadi kushangaza!

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
3,865
5,684
1. Zanzibar ya Harmonize.
Niliposikia tangazo lake la kutoa wimbo wake wenye jina hilo nikajua tunaenda kusikia bonge la wimbo utakaotetemesha si tz tu bali afrika mashariki yote. Matokeo yake hiko kitu kilichotoka ni bora angeupa jina jingine tu. Yaani kibao ni hovyo hata kile cha yule mwanamuziki wa Afrika kusini alichokitoa miaka ya 70s kama sio 80s ni bora mara 10. Alipoteza muda wake na wetu kweli mmakonde yule.

2. Yalaiti ya alikiba
Akiwa ametoka kutoa kibao safi kabisa cha mahaba, ingawa nacho alikiharibu kwa kile cha so lonely, akatusisimua mashabiki wake kwa kututangazia ujio wa kibao cha yalaiti akishirikiana na mwanadada fulani. Kutokana na umaarufu wa jina hilo kutokana na kibao matata kilichoimbwa miaka hiyo na dada yetu shakila, basi tukajua kijana huyu kajipanga kweli kutoa kitu kitakachotikisa. Matokeo yake sijui waliimba nini na waliimbaje sijui?

Tuongeze list wadau......
 
Kalapina_kufa_au_kupona japo kamanda wa kikosi hakuniangusha kwenye umoja ni nguvu na mstari wa mbele ila kweye kufa au kupona nilijua kamanda wa kikosi ataua humo ndani kumbe ni songi la kifala kishenzi.
 
1. Zanzibar ya Harmonize.
Niliposikia tangazo lake la kutoa wimbo wake wenye jina hilo nikajua tunaenda kusikia bonge la wimbo utakaotetemesha si tz tu bali afrika mashariki yote. Matokeo yake hiko kitu kilichotoka ni bora angeupa jina jingine tu. Yaani kibao ni hovyo hata kile cha yule mwanamuziki wa Afrika kusini alichokitoa miaka ya 70s kama sio 80s ni bora mara 10. Alipoteza muda wake na wetu kweli mmakonde yule.

2. Yalaiti ya alikiba
Akiwa ametoka kutoa kibao safi kabisa cha mahaba, ingawa nacho alikiharibu kwa kile cha so lonely, akatusisimua mashabiki wake kwa kututangazia ujio wa kibao cha yalaiti akishirikiana na mwanadada fulani. Kutokana na umaarufu wa jina hilo kutokana na kibao matata kilichoimbwa miaka hiyo na dada yetu shakila, basi tukajua kijana huyu kajipanga kweli kutoa kitu kitakachotikisa. Matokeo yake sijui waliimba nini na waliimbaje sijui?

Tuongeze list wadau......
Tabulele..ovya sana.
 
Kina shida gani hiko mkuu?!!
Wimbo hauna vina, hauna mizani, hauna beat la kueleweka, hauna harmony, mtu anafoka tu stream of consciousness inakwenda kama farasi shoti aliyekosa muendeshaji, kwa sauti kama ya mtoto mwenye degedege aliyebanwa na mlango.

Ila I have to give it to Dudubaya for the storytelling.

Jamaa anawakataa wazazi wake anawaita choka mbaya, anadai wazazi waje wako Ulaya 🤣🤣🤣
 
🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom