Lissu, Zitto na Magufuli ni wazalendo wa kweli wa nchi hii..

Lisu sio mzalendo,,ni muongo sana.alitudanganya miaka 8 kwamba Lowasa ni mwizi halafu baadae akayarudia matapishi yake.huyu Lisu ni mchungaji anayetawanya kondooo
Na yule ambaye alikuwa anaitikia ndiooooo wakati wa kupitisha mikataba fake ya madini halafu sasa anaanza kuuliza nani alituloga, unadhani kichwa chake kiko sahihi?
 
Sawa sawa kabisa! Uzalendo sio maamuzi tuu! Kusikilizana kuna faida zake pia!
 
Umeandika uzi mzuri usio na ushabiki wowote.. ila ktk mtazamo wako kuna tatizo kidogo.. kwenye kipengere cha mtendaji umestate below mno, hujatambua kuwa ili lissu na zitto wafanye kazi yao vzr wanatakiwa, yule wa utendaji awe tayari kupokea mawazo yao.. Tatizo huyu unayemuita mtendaji hayupo tayari kujishusha na kukosolewa.. Anajitia umungu mtu dhidi ya ushauri wowote.
 
NAMPENDA RAIS MAGUFULI

Ni Rais mzalendo kwa nchi yake. Ana uchungu sana kuona watu wanatajirika kwa rasilimali za umma. Ni kiongozi ambaye anataka kuona watu wananufaika kwa jasho halali na siyo upigaji.

Ni Rais jasiri mno. Anaweza kuingia kwenye anga ngumu na kuzitikisa. Kujenga nchi yenye heshima unahitaji kiongozi mkuu mwenye uthubutu kama Magufuli a.k.a John The Iron 'Chuma'.

Ni Rais ambaye yupo tayari kuingia kwenye mgogoro wowote wa ama ndani au nje, mradi tu asimamie kile ambacho anakiamini.

Iwe yupo sahihi au anakosea, ikiwa yeye anajiona yupo sahihi, Rais Magufuli huwa hapindi. Husimamia anachokiamini kwa nguvu zote.

Si mnafiki, si mwoga, si wa nyekundu na njano au nusu kwa nusu, akisema nyekundu, keshokutwa utamkuta na nyekundu yake. Hana ndimi mbili.

NAMPENDA TUNDU LISSU

Siku zote hutafuta makosa ya Serikali na kuyaweka wazi. Hata pale ambapo kila mtu huamini Serikali imepatia na kuishangilia, Lissu akiibuka utampenda tu.

Anafahamu mantiki ya kuwa mpinzani kwa nchi za Afrika hususan Tanzania. Anatambua kuwa yeye si sehemu ya watu wanaopaswa kuiimbia mapambio Serikali inapofanya vizuri. Anajua kuwa uhai wa upinzani ni makosa ya Serikali na Chama Tawala, kwa hiyo anakosoa tu.

Uzuri wa Lissu ni kwamba hakosoi ilimradi aonekane anakosoa, isipokuwa hukosoa kwa hoja na vielelezo yakinifu. Lissu akizungumza, hata kama sauti yake na maneno yake yanakera lakini wewe sikiliza ujumbe, hutaambulia sifuri.

Ukiona Lissu anafungua kinywa ujue amejipanga. Japo yapo maeneo mengi huonekana mpiga kelele lakini ukiona analibebea bango jambo ujue ana hoja za msingi.

Ni faida kubwa kuwa na Lissu katika nchi hii, maana haogopi kukosoa. Haogopi nafasi ya anayemkosoa.

Katika nchi ambayo watu wengi wanaogopa kufunua vinywa vyao kumkosoa Mkuu wa Nchi, angalau sauti ya Lissu itasikika ikikosoa. Akiwa bungeni au nje ya Bunge, msamiati unaoitwa woga, haumo kichwani kwa Lissu.

Unamhitaji Lissu kumfanya mtawala asibweteke. Hata kama mtawala anafanya vizuri, uwepo wa Lissu husaidia kuchokonoa hata makosa madogo yenye kujificha na kuyaweka wazi. Katika nchi ni hasara kubwa kukosa watu wa kuikosoa Serikali.

NAMPENDA ZITTO KABWE

Mwanasiasa muungwana na mzalendo kwa nchi yake. Si mtoa lugha za kushambulia, isipokuwa hujikita katika kujenga hoja zenye kuifaa nchi.

Ni mpinzani lakini Serikali inapofanya sawa husifia. Serikali inapokosea husimama na kukosoa bila woga.

Kila jambo linalofanyika kwa masilahi ya umma hutakosa kauli ya Zitto. Kauli yake inaweza kuwa chanya au hasi kulingana na mapokeo yake.

Tabia yake ya kuisifu Serikali inapofanya vizuri na kuikosoa inapofanya vibaya, humfanya wakati mwingine ajikute anapokea mashambulizi kila upande; kutoka Chama Tawala, vilevile kwa wapinzani wenzake.

Zipo nyakati Zitto hujikuta anatofautiana na wapinzani wenzake pale anapoona hawapo sawa. Ndiye mpinzani anayeongoza kwa kushambuliwa na wapinzani wenzake, wakati huohuo akishambuliwa na watu wa utawala.

Ni mwanasiasa mwenye maono makubwa. Hoja zake si za kukosoa tu, isipokuwa hukosoa, husahihisha na kuelekeza njia ya kufikia jawabu.

Akisimama bungeni huwa hasemi "Serikali imeshindwa", bali husema " Serikali inatakiwa ifanye haya ili ifanikiwe", daima hutoa hoja zenye thamani kubwa. Hutoa hoja za dhahabu. Zitto si mlalamikaji, ni mtoaji wa ufumbuzi kisha husherehesha ufumbuzi wake.

Wakati mwingine hoja zake na namna ambavyo huzitoa kwa uchambuzi wa kina, huwafanya watu waone anajifanya anajua. Kiukweli Zitto ni fundi hasa katika kujenga hoja.

Muogope sana Zitto akizungumzia jambo baada ya kitambo japo kifupi. Hapo ujue tayari ameshasoma na ameshakuwa na pointi nyingi kichwani.

Unamhitaji Zitto kwa ajili ya kupata sura ya pili, maana anapokosoa sura ya kwanza, huja na uchambuzi wa kina kuhusu faida za sura ya pili. Ndiye kiongozi mwenye hoja mbadala.

Ni tunu kwa nchi kuwa na Zitto Kabwe. Ni kiongozi ambaye huwa hafichi hisia zake. Akiumizwa huwa hanyamazi.

HITIMISHO

Tunamhitaji Rais Magufuli kwa nafasi yake na utashi wake wa kizalendo.

Tunamhitaji Lissu kwa jicho lake la kuyasaka makosa ya Serikali na kuyaweka wazi.

Tunamhitaji Zitto kwa maono mapana na hoja mbadala zenye tija kwa taifa.

Mwisho kabisa, Rais Magufuli, Lissu na Zitto wote ni Watanzania na wanaipenda sana nchi yao. Hilo ndilo ambalo naliona kwa wote hao.

Rais Magufuli anataka mabadiliko makubwa kwenye nchi ili taifa linufaike kwa rasilimali zake, hii ni kwa sababu Rais Magufuli anaipenda sana Tanzania yake.

Lissu anakosoa mbinu ambazo Rais Magufuli anazitumia kwa sababu anaona zinaweza kuigharimu nchi. Lissu anajua kuwa nchi haiwezi kubeba gharama bila yeye kuathirika. Hii ni kwa sababu Lissu anaipenda sana Tanzania yake.

Zitto anatoa hoja za utatuzi wa changamoto za sekta ya madini, akisahihisha hatua za Rais Magufuli kwa sababu anaamini kwamba Rais Magufuli hapaswi kuachwa peke yake kwenye vita hii ya uchumi kupitia madini ya Tanzania. Hii ni kwa sababu Zitto anaipenda sana Tanzania yake.

Nawapenda sana hawa wazalendo wa nchi hii. Kila mmoja ana nia njema. Ni vizuri kusikilizana na kukopeshana kama siyo kuazimana mawazo ili kufikia mafanikio ya pamoja kama nchi.

Tanzania haina malaika, kwamba akifanya jambo asikosolewe hata kama ni jema kiasi gani. Wanaokosoa nao ni Watanzania wazalendo. Vema kusikilizana. Mwisho kabisa wote wanaipenda Tanzania.

Wasioipenda Tanzania wote wapo kimya, hawana maoni, wala hawawezi kuingia kwenye malumbano, maana wanaogopa 'kuamsha dude', wakifunua vinywa watakumbushwa usaliti wao kwa nchi na wizi waliofanya.

Kila mtu aachwe huru kutoa maoni yake. Nchi inawahitaji Rais Magufuli, Lissu na Zitto kwa wakati mmoja.

Imeandikwa na Luqman MALOTO
-----------

Mtazamo wangu: Zitto ni mchumi mzuri, Lissu ni mwanasheria mzuri na Rais Magufuli ni mtendaji na msimamia UKWELI.

Kwa maslahi mapana ya nchi, hawa watu watatu ni watu muhimu sana wakifanya kazi kwa mwendo huu huu kwa kuwa najua hawawezi kufanya pamoja..

Nchi yetu tamu sana..
Lissu hana hata chembe ya uzalendo bali ni Mbangaizaji na msaka sifa. Licha ya kuwa ni mwanasheria lakini hajui kanuni za msingi za kujenga hoja. Anauwezo mkubwa wa kuingiza misamiati ya matusi katika hoja zake,

Hana adabu kiasi kwamba aliwahi kumtusi Mwl. Nyerere wakati wa mchakato wa katiba.
 
NAMPENDA RAIS MAGUFULI

Ni Rais mzalendo kwa nchi yake. Ana uchungu sana kuona watu wanatajirika kwa rasilimali za umma. Ni kiongozi ambaye anataka kuona watu wananufaika kwa jasho halali na siyo upigaji.

Ni Rais jasiri mno. Anaweza kuingia kwenye anga ngumu na kuzitikisa. Kujenga nchi yenye heshima unahitaji kiongozi mkuu mwenye uthubutu kama Magufuli a.k.a John The Iron 'Chuma'.

Ni Rais ambaye yupo tayari kuingia kwenye mgogoro wowote wa ama ndani au nje, mradi tu asimamie kile ambacho anakiamini.

Iwe yupo sahihi au anakosea, ikiwa yeye anajiona yupo sahihi, Rais Magufuli huwa hapindi. Husimamia anachokiamini kwa nguvu zote.

Si mnafiki, si mwoga, si wa nyekundu na njano au nusu kwa nusu, akisema nyekundu, keshokutwa utamkuta na nyekundu yake. Hana ndimi mbili.
...........
HITIMISHO

Tunamhitaji Rais Magufuli kwa nafasi yake na utashi wake wa kizalendo.
.....

Tanzania haina malaika, kwamba akifanya jambo asikosolewe hata kama ni jema kiasi gani. Wanaokosoa nao ni Watanzania wazalendo. Vema kusikilizana. Mwisho kabisa wote wanaipenda Tanzania.

Wasioipenda Tanzania wote wapo kimya, hawana maoni, wala hawawezi kuingia kwenye malumbano, maana wanaogopa 'kuamsha dude', wakifunua vinywa watakumbushwa usaliti wao kwa nchi na wizi waliofanya.

Kila mtu aachwe huru kutoa maoni yake. Nchi inawahitaji Rais Magufuli, Lissu na Zitto kwa wakati mmoja. ..
Nchi yetu tamu sana..
Link Mbunge huyu ni nani na wa chama gani? Hakika anajitambua

Link2. Dr. Slaa: Nikiwa Rais nitamtia Magufuli ndani kwa kuuza nyumba za Serikali

Link3. Kaduma: JPM arejeshe nyumba za Serikali
 
uzalendo wa magu nina wasiwasi nao. kitendo cha kuwalinda wastaafu. lissu ndo mzalendo wa kweli...
 
Tobo Tundu Lissu siyo mzalendo, angelikuwa mzalendo angelipeleka kwanza maendeleo kwenye jimbo lake wana hali mbaya. Ni huyu huyu Tobo Tundu alitupiga 'biti' tukizuia mchanga tutashitakiwa. Huyu siyo mzalendo, huyu ni mnafiki na msaliti.
 
huko n
Magufuli angekuwa nje ya system ya CCM angefanya vizuri zaidi ya hivi, tatizo ni CCM ambao wanamchelewesha na watafanya Magufuli asifanye vizuri zaidi, kwa kuwa muda mwingi anautumia kwa kurekebisha makosa yao wakati mwingine ana lazimika kutumia muda mwingi kuwalinda CCM ili wasiishie jela,maana yake akiamua kufanya kazi kwa weledi hasa kwa kufuata taratibu na sheria nusu ya CCM Kama siyo wote wataishia jela,kwa hiyo mchawi wa maendeleo na Magufuli ni CCM wenyewe.

huko nje ya CCM wamejaa wajanja wajanja tu wameridhika kuwa pale sababu yao yanaenda. Alipo Magufuli sasa hivi ndio sehemu sahihi tumpe muda na tumuunge mkono
 
Lisu sio mzalendo,,ni muongo sana.alitudanganya miaka 8 kwamba Lowasa ni mwizi halafu baadae akayarudia matapishi yake.huyu Lisu ni mchungaji anayetawanya kondooo
Hahaha yaani ukianza mambo yauongo kwa hawa wanasiasa hamna atakaebaki magufuli pia mbona ni muongo ni mtu anaeongea kesho anaamka anasahau alichokiongea juzi.....hao ndo wanasiasa bwana ila ukitoa mapungufu yao kama wanasiasa naunga hoja ya mtoa mada
 
huko n

huko nje ya CCM wamejaa wajanja wajanja tu wameridhika kuwa pale sababu yao yanaenda. Alipo Magufuli sasa hivi ndio sehemu sahihi tumpe muda na tumuunge mkono
Walioko nje ya CCM hawaathiri chochote ngoma iko ndani ya CCM,athari za CCM zimemuathiri mpaka Magufuli mwenyewe ambaye amelazimika kujitoa muhanga kuwatetea baadhi ya vigogo wa CCM Ili wasikumbwe na mkono wa sheria.
 
Nampenda Magufuli

Ni Rais mzalendo kwa nchi yake. Ana uchungu sana kuona watu wanatajirika kwa rasilimali za umma. Ni kiongozi ambaye anataka kuona watu wananufaika kwa jasho halali na siyo upigaji.

Ni Rais jasiri mno. Anaweza kuingia kwenye anga ngumu na kuzitikisa. Kujenga nchi yenye heshima unahitaji kiongozi mkuu mwenye uthubutu kama Magufuli a.k.a John The Iron 'Chuma'.

Ni Rais ambaye yupo tayari kuingia kwenye mgogoro wowote wa ama ndani au nje, mradi tu asimamie kile ambacho anakiamini.

Iwe yupo sahihi au anakosea, ikiwa yeye anajiona yupo sahihi, Rais Magufuli huwa hapindi. Husimamia anachokiamini kwa nguvu zote.

Si mnafiki, si mwoga, si wa nyekundu na njano au nusu kwa nusu, akisema nyekundu, keshokutwa utamkuta na nyekundu yake. Hana ndimi mbili.

Nampenda Lissu

Siku zote hutafuta makosa ya Serikali na kuyaweka wazi. Hata pale ambapo kila mtu huamini Serikali imepatia na kuishangilia, Lissu akiibuka utampenda tu.

Anafahamu mantiki ya kuwa mpinzani kwa nchi za Afrika hususan Tanzania. Anatambua kuwa yeye si sehemu ya watu wanaopaswa kuiimbia mapambio Serikali inapofanya vizuri. Anajua kuwa uhai wa upinzani ni makosa ya Serikali na Chama Tawala, kwa hiyo anakosoa tu.

Uzuri wa Lissu ni kwamba hakosoi ilimradi aonekane anakosoa, isipokuwa hukosoa kwa hoja na vielelezo yakinifu. Lissu akizungumza, hata kama sauti yake na maneno yake yanakera lakini wewe sikiliza ujumbe, hutaambulia sifuri.

Ukiona Lissu anafungua kinywa ujue amejipanga. Japo yapo maeneo mengi huonekana mpiga kelele lakini ukiona analibebea bango jambo ujue ana hoja za msingi.

Ni faida kubwa kuwa na Lissu katika nchi hii, maana haogopi kukosoa. Haogopi nafasi ya anayemkosoa.

Katika nchi ambayo watu wengi wanaogopa kufunua vinywa vyao kumkosoa Mkuu wa Nchi, angalau sauti ya Lissu itasikika ikikosoa. Akiwa bungeni au nje ya Bunge, msamiati unaoitwa woga, haumo kichwani kwa Lissu.

Unamhitaji Lissu kumfanya mtawala asibweteke. Hata kama mtawala anafanya vizuri, uwepo wa Lissu husaidia kuchokonoa hata makosa madogo yenye kujificha na kuyaweka wazi. Katika nchi ni hasara kubwa kukosa watu wa kuikosoa Serikali.

Nampenda Zitto

Mwanasiasa muungwana na mzalendo kwa nchi yake. Si mtoa lugha za kushambulia, isipokuwa hujikita katika kujenga hoja zenye kuifaa nchi.

Ni mpinzani lakini Serikali inapofanya sawa husifia. Serikali inapokosea husimama na kukosoa bila woga.

Kila jambo linalofanyika kwa masilahi ya umma hutakosa kauli ya Zitto. Kauli yake inaweza kuwa chanya au hasi kulingana na mapokeo yake.

Tabia yake ya kuisifu Serikali inapofanya vizuri na kuikosoa inapofanya vibaya, humfanya wakati mwingine ajikute anapokea mashambulizi kila upande; kutoka Chama Tawala, vilevile kwa wapinzani wenzake.

Zipo nyakati Zitto hujikuta anatofautiana na wapinzani wenzake pale anapoona hawapo sawa. Ndiye mpinzani anayeongoza kwa kushambuliwa na wapinzani wenzake, wakati huohuo akishambuliwa na watu wa utawala.

Ni mwanasiasa mwenye maono makubwa. Hoja zake si za kukosoa tu, isipokuwa hukosoa, husahihisha na kuelekeza njia ya kufikia jawabu.

Akisimama bungeni huwa hasemi "Serikali imeshindwa", bali husema " Serikali inatakiwa ifanye haya ili ifanikiwe", daima hutoa hoja zenye thamani kubwa. Hutoa hoja za dhahabu. Zitto si mlalamikaji, ni mtoaji wa ufumbuzi kisha husherehesha ufumbuzi wake.

Wakati mwingine hoja zake na namna ambavyo huzitoa kwa uchambuzi wa kina, huwafanya watu waone anajifanya anajua. Kiukweli Zitto ni fundi hasa katika kujenga hoja.

Muogope sana Zitto akizungumzia jambo baada ya kitambo japo kifupi. Hapo ujue tayari ameshasoma na ameshakuwa na pointi nyingi kichwani.

Unamhitaji Zitto kwa ajili ya kupata sura ya pili, maana anapokosoa sura ya kwanza, huja na uchambuzi wa kina kuhusu faida za sura ya pili. Ndiye kiongozi mwenye hoja mbadala.

Ni tunu kwa nchi kuwa na Zitto Kabwe. Ni kiongozi ambaye huwa hafichi hisia zake. Akiumizwa huwa hanyamazi.

Hitimisho

Tunamhitaji Rais Magufuli kwa nafasi yake na utashi wake wa kizalendo.

Tunamhitaji Lissu kwa jicho lake la kuyasaka makosa ya Serikali na kuyaweka wazi.

Tunamhitaji Zitto kwa maono mapana na hoja mbadala zenye tija kwa taifa.

Mwisho kabisa, Rais Magufuli, Lissu na Zitto wote ni Watanzania na wanaipenda sana nchi yao. Hilo ndilo ambalo naliona kwa wote hao.

Rais Magufuli anataka mabadiliko makubwa kwenye nchi ili taifa linufaike kwa rasilimali zake, hii ni kwa sababu Rais Magufuli anaipenda sana Tanzania yake.

Lissu anakosoa mbinu ambazo Rais Magufuli anazitumia kwa sababu anaona zinaweza kuigharimu nchi. Lissu anajua kuwa nchi haiwezi kubeba gharama bila yeye kuathirika. Hii ni kwa sababu Lissu anaipenda sana Tanzania yake.

Zitto anatoa hoja za utatuzi wa changamoto za sekta ya madini, akisahihisha hatua za Rais Magufuli kwa sababu anaamini kwamba Rais Magufuli hapaswi kuachwa peke yake kwenye vita hii ya uchumi kupitia madini ya Tanzania. Hii ni kwa sababu Zitto anaipenda sana Tanzania yake.

Nawapenda sana hawa wazalendo wa nchi hii. Kila mmoja ana nia njema. Ni vizuri kusikilizana na kukopeshana kama siyo kuazimana mawazo ili kufikia mafanikio ya pamoja kama nchi.

Tanzania haina malaika, kwamba akifanya jambo asikosolewe hata kama ni jema kiasi gani. Wanaokosoa nao ni Watanzania wazalendo. Vema kusikilizana. Mwisho kabisa wote wanaipenda Tanzania.

Wasioipenda Tanzania wote wapo kimya, hawana maoni, wala hawawezi kuingia kwenye malumbano, maana wanaogopa 'kuamsha dude', wakifunua vinywa watakumbushwa usaliti wao kwa nchi na wizi waliofanya.

Kila mtu aachwe huru kutoa maoni yake. Nchi inawahitaji Rais Magufuli, Lissu na Zitto kwa wakati mmoja.

Ndimi Luqman MALOTO
 
Mmewasahau: Jaji Warioba, Mzee J.Butiku, S.H.Salim, Mkinga, Prof.Shivij, Prof.Mwesiga Baregu, Makamu wa Rais mama S. Hassan(mama huyu ana busara sana), Angela Kairuki, Anna Makinda(Mkali, lakini linapokuja suala ya Uzalendo hana mchezo)

Huyo Kairuki anauzalendo gani?
Hebu nitajie jambo ambalo nilakipekee kalifanya kwa manufaa ya nchi
 
Magufuli angekuwa nje ya system ya CCM angefanya vizuri zaidi ya hivi, tatizo ni CCM ambao wanamchelewesha na watafanya Magufuli asifanye vizuri zaidi, kwa kuwa muda mwingi anautumia kwa kurekebisha makosa yao wakati mwingine ana lazimika kutumia muda mwingi kuwalinda CCM ili wasiishie jela,maana yake akiamua kufanya kazi kwa weledi hasa kwa kufuata taratibu na sheria nusu ya CCM Kama siyo wote wataishia jela,kwa hiyo mchawi wa maendeleo na Magufuli ni CCM wenyewe.
Mkuu hapa umemaliza kila kitu!upo sahihi mia kwa mia!laiti angefanya kama yule wa Malawi!
 
Lisu sio mzalendo,,ni muongo sana.alitudanganya miaka 8 kwamba Lowasa ni mwizi halafu baadae akayarudia matapishi yake.huyu Lisu ni mchungaji anayetawanya kondooo
Magufuli naye aliuza nyumba za serikali akanunua kivuko kibovu. Leo anashangaa kwanini tumeibiwa miaka mingi
 
Na yule ambaye alikuwa anaitikia ndiooooo wakati wa kupitisha mikataba fake ya madini halafu sasa anaanza kuuliza nani alituloga, unadhani kichwa chake kiko sahihi?
Usipende kuoanisha baya kwa baya,,kwa hio wakidanganya,chadema nao ruksa kudanganya
 
Back
Top Bottom