Lissu umeshindwa kupindua meza?

Lissu umeshindwa kupindua meza?

bumilo

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2014
Posts
352
Reaction score
176
Lissu umeshindwa kupindua meza? Kuna hujuma? Wananchi hawajakuelewa? Timu yako ya kampeni ndio imepwaya? Tatizo ni ukosefu wa fedha?

Kuna tatizo kubwa sana la ajira katika nchi hii. Umeshindwa kutumia gap hilo kuwafanya wananchi wakuone kama mkombozi wao katika hili? Licha ya ajira za uchaguzi zilizotangazwa na Tamisemi nafasi 13,000 kwa nini wewe usije na sera ya kuajiri watumishi zaidi ya 50,000 huku ukilitangaza kwa nguvu zote?

Kuna watu wanateseka sana kupata mafao yao hususani waliomaliza mikataba yao au kuachishwa kazi. Nani awasemee kwa nguvu zote kama sio wewe? Kwanini hulipigii kelele sana swala hili? Naamini wananchi watakuelewa.

Suala la elimu hususani vyuoni hujalitangaza kwa nguvu zote. Sisemi kwamba hujalitangaza kabisa, hapana. Tatizo ni kwamba watu hawajakuelewa bado

Pamoja na uwepo wa hospitali na vituo vingi vya afya bado ni changamoto kubwa sana kupata Huduma bora. Njoo na mkakati mzito wa kuwaaminisha wapiga kura wakuamini na wakuchague wewe

Tunaweza kupambana na kutukanana huku mitandaoni. Lakini ukweli ni kwamba BADO MEZA HAIJAPINDULIWA. Tulioko huku mitandaoni tunaweza kuwa tunapimana kwa mipasho kutokana na mahaba ya dhati tuliyo nayo kwa wagombea wetu but uhalisia uko hivyo kwenye field yenyewe.Mikakati mizito ifanywe ili kuwaaminisha wapiga kura kuwa Lissu ndiye jawabu la changamoto nyingi zinazowakabili wananchi
 
Kwa sasa ni kuhakikisha serikali ya ccm chini ya Jemedari Magufuli inaendelea kubaki madarakani hilo ndo lamsingi kwasasa. Achana na Lissu anapoteza muda wake
20200908_091557.jpg
 
Matatizo ya nchi hii hayaitaji nguvu nyingi kuwaeleza wananchi Kama unavyo dhani.

Tatizo la ajira:watu wote wanajua Kama magufuli ameshindwa kutatua Hilo tatizo.

Elimu:dunia unajua Kama magufuli ameshindwa kwenye elimu.

Afya:dunia yote unajua Kama atufuli hana uwezo wa kuhakikisha Kila mwananchi anakuwa na bima ya Afya.

Barabara:Kila mtu anajua jinsi mzee wetu alivyopiga 10%kwenye miradi ya barabara kipindi akiwa wizarani na mpaka Sasa.

Ndege:inafahamika kwamba mikataba kikubwa ya ununuzi wa ndege imefanyikia gizani,wameuziana ndege kana kwamba wanauziana bange,hakuna anayejua kwanini mzee amelazimisha kununua ndege.

Hayo ni machache Kati ya mengi ambayo huyu mzee ameshindwa vibaya na ndio kitu pekee kinamfanya lissu afanye kampeni kwa kujidai na bila hofu ya kukosa ushindi.
 
ALIKUJA NA KIHEREHERE HUYU JAMAA, MAHESABU YAKE ILIKUA KUPINDUA MEZA FASTA. MATOKEO YAKE KAGALAGAZWA MWENYEWE. HADI ANATIA HURUMA. ALIKUJA NA KIKI YA KUSHUDIA MUUJIZA AKIDHANI NDO KERO YA WABONGO.

haaaaa haaaaaaaa. Anatia huuuuruuumaaaa.
 
Kwa mda uliobak sio rahisi kufanya effective comeback against an overwhelming enemy superiority.....kinachokupa ushindi sa hv ni mikakati madhubuti uliyoiandaa kabla ya kampeni , kutegemea sera za kampeni Tu ili zikuvushe ni hamna , thus why JPM smashed out all political assembly before, akijua miez miwili ya kampeni haiwez kumjeruhi vya kutosha kias cha kuwa out of action.
 
ILANI huwa zinawasilishwa kwa msajili wa vyama; hawezi ongopea kitu ambacho hakipo kwenye mipango yao. Hata hivyo, kwenye suala la ajira si jukumu la serikali kuajiri bali ni uchumi ndio utakaoajiri. Jukumu la serikali ni kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi ili ikue kwa kasi na kuajiri
 
Inatakiwa namba kubwa ya wapiga kura,namba kubwa si wanafunzi wa vyuo,wala si wafanyakazi wa serikali,wala si jobless waliomaliza vyuo vikuu.
Namba kubwa ni wamachinga,bodaboda,wakulima na wafugaji hasa watu walio vijijini.
Ili kushinda uchaguzi huu hasa ngazi ya uraisi ni kuleta hoja batamzinga,zitakazo leta impact kubwa kwa makundi hayo.
 
Matatizo ya nchi hii hayaitaji nguvu nyingi kuwaeleza wananchi Kama unavyo dhani.

Tatizo la ajira:watu wote wanajua Kama magufuli ameshindwa kutatua Hilo tatizo.

Elimu:dunia unajua Kama magufuli ameshindwa kwenye elimu.

Afya:dunia yote unajua Kama atufuli hana uwezo wa kuhakikisha Kila mwananchi anakuwa na bima ya Afya.

Barabara:Kila mtu anajua jinsi mzee wetu alivyopiga 10%kwenye miradi ya barabara kipindi akiwa wizarani na mpaka Sasa.

Ndege:inafahamika kwamba mikataba kikubwa ya ununuzi wa ndege imefanyikia gizani,wameuziana ndege kana kwamba wanauziana bange,hakuna anayejua kwanini mzee amelazimisha kununua ndege.

Hayo ni machache Kati ya mengi ambayo huyu mzee ameshindwa vibaya na ndio kitu pekee kinamfanya lissu afanye kampeni kwa kujidai na bila hofu ya kukosa ushindi.
Sijui ni wangapi wanajua maana huko vijijini wanaulizia hivyo vyama vya upinzani viko wapi? Na watatusaidiaje tutoke kwenye hili lindi la umaskini?
Upinzani karibuni vijijini mkiwa na majibu sahihi kwa wapiga kura!
 
Inatakiwa namba kubwa ya wapiga kura,namba kubwa si wanafunzi wa vyuo,wala si wafanyakazi wa serikali,wala si jobless waliomaliza vyuo vikuu.
Namba kubwa ni wamachinga,bodaboda,wakulima na wafugaji hasa watu walio vijijini.
Ili kushinda uchaguzi huu hasa ngazi ya uraisi ni kuleta hoja batamzinga,zitakazo leta impact kubwa kwa makundi hayo.
Na hata hivyo kundi la Kwanza ulilolitaja ni helpless kwenye upigaji kura, ni nadra kumuona mfanyakaz ameenda kupanga folen kuanzia asubhi mpak jion akipigwa jua ili apige kura , Weng hubak home na kushangilia , wanachuo nao ndo hvo ikitangazwa Tu kila mmoja akapige kura kituo alichojiandikishia 80% wanakuwa dumped out , Ukiachilia mbali mianya ambayo CCM inayo , bado wana mtaji mkubwa wa wapiga kura waaminifu , akina mama na watu wa kijijini hawa watu wanamkubali JPM Zaid ya maelezo
 
Lissu ameshindwa kivipi? Kwa Tume kuengua wagombea wa upinzani? Kwa kuvutia watu kwa fiesta za wasanii wakubwa huko usukumani (Mwanza na Geita)! Kwa kujaza watu kwa mabasi na malori ? Kwa kujaza watoto wadogo mikutanoni? Kwa sera zipi za maendeleo ya watu ambazo hazipinduliki!
 
Back
Top Bottom