Lissu umeshindwa kupindua meza?

Lissu umeshindwa kupindua meza?

Kwa masilahi mapana ya nchi yaliyotendeka yalipaswa kutendeka. Hakuna ubishi Magufuli kafanya mambo makubwa sana katika kipindi chake cha kwanza
Kuharibu ndoto za vijana ndio maslahi mapana ya nchi? Aliyekuroga alishakufa maana angekuwa hai angekuonea huruma.
 
Na hata hivyo kundi la Kwanza ulilolitaja ni helpless kwenye upigaji kura, ni nadra kumuona mfanyakaz ameenda kupanga folen kuanzia asubhi mpak jion akipigwa jua ili apige kura , Weng hubak home na kushangilia , wanachuo nao ndo hvo ikitangazwa Tu kila mmoja akapige kura kituo alichojiandikishia 80% wanakuwa dumped out , Ukiachilia mbali mianya ambayo CCM inayo , bado wana mtaji mkubwa wa wapiga kura waaminifu , akina mama na watu wa kijijini hawa watu wanamkubali JPM Zaid ya maelezo
Sijui kwanini hawalioni hili.
 
Inatakiwa namba kubwa ya wapiga kura,namba kubwa si wanafunzi wa vyuo,wala si wafanyakazi wa serikali,wala si jobless waliomaliza vyuo vikuu.
Namba kubwa ni wamachinga,bodaboda,wakulima na wafugaji hasa watu walio vijijini.
Ili kushinda uchaguzi huu hasa ngazi ya uraisi ni kuleta hoja batamzinga,zitakazo leta impact kubwa kwa makundi hayo.
Nakubaliana na wewe. Kwa sababu sasa wilayani na vijijini kwa chopa lazima aandae sera nzuri kwa ajili ya kuinua maisha ya wakulima, wafugaji na wavuvi. Timu ya kampeni ya chadema fanyieni kazi hili swala. Ni muhimu sana.
 
Kuharibu ndoto za vijana ndio maslahi mapana ya nchi? Aliyekuroga alishakufa maana angekuwa hai angekuonea huruma.
Wacha porojo bwana leta data hapa tuzichambue ni vijana wangapi wameharibiwa ndoto zao kwa kukosa fao la kujitoa (hapo naamini ulifanya utafiti) ila kama ni mawazo yako wewe na ya mme wako sina haja ya kujadiliana na wewe.

Pia inasikitisha sana kuona karne ya leo bado kuna watu wenye fikra duni kama wewe wanaamini kwenye ulozi na ushirikina.
 
Lissu umeshindwa kupindua meza? Kuna hujuma? Wananchi hawajakuelewa? Timu yako ya kampeni ndio imepwaya? Tatizo ni ukosefu wa fedha?

Kuna tatizo kubwa sana la ajira katika nchi hii. Umeshindwa kutumia gap hilo kuwafanya wananchi wakuone kama mkombozi wao katika hili? Licha ya ajira za uchaguzi zilizotangazwa na Tamisemi nafasi 13,000 kwa nini wewe usije na sera ya kuajiri watumishi zaidi ya 50,000 huku ukilitangaza kwa nguvu zote?

Kuna watu wanateseka sana kupata mafao yao hususani waliomaliza mikataba yao au kuachishwa kazi. Nani awasemee kwa nguvu zote kama sio wewe? Kwanini hulipigii kelele sana swala hili? Naamini wananchi watakuelewa.

Suala la elimu hususani vyuoni hujalitangaza kwa nguvu zote. Sisemi kwamba hujalitangaza kabisa, hapana. Tatizo ni kwamba watu hawajakuelewa bado

Pamoja na uwepo wa hospitali na vituo vingi vya afya bado ni changamoto kubwa sana kupata Huduma bora. Njoo na mkakati mzito wa kuwaaminisha wapiga kura wakuamini na wakuchague wewe

Tunaweza kupambana na kutukanana huku mitandaoni. Lakini ukweli ni kwamba BADO MEZA HAIJAPINDULIWA. Tulioko huku mitandaoni tunaweza kuwa tunapimana kwa mipasho kutokana na mahaba ya dhati tuliyo nayo kwa wagombea wetu but uhalisia uko hivyo kwenye field yenyewe.Mikakati mizito ifanywe ili kuwaaminisha wapiga kura kuwa Lissu ndiye jawabu la changamoto nyingi zinazowakabili wananchi

Buku 7 mbona shughuli?
 
Na hata hivyo kundi la Kwanza ulilolitaja ni helpless kwenye upigaji kura, ni nadra kumuona mfanyakaz ameenda kupanga folen kuanzia asubhi mpak jion akipigwa jua ili apige kura , Weng hubak home na kushangilia , wanachuo nao ndo hvo ikitangazwa Tu kila mmoja akapige kura kituo alichojiandikishia 80% wanakuwa dumped out , Ukiachilia mbali mianya ambayo CCM inayo , bado wana mtaji mkubwa wa wapiga kura waaminifu , akina mama na watu wa kijijini hawa watu wanamkubali JPM Zaid ya maelezo
Wewe inafaa kuwa mpanga mikakati wa Chadema huenda ukawasaidia. Wasichokijua ni kuwa wafanyakazi wengi siku ya uchaguzi wameshaipa jina ni siku ya mapuziko wanatamani ifike ili walale hadi saa 5 huo muda wa kupanga foleni wanadai hawana.

Kundi la walalahoi wale mnaowaita mtaji wa CCM hao hao ndio wapiga kura wa nchi hii. Msipobadilika na kutafuta namna ya kuwafikia hakika Lisu akipata nyingi ni 10% havuki hapo
 
Wanataka kutumia helikopta kukusanya watu
Hapana. Ni njia rahisi ya kuwafikia wapiga kura wilayani, majimboni na vijijini. Mbona wasikiliza sera za uhuru na maendeleo ya watu wanakuja wenyewe. Huko kwenu "watoto wengi" wanavutiwa kuja kuona shoo za bure za collabo ya nguvu ya akina Chege Chigunda, Diamond Platnumz, Banana Zorro, Ali Kiba na kadhalika....
 
ALIKUJA NA KIHEREHERE HUYU JAMAA, MAHESABU YAKE ILIKUA KUPINDUA MEZA FASTA. MATOKEO YAKE KAGALAGAZWA MWENYEWE. HADI ANATIA HURUMA. ALIKUJA NA KIKI YA KUSHUDIA MUUJIZA AKIDHANI NDO KERO YA WABONGO.

haaaaa haaaaaaaa. Anatia huuuuruuumaaaa.
Jana ndo alianza kubwabwanja kabisa
 
ALIKUJA NA KIHEREHERE HUYU JAMAA, MAHESABU YAKE ILIKUA KUPINDUA MEZA FASTA. MATOKEO YAKE KAGALAGAZWA MWENYEWE. HADI ANATIA HURUMA. ALIKUJA NA KIKI YA KUSHUDIA MUUJIZA AKIDHANI NDO KERO YA WABONGO.

haaaaa haaaaaaaa. Anatia huuuuruuumaaaa.
Hapana. Meza ilishapinduliwa tayari. Lissu yupo offensive. Na Magu yupo defensive. Sio kama 2015 ambapo kampeni zima Chadema walikuwa wakijitahidi kujibu mapigo ya CCM baada ya kumsimamisha mgombea dhoofu (elimu! elimu! elimu!) na mwenye makandokando mengi ya ufisadi. Lissu ameshaongelea haki vizuri akaeleweka. Pia ameongelea uhuru vizuri akaeleweka. Sasa lazima ajikite kwenye sera za 'maendeleo ya watu" huko kwenye umasikini mkubwa yaani mawilayani na vijijini.
 
Lissu umeshindwa kupindua meza? Kuna hujuma? Wananchi hawajakuelewa? Timu yako ya kampeni ndio imepwaya? Tatizo ni ukosefu wa fedha?

Kuna tatizo kubwa sana la ajira katika nchi hii. Umeshindwa kutumia gap hilo kuwafanya wananchi wakuone kama mkombozi wao katika hili? Licha ya ajira za uchaguzi zilizotangazwa na Tamisemi nafasi 13,000 kwa nini wewe usije na sera ya kuajiri watumishi zaidi ya 50,000 huku ukilitangaza kwa nguvu zote?

Kuna watu wanateseka sana kupata mafao yao hususani waliomaliza mikataba yao au kuachishwa kazi. Nani awasemee kwa nguvu zote kama sio wewe? Kwanini hulipigii kelele sana swala hili? Naamini wananchi watakuelewa.

Suala la elimu hususani vyuoni hujalitangaza kwa nguvu zote. Sisemi kwamba hujalitangaza kabisa, hapana. Tatizo ni kwamba watu hawajakuelewa bado

Pamoja na uwepo wa hospitali na vituo vingi vya afya bado ni changamoto kubwa sana kupata Huduma bora. Njoo na mkakati mzito wa kuwaaminisha wapiga kura wakuamini na wakuchague wewe

Tunaweza kupambana na kutukanana huku mitandaoni. Lakini ukweli ni kwamba BADO MEZA HAIJAPINDULIWA. Tulioko huku mitandaoni tunaweza kuwa tunapimana kwa mipasho kutokana na mahaba ya dhati tuliyo nayo kwa wagombea wetu but uhalisia uko hivyo kwenye field yenyewe.Mikakati mizito ifanywe ili kuwaaminisha wapiga kura kuwa Lissu ndiye jawabu la changamoto nyingi zinazowakabili wananchi

Wewe inawezekana huwa husikilizi na kuelewa....

Meza iko upside down kitambo sana.....

Cha ajabu wewe unaiona imekaa kawaida tu...

Yote hayo uyasemayo yamefungwa kwenye kifungasho kimoja tu...

Ni "...tutafumua mfumo wa KISHERIA, KIKATIBA na KIUTAWALA ili kurudisha uhuru a mamlaka kwa watu wa namna wanavyoweza kuendesha shughuli zao za kiuchumi na kijamii kwa Uhuru na haki bila bughudha..."

Hii ndiyo "general statement" inayojibu kila hoja yako hapo...

Unachoweza kushauri na mimi nakuunga mkono kabisa, ni hili;

Kwamba, aendelee kuielezea na kuifafanua hii kwa ufasaha na kwa lugha rahisi kueleweka kwa watu. Aseme ni kwanini kwa namna gani ukosefu wa UHURU na HAKI imekuwa ndiyo kikwazo cha watu kujiletea maendeleo yao ya kiuchumi na kijamii....

Na yeye na wagombea wake wote kuanzia udiwani na ubunge waeleze kwa ufasaha na lugha rahisi kueleweka ni kwa nini na vipi hii ndiyo itakuwa suluhisho la matatizo yao...

In my opinion, mpaka sasa amefanya na anafanya vizuri sana kulielezea hili. Recently ilikuwa ni Press Conference ya jana trh 9/9/2020 kwa zaidi ya masaa matatu alizungumzia hii kitu....

Kumtaka Tundu Lissu aanze kumwaga ahadi hewa tu, tutakuwa tunarudi kulekule kwenye siasa za kiCCM zilizoshindwa...

Kuna maahadi maelfu tangu Uhuru hayajawahi kutekelezwa na tumeishi ktk uongo huu mpaka leo na Magufuli anaundeleza vivyo hivyo....

Ni wakati wa kufikiri na kutenda tofauti na kwa njia tofauti....
 
Wafanyakazi ( walimu, wajeda ,watumishi mbali mbali), waliofukuzwa kazi, mama ntilie, boda boda, wamachinga, waliokosa ajira na wanyonge wote hao wanawachora tu. Ila yaliyopo moyoni ni kwenye sanduku la kura , pale meza itakopogeuzwa juu chini.

Tuendelee kupiga kampeni ,. Mwaka huu mtapigwa chini kimya kimya.
 
Inatakiwa namba kubwa ya wapiga kura,namba kubwa si wanafunzi wa vyuo,wala si wafanyakazi wa serikali,wala si jobless waliomaliza vyuo vikuu.
Namba kubwa ni wamachinga,bodaboda,wakulima na wafugaji hasa watu walio vijijini.
Ili kushinda uchaguzi huu hasa ngazi ya uraisi ni kuleta hoja batamzinga,zitakazo leta impact kubwa kwa makundi hayo.
Hapa ndipo wapinzani huwa wana feli, kutoangalia namba kubwa ya wapiga kura. Namshangaa mgombea anayedhani hasira za waliobomolewa nyumba zinaweza kumuingiza madarakani sababu ukiangalia idadi yao ni insignificant. sawa na tole la maji kwenye gunia la sukari. Mwaka 2010 wakati wa kikwete walitaka kuyatumia migomo na maandamano ya Waalimu, tuliwaambia wazi watumishi wa umma nchi hii hawazidi 400,000 hawawezi kuwasaidia kushinda, hawakuelewa matokeo yake waliyaona.
 
Hawa bado wanafanya majaribio kwenye mahabara,imekula kwao.
 
Hapa ndipo wapinzani huwa wana feli, kutoangalia namba kubwa ya wapiga kura. Namshangaa mgombea anayedhani hasira za waliobomolewa nyumba zinaweza kumuingiza madarakani sababu ukiangalia idadi yao ni insignificant. sawa na tole la maji kwenye gunia la sukari. Mwaka 2010 wakati wa kikwete walitaka kuyatumia migomo na maandamano ya Waalimu, tuliwaambia wazi watumishi wa umma nchi hii hawazidi 400,000 hawawezi kuwasaidia kushinda, hawakuelewa matokeo yake waliyaona.
Ni kweli. Yeye ni mpigania haki wa muda mrefu kiasi kwamba ndio upande anaouongelea vizuri akionyesha maendeleo ya vitu lazima yawe na haki ndani yake. Kwa sasa anatakiwa aongelee maendeleo ya watu haswà wakulima, wafugaji na wavuvi (wapiga kura wengi sana hawa). Ingawaje hata kupata uhuru na haki ni maendeleo ya watu pia.
 
Lisu hata asipopiga kampeni kuanzia Leo mpaka siku ya uchaguzi bado atafunika tu kikubwa kuwe na fair play...jamani shida ni maisha yamekua siyo miaka hii mitano
 
Kwa masilahi mapana ya nchi yaliyotendeka yalipaswa kutendeka. Hakuna ubishi Magufuli kafanya mambo makubwa sana katika kipindi chake cha kwanza
Umejiunga JF kwa mission maalum naona.
 
Back
Top Bottom