Lissu Tundu anza mchakato wa kupunguza michango lukuki TLS

moma2k

JF-Expert Member
Dec 12, 2010
1,091
1,404
Tumekuchagua kwa kura nyingi ili ufanye mageuzi makubwa TLS.
1.Kupunguza michango ya TLS.
2.Kufuta michango isiyo ya lazima.
3.Mchango wa Afrika mashariki uwe ni HIARI.
4. Kupeleka madaraka chapter(devolusion of power).
5.Chapter kupewa fedha za kiutawala. 6.Mawakili wazee above 60 yrs wasitoe mchango wa aina yoyote TLS.
7.Mawakili wapya wasitoe mchango TLS au wapunguziwe kwa mwaka moja wakati wanajipanga.
8.Bima ya afya kwa mawakili. Haya ni kuanza kuyafanyia kazi mara moja.Usipoteze muda na matamko. Mwaka moja siyo mbali.
 
tundu lissu na viongozi wenzake ni wenzake ni mashine inayo fanya kazi vyema kwahiyo kwa hilo watalifanyia kazi.
 
Hii Namba 6."Mawakili wazee above 60 yrs wasitoe mchango wa aina yoyote TLS" ni sahihi kabisa. Nia mzee wangu over 70yrs old kutokana na matatizo ya kiafya hayuko active ku-practise lakini kwa miaka kama 40 hivi amekuwa active member kwa kulipa michango yake. Sasa hivi kipato hakipo sisi watoto inatubidi tuchangashane kumlipia TLS ili kulinda status yake na mafao mengine kama yapo.

TLS inabidi wawaenzi hao wazee kwani michango yao ndio imewafikisha hapo.
Kuwafuta kwa kushindwa kulipa michango ni ukatili na kukosa shukrani na heshima kwao.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom