Lissu ni mtu ambaye anawashangaza hata CHADEMA wenyewe

ngebe

JF-Expert Member
Jun 8, 2020
1,789
5,105
kwa namna moja au nyingine mtakubaliana na mimi wadau, Lissu ameshindikana,

CHADEMA wanamshangaa
CCM wanamshangaa
ACT wanamshangaa

Na hata vyama vyote na Watanzania wengi wanamshangaa.

Lissu amebaki ni miongoni mwa watu wachache kabisa humu duniani wasiotishwa na mtu yoyote, ukiangalia kwenye mikutano yake ndani ya CHADEMA wajumbe hawaamini kabisa, ACT pia.

Inakuaje mtu aliyenusurika kifo kwa kupigwa risasi nyingi kiasi kile, amepona halafu bado hajaonyesha kutishwa na lolote? Inakuaje? anajiamini na nini?

Hakuna mtu aliyetarajia kua Lissu ataendelea na harakati zake za siasa lakini cha ajabu ni kama vile ndio moto unazimwa kwa petroli.

Lissu hana hofu kabisa ya kuogopa mtu yeyote, wapinzani wetu na wanaharakati wakishikwa tu kidogo wanaufyata lakini Lissu sijui hana hata chembe ya uoga huyu mtu?

Kwakweli wasiojulikana msimdhuru tena Lissu, huyu ni mtu wa maajabu. Muacheni aendelee kuleta amsha amsha kwenye ulimwengu wa siasa.

Angalia mwanaharakati Roma Mkatoliki aliguswa kidogo tu mpaka akaufyata akaanza kuimba taarabu akaona haitoshi akakimbia na nchi.
 
Na ukitaka kujua Lisu ni nani au kama huamin mwaka 2020 ni mwaka wa kumwaga pombe basi tume wajaribu kuiba kura za Lissu ndipo watajua hawajui.

Na hiii Magufuli atajua kama hajui kujenga hoja, kafanya siasa kwa miaka mitano lakini Antipasi atafanya kwasiku 60 na zinamtosha kumwaga pombe.
 
ngolani,

Unaweza sema hivyo kumbe akili zimemruka. Hivi unajua risasi sio nzuri?ukizipiga sana huwa zinawehusha mpigaji na mpigwaji hata kama zinamkosa.
 
Na ukitaka kujua Lisu ni nani au kama huamin mwaka 2020 ni mwaka wa kumwaga pombe basi tume wajaribu kuiba kura za Lisu ndipo watajua hawajui.... Na hiii magufuli atajua kama hajui kujenga hoja, kafanya siasa kwa miaka mitano lakin antipasi atafanya kwasiku 60 na zinamtosha kumwaga pombe
Utoto na ndoto zinazidi kupamba moto hapa barazani.
 
ngolani,

Ni kweli kabisa. This man is unique creature!

Nimemaliza kukusoma tu, nimemkumbuka mtu mmoja anaitwa Dr Ulimboka, mwanaharakati na mtetezi wa madaktari ktk utawala wa JK.

Huyu bwana viboko na makofi tu (siyo risasi za SMG na AK47) zilimfanya aufyate kimyaaaa na mpaka leo haijulikani yuko kona gani ktk Tanzania hii!!

Lakini huyu mtu aitwaye Tundu Lissu ni binadamu wa kipekee sana sana sanaaa. Huyu ni wa kumcheki na kumsikiliza kwelikweli.
 
Na ukitaka kujua Lisu ni nani au kama huamin mwaka 2020 ni mwaka wa kumwaga pombe basi tume wajaribu kuiba kura za Lisu ndipo watajua hawajui.... Na hiii magufuli atajua kama hajui kujenga hoja, kafanya siasa kwa miaka mitano lakin antipasi atafanya kwasiku 60 na zinamtosha kumwaga pombe
Siku 14 alizokaa mpaka nchini tayari zishabadilisha upepo wa kisiasa nchini
 
Back
Top Bottom