Uchaguzi 2020 Lissu na Urais 2020: Fursa na Changamoto

Oct 7, 2019
51
156
Niliwahi kuandika kuhusu nia ya Lissu kuutaka Urais wa Tanzania 2020. Huenda
chama chake kikampitisha 2020 badala ya Msigwa. Huyu ni msomi mzuri, ni mwanaharakati na ni mpinzani haswa haswa. Kwa sifa hizo anatosha sana kupeperusha bendera za Chadema Kwa sasa.

TWENDE SAWA

Huyu hakuwahi kushika nafasi kubwa za kiuongozi ila ni mwanasiasa mkubwa sana kwenye ukanda huu wa Africa Mashariki.. angelikuwa CCM huyu ni dhahiri angeliteuliwa kushika nafasi kubwa kabisa za Kiuongozi.

Ili nimzungumzie kwa haki kabisa Lissu nitatumia SWOT analysis ambayo itatupatia mambo makuu matatu (Strength,Weakness, na threats) hii ni kanuni ambayo haidanganyi na ambayo hutumiwa sana kupata uhalisia wa kitu kabla ya kuamua kufanya jambo. SWOT ya Lisu itaisaidia Jamii ambao ni walengwa wa huduma na nafasi anayoitaka Lisu kwa maana ya kwamba jamii itamfahamu kwa undani kabla ya kumchagua au kutikumchagua, itamsaidia yeye peke yake kujijua na itakisaidia Chama chake mwenyewe.

STRENGTH

1. Ni mzuri katika kujenga hoja, ukikutana naye kwenye hoja hasa zilizo na uelekeo wa fani yake ya Kisheria atakupoteza kabisa. Tuneshuhudia Bungeni mara nyingi akitoa somo la kutosha kuhusu kanuni za bunge na matumizi yake.

2. Akiwa kama wakili ameshinda kesi nyingi sana zake binafsi na zile alizosimamia watu wengine. Lisu ni mojawapo ya mawakili ambao wakisimamia kesi yako unakuwa na uhakika wa kushinda.

3. Ana jiamini sana katika kile anachokiamini, hata kama wengine wote watakataa kumuunga mkono yeye atapambana mwenyewe.

4. Ana ujasiri wa aina yake, Lissu sio mtu mwoga anaweza kupambana na yeyote yule bila kujali status kwenye jamii. Kwa hali ya kawaida ni vigumu kumshambulia Rais wa nchi lakini Lisu alijitoa kufanya hivyo. Ni watu wengi toka mataifa mbalimbali ambao hawawezi hiki kitu.

5. Hutimiza majukumu yake kisiasa sio kiutendaji ipasavyo, kuna wakati watu walimtilia Shaka kuwa Lisu si Mzalendo lakini kwa nature ya kazi yake ndani ya Upinzani alikuwa sahihi kutukosoa. Kilichotakiwa kufanywa kilikuwa ni kuchukua alichokuwa anakisema na kukifanyia kazi.

WEAKNESS

1. Kipingamizi cha kwanza cha Lissu hana agenda ya msingi ya Kiuchumi ya kumpeleka Ikulu zaidi ya kuwa mkosoaji mkubwa. Lisu anapaswa sasa kuanza kuonyesha Plan B zake katika maswala ya kitaifa yaani kama jambo limefeli yeye kama yeye angelifanyaje.

Naamini na ndivyo ilivyo kiongozi mzuri ni yule mwenye maono yake juu ya mambo flan yaani mawazo yake binafsi na sio ya kuandikiwa (Ilani) na ndio maana hata Rais wetu kuna saa anaweka ilani Pembeni na kunyoosha kwa namna anavyoamini yeye.
Lisu anatakiwa sasa atuonyeshe nje ya Ukosoaji wake nini plan na Dira yake kwa taifa hili.

2. Tundu Lissu ni mojawapo ya wanasiasa ambao wanapatwa na jazba kwa haraka hasa pale wanapotaka kuzidiwa na hoja.

Amekuwa akitamka maeneo ambayo mara nyingi huleta ukakasi masikioni mwa watu. Mara nyingi na kiutamaduni huwa tunasema Marehemu huwa hashambuliwi lakini Lisu bila kujali aliwahi kumshambulia Mwl Nyerere kipindi cha bunge la Katiba. Kwa heshima ya Mwl Nyerere Lisu hapa alikosea.... na anapaswa kujirekebisha.

3. Udhaifu mwingine wa Lisu ni makundi na urafiki usioeleweka alio nao na mwenyekiti wa chama chake. Kwa ufahamu wa sheria alionao Lissu alishindwa kuonyesha ni wapi kina Mwigamba, Kitila na Zitto walikosea hadi akasimamie kesi zao za kufukuzwa Chadema. Lisu ana Urafiki mkubwa sana na nwenyekiti na mwenyekiti amekuwa akimtumia Lisu kwa maslahi yake binafsi kuliko kukisaidia Chama.

Kama Lissu angelisimama katikati bila kutekwa na kundi la Mwenyekiti huenda angelinusuru kina Zitto kufukuzwa na angelikuwa amekisaidia sana chama kwa kuwabakisha watu muhimu sana kwenye chama. Lisu anaonekana kama anamwogopa sana Mwenyekiti na ushauri anaompa mwenyekiti ni lazma uwe na manufaa kwa Mwenyekiti.

OPPORTUNITY

1.Lisu bado ana fursa inayomzunguka na fursa kuu ni Tukio lililomtokea. Yaani tukio la kupigwa marisasi kwake ni fursa number moja. Kwa lugha ya malkia tunasena CONFLICT has two sides one At the best it Provides an opportunity to learn and a chance for innovation. And second At the worst it destroys individual, block up families and halts production Within organisation. Kwa tafsiri isiyo rasmi Mgongano na Misuguano INA pande mbili unaweza kutumia kujijenga na unaweza kukuharibia kabisa. Kama Lisu atachanga karata zake vizuri tukio like litamjenga zaidi na limeshaanza kumjenga.

2. Fursa ya pili ni kuwa watu wenye age yake kisiasa ndani ya Chama wameanza kupotea kwa Hoja. Watu kama Mnyika walikuwa wanaweza kumletea Upinzani ndani ya Chama ila siku hizi Mnyika ni Togwa.

THREATS

1. Jimboni kwake mambo si mazuri sana, yaani kwa umaarufu alionao haulingani na maendeleo aliyoyapeleka kwenye jimbo lake. Bado jimbo lake ni mojawapo ya majimbo maskini kimiundombinu na hata kipato cha mtu mmoja mmoja. Hii inatokana na yeye kutumika mno Kitaifa na kusahau jimboni kwake. "Kuna msemo unaosema Charity begins at Home" Lisu anatakiwa afanye mambo makubwa ambayo yatafanya kila mtu Jimboni kwake amkubali na hata Singida yote.

2.Kipingamizi kikubwa cha Lisu kwa sasa ni Afya yake. Lisu anatakiwa kwa sasa apiganie zaidi Afya yake kuliko kitu kingine kile.
3. Lisu yupo kama Mwigulu Ndani ya CCM kuwa haamini kuna mawazo Productive njee ya Chama chake. Yaani yeye anaamini kila siku CCM Inakosea hii si sifa ya kiongozi mzuri.

4. Hatari nyingine kwa Lisu ni kitendo chake cha kupenda kuattack Personalities badala ya kujikita kwenye hoja za nchi hii inatakiwa iende wapi. Tuliona alivyokuwa anamkosoa Personally Rais Magufuli badala ya kukosoa Sera na kuonyesha njia. Hata juzi juzi alikuwa anaongelea kitu personally sana kuhusu Kiingereza cha Rais. Mtu anayetaka urais anatakiwa kuwaza mbali sana sio vitu vidogo kama hivyo.

5. Ukaribu unaotaka kujitokeza kati yake na Zitto, who knows Zitto katumwa? Mara nyingine tu hata Upinzani wenyewe wamekuwa wakimtuhumu Zitto kuwa haaminiki. Zitto anaweza kutumia pia yeye Lissu kama ngazi yake ya kisiasa. Kwa sasa ACT wameshalisoma gape na hata Chadema wenyewe wameshaanza Minongono kuwa Zitto hapaswi kuunda ushirika na Lissu. Kwa sasa Brand ya Lisu ni Kubwa kuliko Zitto hivyo hatujui Hesabu za Zitto zipoje. Makachero wa Chadema wanapaswa kufuatilia hili kwa umakini mkubwa.

6.Mwisho kabisa hatari aliyonayo Lisu ni CCM, sio kwamba CCM imelala kutaka kuzima ndoto za Lisu kuendelea kushine kwenye Siasa. CCM bado ina Deal naye kwa umakini mkubwa kuhakikisha Lisu hachanui zaidi ya hapo Bali anazidi kufifia kisiasa.
Screenshot_2020-06-06 (9) Thadei Ole Mushi Facebook.png
 
Wangalau uchambuzi huu unaridhisha kwani haiko biased sana. Ni nadra sana kupata wachambuzi wa aina hii kwa sasa hapa jukwaani.

Ukweli hata mimi naikubali cdm na ninamkubali sana Lisu. Lakini siamini kama Lisu anaweza kuwa rais mzuri. Tabia ya Lisu inafanana sana na tabia ya Magufuli. Tatizo ninaloliona kwa Magufuli kujikita kwenye miundombinu na kusahau karibia kila kitu, naona pia tutalipata kwa Lissu kujikita zaidi katika mifumo ya kisheria. Ila kama sasa tumejikita kwenye miundombinu na tunaaminishwa ni sawa, acha tumchague huyo Lissu naye ajikite kwenye mifumo ya kisheria na kiutawala. Huenda tukapata katiba ya wananchi. Hadi hapo tutakapoona hatufanyi sawa kama taifa ndio akili itaturudia kwa kutengeneza mifumo, na sio kutengeneza taifa la kuongozwa na utashi wa rais aliye madarakani.
 
Wangalau uchambuzi huu unaridhisha kwani haiko biased sana. Ni nadra sana kupata wachambuzi wa aina hii kwa sasa hapa jukwaani.

Ukweli hata mimi naikubali cdm na ninamkubali sana Lisu. Lakini siamini kama Lisu anaweza kuwa rais mzuri. Tabia ya Lisu inafanana sana na tabia ya Magufuli. Tatizo ninaloliona kwa Magufuli kujikita kwenye miundombinu na kusahau karibia kila kitu, naona pia tutalipata kwa Lissu kujikita zaidi katika mifumo ya kisheria. Ila kama sasa tumejikita kwenye miundombinu na tunaaminishwa ni sawa, acha tumchague huyo Lissu naye ajikite kwenye mifumo ya kisheria na kiutawala. Huenda tukapata katiba ya wananchi. Hadi hapo tutakapoona hatufanyi sawa kama taifa ndio akili itaturudia kwa kutengeneza mifumo, na sio kutengeneza taifa la kuongozwa na utashi wa rais aliye madarakani.
Very true japo kuna watu hapa watakuja wataanza kutukana badala ya kuchangia kwa ustaarabu.
 
Hapo kwenye THREATS" kuna upogo kidogo kwenye hoja yako. Na nafikiri labda hata wewe kidogo ufahamu wako kwenye baadhi ya mambo uko tenge kidogo....

Mimi nikukosoe kwenye eneo moja tu na mengine watasema wengine...

#Lissu na maendeleo jimboni kwake
- Kwamba hajaleta maendeleo jimboni, watu wake masikini na social services kwa ujumla ni hovyo

- Ukamalizia kwa kusema "Charity begins at home"

MASWALI KWAKO;

1. Hivi ni nani hasa wa kupeleka maendeleo ktk jimbo la uchaguzi lolote? Mbunge au serikali?

2. Nafahamu kazi ya mbunge kubwa ni kupeleka kero ama mahitaji ya watu wake huko bungeni/serikalini kwa ku - shout ili kero fulani zitatuliwe kibajeti au kisera....

Je, unadhani Lissu ktk umri wake wote wa ubunge hakutimiza wajibu huu muhimu wa uwakilishi kwa watu wake waliomchagua kwa awamu mbili?

3. Kila Jimbo la uchaguzi Tanzania lazima limo ndani ya halmashauri fulani ya jiji, manispaa, mji, ama wilaya na mkoa fulani. Huko wako viongozi kibao wa serikali mathalani DC, DEDs, RCs DSO, na wengine wengi tu ambao kiuhalisia hawa ndiyo ma - in charge wa shughuli za kijamii na maendeleo ya siku kwa siku ktk maeneo yao ya kiutawala....

Ndo tuseme hawa wote wanakuwa hawaoni kuwa eneo fulani ktk vijiji, miji, ama kata na wilaya kwa ujumla wananchi hawana maji, shule, kituo cha afya nk hadi tu wamsubiri mbunge?? Ni nini nafasi na uwepo wao kama lawama zinakwenda kwa mbunge? Kwa akili yako unadhani hii ni sawa?

MWISHO:
Kwa mfumo wetu wa utawala wa kisiasa na kijamii, ni ngumu kwa mbunge asiyetokana na chama kilicho madarakani na mkosoaji mkubwa wa serikali hiyo, jimbo lake la uchaguzi likapata bajeti ya maendeleo ktk miradi mbalimbali...

Kwa sababu kwa mfumo wa utawala wetu ukiwa mbunge wa upinzani na ukataka jimbo lake lipate favour, basi lazima u - compromise na utawala wa serikali iliyopo...

Ktk hali hii na kwa "nature" ya mtu kama Tundu Lissu huyu kamwe hawezi ku - compromise na Rais John Pombe Magufuli na CCM na ni bahati njema kuwa na wewe mwenyewe umelisema hili ktk uchambuzi wako kwanini yuko hiyo, is a person with his own and unquestionable stands...!!

Ndivyo ilivyokuwa kwa Tundu Lissu. Na kuthibitisha hili, immediately baada ya jimbo kupata mbunge yule wa Viti maalumu - CCM (Miraji Mtaturu) - chama cha Rais aliyeko madarakani hata kabla mbunge huyo kusimama bungeni kusema lolote, haraka haraka Rais Magufuli aliamuru pesa bilioni kadhaa ziende jimboni kwa Lissu kwa ajili ya mradi fulani wa maji...!!

Unasemaje hapo? Hiyo SWOT analysis yako inafaa kweli kufanya kazi ktk mazingira hayo??... Ukiitumia na kuja na conclusion yoyote, utakuwa hujitendei haki mwenyewe na nafsi yako....!!
 
Asante sana mkuu. Kwa wale wahusika huu ni uchambuzi mzuri kwa maoni yangu. Ni vyema chambuzi kama hizi zikafanyiwa kazi kwa maslahi mapana zaidi.
 
Wangalau uchambuzi huu unaridhisha kwani haiko biased sana. Ni nadra sana kupata wachambuzi wa aina hii kwa sasa hapa jukwaani.

Ukweli hata mimi naikubali cdm na ninamkubali sana Lisu. Lakini siamini kama Lisu anaweza kuwa rais mzuri. Tabia ya Lisu inafanana sana na tabia ya Magufuli. Tatizo ninaloliona kwa Magufuli kujikita kwenye miundombinu na kusahau karibia kila kitu, naona pia tutalipata kwa Lissu kujikita zaidi katika mifumo ya kisheria. Ila kama sasa tumejikita kwenye miundombinu na tunaaminishwa ni sawa, acha tumchague huyo Lissu naye ajikite kwenye mifumo ya kisheria na kiutawala. Huenda tukapata katiba ya wananchi. Hadi hapo tutakapoona hatufanyi sawa kama taifa ndio akili itaturudia kwa kutengeneza mifumo, na sio kutengeneza taifa la kuongozwa na utashi wa rais aliye madarakani.

Magufuli yupo na miundombinu,kwa sababu ndivyo ana experience navyo,lol...tunahitaji mtu mwenye uzoefu na Community development.lol
 
Mleta.mada siku hizi hakuna SWOT Kuna SWOC ile kitu.mlisoma zamani inayoitwa Threat haipo imekuwa replaced na challenges

Threat haipo Tena duniani
Binadamu anataka kuweza kila kitu, hivyo matishio (yaliyokuwa yanampa woga) siku hizi anaziita changamoto (Ili iwe rahisi kuzikabili).
 
Mleta.mada siku hizi hakuna SWOT Kuna SWOC ile kitu.mlisoma zamani inayoitwa Threat haipo imekuwa replaced na challenges

Threat haipo Tena duniani
Mkuu,, Hebu tuambie hiyo SWOC imeanza kutumika lini?
 
Mkuu,, Hebu tuambie hiyo SWOC imeanza kutumika lini?
Ina miaka zaidi ya kumi .Threats inataka ukimbie challenge unatakiwa kukabiliana nayo kilichobadikika Ni kuondoa threat na. Kuweka challenges kwa waliosoma zaman wanafanya SWOT analysis modern management inatumia SWOC analysis
 
Umeandika mengi; mengine kwa mtazamo wangu naona umekosea, na mengine naona umepatia.

Mfano
Maendeleo jimboni kwake; hapa umenishangaza sana, kama mtu anaeonekana ana uelewa kama wako nae anaamini mbunge, tena wa upinzani ana jukumu la kupeleka maendeleo jimboni kwake!, Lissu hakusanyi kodi.

Kwa utawala huu wa Magufuli anavyochukia wapinzani; na hasa Lissu, ulitegemea hayo maendeleo jimboni kwa Lissu yapelekwe kweli?! mara ngapi tumemsikia Magufuli akisema hapeleki maendeleo kwa wapinzani? hapa naona umeyumba.

Nakubaliana nawe zaidi kwenye ajenda ya kiuchumi ya Lissu - hapa tuko pamoja; lakini hata kwenye suala la makundi kati ya Lissu na Mbowe kulikosababisha kufukuzwa Zitto, Kitila, na wenzake; hapa nakupinga kwa hoja nzuri tu: NINAZO, tatizo muda.

Mwisho kabisa, lazima ujue kazi ya Rais sio binafsi, Rais ana washauri, ana wasaidizi, ni jukumu lake kuwasikiliza hao washauri ili awe Rais bora, hivyo wote mnaom-judge Lissu kwamba atakuja kuwa kama Magufuli au sio presidential material hii hoja yenu haina msingi, hakuna binadamu aliekamilika asilimia 100.

Kinachomuharibia zaidi Magufuli ameshathibitisha kwa vitendo hataki ushauri wa mtu, anafanya anayoyapenda, hivyo mpaka Lissu nae atapopewa nafasi ndio tutahakikisha kama na yeye kweli ana tabia kama za Magufuli, na anayatenda kama Magufuli; na zaidi anaogopwa na wasaidizi wake kama Magufuli, na hakuna wala hapatatokea candidate yeyote wa nafasi ya Urais nchini ambae atakuwa hana fani yoyote ili tumuamini akipewa madaraka ata-perform kwa asilimia zote kwenye kila angle.

Kusikiliza wengine ndiko kunamfanya Rais awe bora, huwezi kumhukumu mtu kabla ya kumpa nafasi ya kutenda, hili ni sawa na wanaosema wapinzani hawastahili kupewa nchi watafanya kama CCM, How! wapeni nafasi muone mapungufu yao mthibitishe, kama Lissu nae anavyostahili kupewa hiyo nafasi, msihukumu kwa hisia.

Hakuna binadamu asie na Weakness na Strengths, wote tunazo; hizi ni sawa na tabia, kila mwanadamu ana tabia zake, huwezi kupingana na hili utakuwa against nature, hivyo hakuna sababu ya kumuogopa mtu just because of that.

Kama yupo wa kuipinga hoja yangu ajitokeze; ataje sifa za Rais kuitwa "presidential material" tuzijue, halafu tuone ni Rais yupi kati ya tuliowahi kuwa nao alikuwa na hizo sifa zote, na akazitekeleza baada ya kupewa majukumu.

Lazima mjue jambo moja, hata Rais kuwa mpole kupitiliza kama Kikwete, bado hakumfanyi kuwa Rais bora, zaidi ataacha wajanja wachezee rasilimali za taifa kama ilivyotokea awamu iliyopita, hivyo kumbe hata huyu nae alitakiwa kusikiliza washauri wake, inavyoonekana japo alikuwa mpole, but hakuwa anasikiliza kila alichoshauriwa na wasaidizi wake.
 
Mungu ndie ajuaye dhamira yake na visasi vilivyomsonga moyoni mwake hawezi pata hata kura mil 2,atajuta na atakuwa amepotea kisiasa.
Mshaurini vizuri hatokuja kuamini!
Sorry sio mwanasiasa. Lakin kuja hapa kushtaki as if ww na Mungu mnaishi nyumba moja, umepotea.
Mungu si kikaragosi cha siasa.. haamuliwi na mtu anaamua mwenyewe.
Hakuna ajuae kesho yetu, tumuachie Mungu afanye maamuz yake.. lakin si kuwa msemaji wake.
 
Back
Top Bottom