Lissu, Mhariri wa Mawio wafikishwa kizimbani leo

Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
27,263
16,288

Wakili wa upande wa utetezi alikuwa ni Wakili Msomi Peter Kibatala na washitakiwa waliofika ni namba 2 na 3 ambao ni Bwana Ismair na Mkina washtakiwa wengine akiwepo Tundu Antiphas Lissu hawakuhudhuria mahakamani kwa sababu mbalimbali.

Mashitaka walisomewa ni matano na washitakiwa wote ndugu Mkina na Ismair walikataaa mashitaka yote matano.

Pia kwasababu washitakiwa wengine hawapo akiwepo Tundu Antiphas Lissu, mahakama iliombwa itoe wito kwa washitakiwa kufika mahakamani.

Peter Kibatala akisaidiwa na mawakili wawili anawaombea washitakiwa walioko mahakamani mdhamana kwa masharti nafuu. Kwasababu wametii na kujisalimisha mahakamani wenyewe. Dhamana ilikuwa wazi kwa washitakiwa hao wawili, na kila mmoja anatakiwa kudhaminiwa na watu wawili watakaoweka saini ya Bond

Washitakiwa woote walipewa dhamana na kesi itatajwa tena tarehe 28/06/2016

===============================

Serikali itawafikisha Mahakama ya Kisutu leo, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na mmiliki wa gazeti lililofungiwa la Mawio, Simon Mkina kwa kuandika habari za uchochezi.

Mkina alisema baada ya kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi kuwa kwa mara ya kwanza watafikishwa mahakamani.

“Nimekuja kama ilivyo amri kufika hapa kila siku asubuhi, ila nimeambiwa kesho ( leo ) tunatakiwa kufika mahakamani na wenzangu,” alisema Mkina.

Katika kesi hiyo, atakuwapo pia mhariri na mwandishi wa habari iliyosababisha kufungiwa, Jabir Idrisa pamoja na mchapishaji wa gazeti hilo.

Lissu ameunganishwa katika kesi hiyo kwa madai ya kutoa kauli za uchochezi zilizoandikwa kwenye gazeti hilo.

Pamoja na Gazeti la MAWIO kufungiwa Januari mwaka huu baada ya kudaiwa kuandika habari za uchochezi zilizohusu mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar ikiwa na kichwa cha habari ‘Machafuko yaja Z’bar’ katika toleo lake la 182 la Januari 14-20, 2016, bado serikali inawang’ang’ania.

Akizungumza na wanahabari Mkina alilaumu kitendo cha polisi kukamata hadi watoa maoni wa gazeti.

Mkina alisema, serikali inabana uhuru wa habari pia kunyima fursa ya kuikosoa hata kama imefanya mabaya.

Zaidi soma;
DPP awafutia Tundu Lissu na Wahariri wa Gazeti la Mawio kesi ya Uchochezi
 
Tena kwa speed ya 4G
IMG-20150711-WA0045.jpg
 
Serikali imeshindwa kuwatumikia wananchi imekalia kushindana na wakosoaji wake, mwambie jamaa yenu asidhani siku zinarudi nyuma, kama anaona miaka 5 mingi basi aendelee kuamini tu,
Labda atafanya kama walivyofanya zanzibar, kwa mwendo huu wengi tumeshamchoka mapemaaaa.
 
Serikali imeshindwa kuwatumikia wananchi imekalia kushindana na wakosoaji wake, mwambie jamaa yenu asidhani siku zinarudi nyuma, kama anaona miaka 5 mingi basi aendelee kuamini tu,
shangaa sasa
haitaki kukosolewa
kuambiwa
wala kusemwa

hivi hata kama ni mwanao anaweza kujirekebishaje bila kumkanya ama kumkosoa
 
Serikali itawafikisha Mahakama ya Kisutu leo, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na mmiliki wa gazeti lililofungiwa la Mawio, Simon Mkina kwa kuandika habari za uchochezi.

Mkina alisema baada ya kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi kuwa kwa mara ya kwanza watafikishwa mahakamani.

“Nimekuja kama ilivyo amri kufika hapa kila siku asubuhi, ila nimeambiwa kesho ( leo ) tunatakiwa kufika mahakamani na wenzangu,” alisema Mkina.

Katika kesi hiyo, atakuwapo pia mhariri na mwandishi wa habari iliyosababisha kufungiwa, Jabir Idrisa pamoja na mchapishaji wa gazeti hilo.

Lissu ameunganishwa katika kesi hiyo kwa madai ya kutoa kauli za uchochezi zilizoandikwa kwenye gazeti hilo.

Pamoja na Gazeti la MAWIO kufungiwa Januari mwaka huu baada ya kudaiwa kuandika habari za uchochezi zilizohusu mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar ikiwa na kichwa cha habari ‘Machafuko yaja Z’bar’ katika toleo lake la 182 la Januari 14-20, 2016, bado serikali inawang’ang’ania.

Akizungumza na wanahabari Mkina alilaumu kitendo cha polisi kukamata hadi watoa maoni wa gazeti.

Mkina alisema, serikali inabana uhuru wa habari pia kunyima fursa ya kuikosoa hata kama imefanya mabaya.
mwka huu nakwmbia CCM wameshikw pabaya wanatafuta pa kutokea! utashinda tyuu Mr Lissu! haki huwa haipotei milele daima!
 
watawala wetu bhana mnadhani miaka iarudi nyuma? subirini mkipazunka 2020 hiyo ili tuheshiumiane!
 
Serikali imeshindwa kuwatumikia wananchi imekalia kushindana na wakosoaji wake, mwambie jamaa yenu asidhani siku zinarudi nyuma, kama anaona miaka 5 mingi basi aendelee kuamini tu,
Yaani ni kinyume chake wabunge wameshindwa watumikia wananchi wamekalia makesi kila kukicha!
 
Serikali imeshindwa kuwatumikia wananchi imekalia kushindana na wakosoaji wake, mwambie jamaa yenu asidhani siku zinarudi nyuma, kama anaona miaka 5 mingi basi aendelee kuamini tu,
Acha ujinga!!
Magufuli na mahakama wapi na wapi?
Mbona mnakuwa wajinga kiasi hicho?
 
Serikali imeshindwa kuwatumikia wananchi imekalia kushindana na wakosoaji wake, mwambie jamaa yenu asidhani siku zinarudi nyuma, kama anaona miaka 5 mingi basi aendelee kuamini tu,
Ashakata tamaaa ya kuendelea kuwepo ndio maana unayaona haya
 
Back
Top Bottom