Lissu: Makampuni yaliyotunyonya tangu 90's hayapo kwenye sheria ya madini

Eti "professorial rubbish"....hahahaaaaaaaaaa!

Hivi Trillioni 108 watu weupe wakupatie hivi hivi tu, in a silver plate!? Hawajawa wajinga na mazezeta wa kiwango hicho.

Hebu tuwe serious kidogo.
 
Tulimwambia aje kutoa maoni akakimbia sasa hivi anakuja kujivua nguo na porojo zake za MIGA
acha kujidhalilisha toka mwaka 1995 anatoa maoni kwani si yapo kwenye makaratasi kama mngetaka kutumia mngetumia.
pili,unaonenaka tahira unaposema kuwa mulimwambia atoe maoni hakuja-hapa ni sawa na kukiri kuwa sheria hii mpya maoni yaliyofanyiwa kazi ni ya watu vilaza ndio maana imekuja sheria hiyo mbovu ,licha ya kutukana wenzako pia unajitukana mwenyewe
 
acha kujidhalilisha toka mwaka 1995 anatoa maoni kwani si yapo kwenye makaratasi kama mngetaka kutumia mngetumia.
pili,unaonenaka tahira unaposema kuwa mulimwambia atoe maoni hakuja-hapa ni sawa na kukiri kuwa sheria hii mpya maoni yaliyofanyiwa kazi ni ya watu vilaza ndio maana imekuja sheria hiyo mbovu ,licha ya kutukana wenzako pia unajitukana mwenyewe
Nafasi imetolewa ya kuchangia mjadala wa kisheria eti mmataka mwaka mzima...huu ni ukilaza wa kiwango cha PHD
 
Aiseeeeeeeee....ina maana hizi sheria mpya hazitahusu kampuni za madini ambazo ziko nchini tayariiiiiii?????????????????????????????.?.............???????
So Acacia hawataguswa na sheria hii? Hii ni kweli jamani?????????? *Hivi ni sehemu gani ya nchi yetu yenye madini na hayana mwenyewe tayari*? Mmmmmmmhhh...!!!

Nahitaji kujua.. Eeeeeeeeehhhhhh...!!
 
Tundu Lissu kuonyesha yuko vizuri angewapa ushauri wa bure na technicalities ya vipi tutanasuka katika hili
Bob hebu utuambie Unawashauri vipi wasioshaurika na wanaoamini kwamba kila ushauri wanaopewa na mtu yeyote wa itikadi tofauti na yao ni mbaya?!
 
Leo Bunge linajadili Muswada wa marekebisho ya sheria za madini na za kodi katika sekta ya madini.

Makampuni ya kigeni ambayo yametunyonya tangu miaka ya mwisho ya '90, na yanaendelea kutunyonya hadi sasa, hayapo kwenye mjadala huu.

Acacia Mining PLC, ambayo Magufuli na maprofesa wake wamedai imetupiga zaidi ya shilingi trilioni 139 wakati haina hata leseni ya uchimbaji madini, nayo haipo kwenye mjadala huu.

Kama nilivyotabiri mwezi uliopita, Magufuli amesalimu amri mbele ya makampuni haya na mbele ya Acacia Mining PLC.

Naomba kufafanua.

Muswada unaojadiliwa leo umetamka wazi kuwa mikataba ya uendelezaji madini iliyopo sasa itaendelea.

Hii ni pamoja na mikataba ya Acacia Mining PLC kuhusu Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara. Kwa Muswada huu, mikataba hii ni halali.

Kusalimu amri huku kwa Magufuli kuna maana kubwa sana.

Mjadala wa makinikia ya dhahabu sasa ndio umezikwa rasmi.

Kama mikataba ya Acacia Mining PLC ni halali, maana yake ni kwamba usafirishaji wa makinikia ulikuwa halali muda wote. Watayarudishiwa makinikia yao kimya kimya.

Sidhani kama tutamsikia mtukufu Rais wetu akizungumzia makinikia tena. Na mtakaong'ang'ania tuyajadili mtaanza kutishwa ili mnyamaze.

Hayo matrilioni ya akina Prof. Mruma na Prof. Osoro ndio hatutayasikia tena. Yalikuwa ni ya uongo, 'professorial rubbish', tangu mwanzo.

Ndio maana hata wabunge wameambiwa Taarifa za hao wasomi wabobezi ni mali ya Rais peke yake. Wengine haturuhusiwi kuziona.

Kama mikataba ni halali kwa mujibu wa Muswada wa leo, maana yake nyingine ni kuwa waliohusika kuiandaa au kuisaini hawana kosa lolote.

Hoja ya kuwashtaki akina Chenge, Ngeleja, Muhongo na wengineo waliotajwa kwa majina na Kamati ya Prof. Osoro, nayo sasa ni marehemu.

Kama mikataba ni halali watakamatwa na kushtakiwa kwa kosa gani???

Kwa hiyo, kwenye signature issue yake kubwa juu ya rasilmali zetu, huyu anayeitwa mtetezi wa wanyonge na mlinzi wa rasilmali zetu, ameshindwa vibaya. Magufuli ameshindwa, kama nilivyosema atashindwa.

Kwa Muswada huu, Magufuli ameendeleza na kuhalalisha matendo ya watangulizi wake Mkapa na Kikwete ya kugawa rasilmali zetu kwa wageni.

Kwa Muswada huu, waliotunyonya na kutuibia juzi na jana na wanatuibia leo, wataendelea kutunyonya na kutuibia kesho na kesho kutwa.

Muswada wa leo unafanya mabadiliko makubwa ya kisheria kwa makampuni yatakayokuja miaka ijayo.

Sawa kabisa. Lakini naomba Magufuli na wapambe wake watusaidie hili: hivi ni sehemu gani ya nchi yetu ambayo ina madini na hayana mwenyewe tayari???

Ni sehemu ipi ya eneo letu la bahari au eneo maalum la kiuchumi ambalo bado halina mikataba ya kutafuta au kuchimba mafuta au gesi asilia???

Nchi hii ilishagawanywa vipande vipande na kupewa wawekezaji wakati wa Mkapa na Kikwete.

Muswada huu ni mzuri kwenye karatasi, kiuhalisia sheria yake haitatekelezeka kwa sababu mali tayari ilishauzwa na Muswada huu umebariki biashara hiyo.

Magufuli na watu wake hawataki watanzania wajue hili. Ndio maana Muswada unaletwa kwa dharura, ili kusiwe na mjadala wowote wa kuna.

Baadae kidogo nitazungumzia Sheria mpya zilizopitishwa jana kwa mpigo na kwa Hati ya Dharura. Sheria hizo ni uongo mwingine mkubwa kwa watanzania.
Kuwa na akiba ya maneno
 
Rais wa Wanyonge lakini anafuata nyayo zile zile za walioitwa mafisadi - peleka muswada kwa hati ya dharura ili madhaifu yasijadiriwe kwa kina!!

Yale Makinikia wasipoyaachia haraka, tutakumbwa na dhoruba kama ile ile ya "samaki wa Magufuli". Mbwembwe nyiiingi mwisho tunaishia kuinamisha vichwa chini.
 
Narudia kusema,watu aina ya Tundu Lissu hakupaswa kuzaliwa katika nchi kama hii bali walipaswa kuzaliwa katika nchi za wenzetu ambako bila shaka wangekuwa wameshapata recognition.

Bahati mbaya sana, maoni haya ya kina Lissu yanaishia tu mitandaoni ila ya bwana yule ndio yanatangazwa dunia muzima na bahati mbaya sana sisi binadamu wengi hatutafuti habari za siasa na wanasiasa kama tunavyotafuta habari zinazohusu gossip,sex,soccer,jokes,etc na badala yake tunasubiri kuletewa/kutangaziwa habari hizi na bahati mbaya zaidi kwa hapa kwetu habari zinazotangazwa zaidi na media ni zile za watawala na sio hizi za kina Lissu tunazopaswa kuzitafuta mitandaoni na kwingineko.

Angalieni hata magazeti yetu siku hizi yalivyojaa ushabiki.

Tundu Lissu nakushauri angalia uwezekano wa kuongea na wahariri wa vyombo vya habari ili wakusaidie kufikisha kwa wananchi haya unayosema na kuyaandika mitandaoni maana wengi hayawafikii.
Wewe endelea na Lissu wako hana lolote anadhani ana akili kuliko maprofesa wa Magufuri ? Toeni upuuzi wenu hapa
 
Ila nchi yetu imejaa wapumb*vu kama alivyosema mtukufu mstaafu.

Ripoti itangazwe kwa mbwembwe zoote in live media, ila haiwekwi wazi ni mali ya aliyoisoma. Sasa kama alikuwa hataki kuiweka wazi yale matangazo yalikuwa ya nini?

Hii miswada ya dharura objective yake nini hasa kama haitatui kasoro za mikataba yenye kasoro?
 
Umeambiwa kuna mbadala huo mwaka? No tume huru ya uchaguzi ,no changes.
Naam maneno kuntu hayo! Tume huru ua uchaguzi isiyotakiwa ndio ingefaa kubadili mambo lakini tukiendelea na hizi TUME ZA UCHAFUZI yale maneno "mwafwaa!" yatatuhusu haswa
 
Aiseeeeeeeee....ina maana hizi sheria mpya hazitahusu kampuni za madini ambazo ziko nchini tayariiiiiii?????????????????????????????.?.............???????
So Acacia hawataguswa na sheria hii? Hii ni kweli jamani?????????? *Hivi ni sehemu gani ya nchi yetu yenye madini na hayana mwenyewe tayari*? Mmmmmmmhhh...!!!

Nahitaji kujua.. Eeeeeeeeehhhhhh...!!
Mkuu hiyo ndio habari yenyewe... wezi wataendelea kulindwa na wazee wa ndiyo watapitisha sheria kwa makampuni mapya ambayo hayatakuja!! Labda kwa kina Chacha na Masanja kule Geita na Nyamongo wenye vitalu vidogo vya uchimbaji!
 
Back
Top Bottom