saronga
JF-Expert Member
- Mar 5, 2008
- 909
- 218
Hili Jeshi la Polisi limethibitisha kwa mara nyingine tena linafanya shughuli zake kwa maelekezo ya CCM.
Wameshindwa kuwapata waliomteka Dr Ulimboka tokea alipotekwa mwaka jana, wameshindwa kuwakamata waliomteka Kibanda siku kadhaa zilixopita, eti sasa wanadai wamemkamata Lwakatare kwa tukio la `kufikirika' la kutekwa kwa Msacky, tena amefunguliwa mashtaka ya ugaidi!!
Inashangaza kwa madudu yote haya ya Jeshi la Polisi, inawezekanaje IGP Mwema aendelee na kazi. Kama waTZ tusiposhinikiza IGP Mwema aondoke kwenye nafasi hiyo, tusije kushangaa ifikapo mwaka 2015 waTZ wote tunaoipinga CCM tukawa tumesekwa ndani kwa makosa ya ugaidi, ili CCM ipite bila kupingwa!!!!!
we waache tu, watakuja kuumbuka siku watakapotakiwa kutoa definition ya ugaidi na gaidi, hapo m..a..vi yatagonga bukta zao za ndani. Manake hili wamekurupuka kwa kufuata maagizo bila ya kulitafakari kwa kina. Maji yamekwisha mwagika na hawawezi tena kuyazoa, wasubiri mrejesho wake. Sijui wataficha wapi mijisura yao