Hili la universal health au nhif/chf zinatakiwa zifanyiwe kazi ya kitaaluma kutokana na mfumo wetu kama nchi kuwa na watu wengi kwenye informal sector ambao hawajawa integrated kwenye hizo funds na kuona kiasi cha kuchangia na namna ya kuchangiaLissu akiwa Sumbawanga kadai kuwa wakina mama wajawazito wanatozwa tozo mahospitalini pindi wanapojifungua.
Kuwa mama akijifungua mtoto wakiume anatozwa tozo kubwa kuliko aliejifungua mtoto wa kike. Je, nikweli juu yahaya ndugu zangu CCM, au Lissu anadanganya?
Je, kama nikweli, kwanini tozo zitofautiane juu ya mtoto wakiume na kike? Je, hii ipo kisheria? Au Kuna baadhi ya hospital zinamuhujumu raisi wetu mpendwa JPM?
Kama muheshimiwa raisi anatoa elimu bure, kwa nini asiruhusu wajawazito waachwe kutozwa tozo mara wanapojifungua? Maana anahimiza tufyatue watoto kwa wingi zaidi.
Nataka nifahamu ukweki juu yahili, kama nikweli Serikali imeweka tozo mpaka kwa wajawazito, na kama tozo hizo zinatozwa tofauti kwa mtoto wakike na kiume, kama kuna ukweli wowote.
Bima ya afya kwa kila mwananchi za bei nafuu ndio suluhisho, itaondoa ukilitimba wote wa tozo za hospitalini.