Lissu: Kiburi cha Mbowe kimeniokoa

Lissu: Kiburi cha Mbowe kimeniokoa

UAMUZI wa kumsafirisha haraka Tundu Lissu, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kwenda Nairobi, Kenya kwa matibabu, kuliokoa maisha yake.

Aliyesimama kidete kuhakikisha Lissu anasafirishwa kwenye Nairobi kwa matibabu zaidi ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe.

“Pamoja na jitihada zote za madaktari wa Hospitali ya Dodoma, ambako nilipewa huduma za awali kuokoa maisha yangu, uamuzi wa Mbowe na wengine wachache, hakika ni kipimo kikubwa cha uhai wangu hata leo,” alisema Lissu wakati akihojiwa na mwandishi wetu kitandani kwake, ndani ya Hospitali ya Nairobi, Januari 5, siku moja kabla ya kusafirishwa kwenda Ubelgiji kwa matibabu zaidi.

“Wengi nimewashukuru, hasa madaktari wa Dodoma na Nairobi, lakini kwa namna ya pekee, niweke wazi hili, kwamba kiburi cha chairman (mwenyekiti) Mbowe, kiliokoa uhai wangu na hata sasa naendelea kupumua…

“Nimeelezwa kuwa kulikuwepo mvutano wa hospitali gani nipelekwe baada ya kutibiwa Dodoma, kwamba iwe Dar es Salaam au eneo jingine ndani ya Tanzania, lakini Mbowe alikataa kupelekwa eneo jingine lolote, isipokuwa Nairobi…

“Mbowe naambiwa alisimama imara na kueleza waziwazi kuwa Lissu atatibiwa Nairobi, huku wengine wakianza kususa…

“Hakika isingekuwa kiburi cha kupingana na wengine, wakiwamo baadhi ya vigogo wa serikali, waliopendekeza nipelekwe Dar es Salaam, msingekuwa na Lissu ambaye, angalau sasa anaishi, licha ya kuwepo juu ya kitanda cha hospitali kwa miezi minne leo,” aliongeza.

Taarifa zinaeleza kuwa “kiburi” cha Mbowe kilishinda uamuzi wa awali na mapendekezo ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai na viongozi wengine wa serikali waliotaka Lissu apelekwe Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

Kudhihirisha shukrani kwa Mbowe, katika mahojiano maalum na Mwanahalisionline, siku moja kabla ya kuruhusiwa kutoka Hospitali ya Nairobi, Lissu alimtaja Mbowe mara 16, ndani ya dakika 42 za mahojiano hayo.

“Nakushukuru sana mwenyekiti Mbowe” ndiyo maneno yaliyotamkwa na Lissu mara kwa mara.

Lissu ambaye alisafirishwa usiku kwa ndege ya kukodi kutokea Dodoma Septemba 7, mwaka jana alishambuliwa kwa risasi siku hiyohiyo mchana, akiwa nje ya nyumba anamoishi, Area D – Site 3, wanakoishi mawaziri na viongozi wengine waandamizi wa serikali.

Lissu alishambuliwa akiwa ametoka kwenye kikao cha bunge na alikuwa akielekea nyumbani kwa mapumziko na kupata chakula cha mchana.

Waliomshambulia mbunge huyo wa Singida Mashariki (Chadema) hadi sasa hawajakamatwa. Jeshi la Polisi limeeleza kuwa Lissu alishambuliwa na “watu wasiojulikana.”

Mbowe aliyekuwa Nairobi wiki iliyopita aliiambia Mwanahalisionline kuwa uamuzi wa kumsafirisha Lissu kwenda Nairobi, haukuwa rahisi, ilibidi kung’ang’ania baada ya kushindwa kukubaliana na baadhi ya viongozi waliokuwepo Dodoma.

“Nashukuru sana kwamba sasa afya ya mheshimiwa Lissu inaendelea kuimarika, hii ni faraja kubwa kwetu na hasa wapenda amani na ukomavu wa demokrasia…

“Uamuzi ule ulikuwa na nguvu ya kipekee, kwani ndiyo uliosababisha Lissu kuwa hai hata sasa, vinginevyo siku ile kungekuwa na taarifa zenye huzuni zaidi, tunamshuuru sana Mungu kwa hatua ile na hata muda huu anaendelea kumpigania,” alisema Mbowe.

Mbowe kama ulivyo msimamo wa Lissu na viongozi wengine wa vyama siasa wanavyoamini, shambulio kwa Lissu lilikuwa na dhamira kuu ya kisiasa; “kummaliza Lissu” kwa kuwa amekuwa mkosoaji mkubwa wa utendaji wa Rais John Magufuli.

Pamoja na msimamo huo, serikali imeshindwa kutoa maelezo ya kukanusha au kukubali na kubaki kueleza kuwa “Lissu ni mgonjwa, aachwe apone, serikali haiwezi kujibishana na mgonjwa.”

Msimamo huo wa serikali umekuwa ukitolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dk. Hassan Abbasi.


Chanzo: Mwanahalisi online
Asante sana
 
Tena usiongelee Muhimbili kabisa.Uzembe wa Madaktari umemuondoa binti yangu.
Una uhakika ilikuwa ni uzembe au nature ya ugonjwa aliokuwa nao?

Kumbuka si kila mgonjwa lazima apone.
 
Akachinje jogoo kwani pale Muhumbili nadhani wangelipasua kichwa chake waangalie kama kuliingia risasi au moshiwa risasi. Ana bahati ya mutende kuwa order kutoka juu haikuja kuwa aombe kibali cha safwari.
Kwa Hekima na ujasusi wa Mbowe alikataa kata, Mbowe akili Kubwa anajua Muhimbili kumejaa watu wasiojulikana pale.
 
Ina maana Kiburi cha Mbowe ndio kimeokoa maisha ya Tundu Lisu kweli!?
Mimi nilijua ni Neema na uponyaji kutoka kwa Mungu na Madaktari waliokuwa wanahangaika nae usiku na mchana bila kusahau maombi ya Watanzania duniani kote. Kama ni "Kiburi cha Chairman" ndio kilimponya basi inabidi Mh. Mbowe atangazwe kuwa mtakatifu.
 
Kwa Hekima na ujasusi wa Mbowe alikataa kata, Mbowe akili Kubwa anajua Muhimbili kumejaa watu wasiojulikana pale.
Mbona yeye alishawahi kulazwa na kupatiwa matibabu pale Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI) !?
Au hayo majasusi unayozungumzia yalikuwa likizo kipindi hicho mkuu?
 
Atakuwa kajifunza kuwa duniani anatakiwa kuwa na huruma na MTU au Serikali ikiwa inadhulumiwa na kuonewa na wawekezaji wawe wa madini au watu washika bombardier hutakuwi kusimama na mtesi wa serikali ambaye utesi wake utaumiza walipa kodi wengi maskini ili walipe madini au bombardier au kodi zilizokwepwa.Ukiwa mbunge uwe wa upinzani au CCM always simamia maslahi ya nchi usiwe kibaraka wa waoneao nchi.Vita ikilipuka watu wa Kwanza kuuawa huwa ni vibaraka wa watu wa nje .Hilo alijue yeye na vibaraka wenzie .Vita ya kiuchumi ni kubwa kuliko uchumia tumbo wa Lisu na familia yake usiozingatia maslahi ya nchi
Mkuu hadithi za kitoto hizo unazoandika hapa. 1.Hao wawekezaji wanaoidhulumu serikali aliwatafuta Lisu?, 2. Hiyo mikataba ya kifisadi aliiandaa na kuisaini Lisu?, 3. Hao walioshikilia bombardier aliwatafuta Lisu?, 4. Hizo kesi za barabara zilizisababisha bombardier kukamatwa Lisu anahusika nazo?, 5. hizo sheria mbovu za madini zinazotuletea Shida na mfarakano hapa nchini ziliandaliwa na Lisu?. Yote haya yameletwa na wenzetu wa kijani ambao muda wote wao wanataka waitwe watakatifu wasiopenda kukosolewa. 2020 siyo mbali....
 
Wala sio siri waliotaka kumuua wangetumia nafasi hiyo kummalizia kama angepewa hifadhi muhimbili.
 
Wana Chadema vipi nyie, mara kaokolewa NA mungu, NA sasa naona ni Mbowe.

Kama kweli mnaa imani, NA siku sake hazija fika basi angepona, hata angepelekwa hospitali ya kijijini kwao
 
Mbona yeye alishawahi kulazwa na kupatiwa matibabu pale Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI) !?
Au hayo majasusi unayozungumzia yalikuwa likizo kipindi hicho mkuu?
Ndio kazi ya kijasusi kufanya situational analysis mkuu.....hata leo au kesho anaweza kulazwa kutegemea na hali ya hewa ya kiusalama. We vipi bwana.
 
0b7c7e93-a5a9-4c3c-9400-bf4e8a8c49e1.jpg


Hata huyu japo kuwa alipigwa NA bazooka, hiyo iliyolewa NA anaishi vizuri. Kama siku hakufika hata upigwe bomu utaishi tuu. Mpango wa mungu hauumbuliwi NA Binadamu
 
Back
Top Bottom