Lissu kapata vyote;CCM yakosa kimoja

Lissu kapata vyote;CCM yakosa kimoja

ccm wanataman kumumwagia mzee Antipas tindikali.mzee KINANA SHAME ON U.
 
Namsikitikia sana mamaangu mzazi , maana hadi anafariki alikuwa mwanachama wa ccm .
 
Katika kesi ya rufani ya kupinga ushindi wake alioupata Mahakama Kuu Dodoma,Wakili Msomi na Mbunge wa Singida Mashariki,Tundu Antipas Mughway Lissu ameibuka kidedea.

Kesi husika ilikuwa katika Mahakama ya Rufani iliyoketi Dodoma. Mahakama ya Rufani iliongozwa na Majaji watatu: Engela Kileo,Nathalia Kimaro na Salum Massati.

Siku nyingi kabla ya kesi hii kupangiwa tarehe ya kusikilizwa,yaani leo,Warufani wawili walijitoa rasmi katika kesi husika kwa kutumia Viapo. Wakili Msomi aliyekuwa akiwaongoza,Wakili Msomi Wasonga,alijua. Akakaa kimya. Ilimpasa atoe taarifa rasmi ya kisheria Mahakamani ili kesi husika isipangiwe hata tarehe ya kusikilizwa seuse kuwekewa pingamizi la awali.

Mahakama ya Rufani imesema leo kuwa kesi haiweza kuondolewa ikiwa tayari kuna mapingamizi ya awali yaliyosubiri kutolewa uamuzi. Ifahamike kuwa,kwakuwa tangu mwanzo wa kesi hii Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa upande wa Lissu(kama Mlalamikiwa wa pili),leo ameendelea kuwa hivyo. Katika kulinda weledi wake,Mwanasheria wa Serikali leo alikubaliana na kila hoja ya Lissu aliyoitoa Mahakamani hapo.

Jambo lingine la kuelewa ni kuwa Wakili Msomi Lissu alijiwakilisha mwenyewe katika kesi hii wakati ikiwa Mahakama Kuu kanda ya Dodoma. Akashinda. Leo,pamoja na kuwa Wakili Msomi Lissu alitegemea kuwepo kwa Wakili Msomi Method Kimomogoro,alijiwakilisha mwenyewe tena. Ifahamike kuwa Wakili Msomi Lissu leo hakuwa Wakili.Alijiwakilisha kama Mjibu Rufani. Ndiyo maana,hakuvaa kama Mawakili wengine waliokuwepo hapo.

Wakili Msomi Wasonga leo ameadhibiwa na kutojali kwake.Kutotoa taarifa.Kujaribu kuichezea Mahakama.Alisahau kuwa hii ilikuwa ni Mahakama ya Rufani ya Tanzania;mahakama ya juu na ya mwisho hapa nchini.Mahakama imelinda hadhi yake. Imekataa kuchezewa.

Wakili Msomi Wasonga tangu mwanzo wa kesi leo alisisitiza kutaka kuiondoa kesi kwakuwa Warufani wamejiondoa na hivyo hana wa kumwakilisha. Lissu na Mwanasheria wa Serikali wakakataa.Wakasema kuwa kesi,kutokana na kuwepo na mapingamizi pamoja na kujitoa kwa Warufani halafu taarifa isifikishwe Mahakamani,haiwezi kuondolewa. Hivyo,wakaomba itupiliwe mbali na gharama za kesi zilipwe kwa Lissu. Wamefanikiwa.

Wakili Msomi Wasonga sasa yu njia panda. Nani ampelekee uamuzi huu? Lakini mwenyewe anamjua.Akishindwa kumjua hata kwa kumburuta MAHAKAMANI,basi itampasa awajibike mwenyewe.Kazi ni kwake!

Wakili Msomi Lissu amepata vyote.Amelinda Ubunge wake,heshima yake,weledi wake,fidia na heshima ya MAHAKAMA. CCM wao (kwakuwa Warufani ni wa-CCM) wamekosa kitu kimoja tu walichokuwa wakikihitaji kwa udi na uvumba. Kitu ambacho wangekipata,leo hapa Lumumba kungekuwa na sherehe.Kesho tungefanya maandamano ya kuiunga mkono Mahakama ya Rufani. CCM wameukosa Ubunge wa Lissu.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

mkuu VUTA-NKUVUTE
...naomba uutendee haki uzi huu kwa ku-edit hapo kwenye
"Wakili Msomi Wasonga" kwa kuondoa "Msomi" badala yake iwe "Mnywa-Maji",na sasa isomeke "Wakili Mnywa-Maji Wasonga"...
 
Last edited by a moderator:
Ccm imekufa, CHADEMA YATOSHA. Hongera lissu,hongera CDM POPOTE MLIPO.
 
aibu sana tulisha sema hapa kuwa kuna wa kuwachezea ila siyo Lissu.

Sasa hizo gharama watamtafuta aliyewatuma asaidie kulipa. Sidhani kama Makamba anahusika au ni kiti kiti alicho kuwa anakalia

buku 7 project watakosa mgao wao hii itafanya wapote jamvini.

Hela ya kulipa wanazo. Watakwapua pale BOT kama kawaida yao....
 
Chama Cha Manyang'au?:shetani::shetani:
 
Hongerra sana kamanda lissu kwa kushinda, honger sana wanaharakati wote ila pia Hongera kwa wafungua mashitaka kwa kutekeleza haki yao ya msingi ya kufungua kesi pale walipo hisi haki yao ya msingi imekiukwa!
 
huyu jamaa nilishapata bahati ya kukaa naye pale tegeta zero pub kwakwel jamaa ni jembe yani mtu asikuambie sheria anaijua sana yani huyu jamaa napenda sana aje kuwa mwanasheria mkuu wa serikali alafu wazungu wawe wanakuja kuingia mikataba...ila niseme kuwa Mungu ampe uzima atufikishie taifa mahali pazuri kwenye maswala ya mikataba
 
wako kwenye kikao cha dharulla, kuhusu donation watalipaje bila kuwatoa mbwa AIRPORT wapitishe unga, baada ya siku si nyngi tutasika pembe za ndovu tena,huku kote ni pesa ya kulipa gharama za kesi
 
Katika kesi ya rufani ya kupinga ushindi wake alioupata Mahakama Kuu Dodoma,Wakili Msomi na Mbunge wa Singida Mashariki,Tundu Antipas Mughway Lissu ameibuka kidedea.

Kesi husika ilikuwa katika Mahakama ya Rufani iliyoketi Dodoma. Mahakama ya Rufani iliongozwa na Majaji watatu: Engela Kileo,Nathalia Kimaro na Salum Massati.

Siku nyingi kabla ya kesi hii kupangiwa tarehe ya kusikilizwa,yaani leo,Warufani wawili walijitoa rasmi katika kesi husika kwa kutumia Viapo. Wakili Msomi aliyekuwa akiwaongoza,Wakili Msomi Wasonga,alijua. Akakaa kimya. Ilimpasa atoe taarifa rasmi ya kisheria Mahakamani ili kesi husika isipangiwe hata tarehe ya kusikilizwa seuse kuwekewa pingamizi la awali.

Mahakama ya Rufani imesema leo kuwa kesi haiweza kuondolewa ikiwa tayari kuna mapingamizi ya awali yaliyosubiri kutolewa uamuzi. Ifahamike kuwa,kwakuwa tangu mwanzo wa kesi hii Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa upande wa Lissu(kama Mlalamikiwa wa pili),leo ameendelea kuwa hivyo. Katika kulinda weledi wake,Mwanasheria wa Serikali leo alikubaliana na kila hoja ya Lissu aliyoitoa Mahakamani hapo.

Jambo lingine la kuelewa ni kuwa Wakili Msomi Lissu alijiwakilisha mwenyewe katika kesi hii wakati ikiwa Mahakama Kuu kanda ya Dodoma. Akashinda. Leo,pamoja na kuwa Wakili Msomi Lissu alitegemea kuwepo kwa Wakili Msomi Method Kimomogoro,alijiwakilisha mwenyewe tena. Ifahamike kuwa Wakili Msomi Lissu leo hakuwa Wakili.Alijiwakilisha kama Mjibu Rufani. Ndiyo maana,hakuvaa kama Mawakili wengine waliokuwepo hapo.

Wakili Msomi Wasonga leo ameadhibiwa na kutojali kwake.Kutotoa taarifa.Kujaribu kuichezea Mahakama.Alisahau kuwa hii ilikuwa ni Mahakama ya Rufani ya Tanzania;mahakama ya juu na ya mwisho hapa nchini.Mahakama imelinda hadhi yake. Imekataa kuchezewa.

Wakili Msomi Wasonga tangu mwanzo wa kesi leo alisisitiza kutaka kuiondoa kesi kwakuwa Warufani wamejiondoa na hivyo hana wa kumwakilisha. Lissu na Mwanasheria wa Serikali wakakataa.Wakasema kuwa kesi,kutokana na kuwepo na mapingamizi pamoja na kujitoa kwa Warufani halafu taarifa isifikishwe Mahakamani,haiwezi kuondolewa. Hivyo,wakaomba itupiliwe mbali na gharama za kesi zilipwe kwa Lissu. Wamefanikiwa.

Wakili Msomi Wasonga sasa yu njia panda. Nani ampelekee uamuzi huu? Lakini mwenyewe anamjua.Akishindwa kumjua hata kwa kumburuta MAHAKAMANI,basi itampasa awajibike mwenyewe.Kazi ni kwake!

Wakili Msomi Lissu amepata vyote.Amelinda Ubunge wake,heshima yake,weledi wake,fidia na heshima ya MAHAKAMA. CCM wao (kwakuwa Warufani ni wa-CCM) wamekosa kitu kimoja tu walichokuwa wakikihitaji kwa udi na uvumba. Kitu ambacho wangekipata,leo hapa Lumumba kungekuwa na sherehe.Kesho tungefanya maandamano ya kuiunga mkono Mahakama ya Rufani. CCM wameukosa Ubunge wa Lissu.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

>Ccm wanatumia hela za wananchi bila sababu ya msingi... Wamejawa na upuuzi...
 
mkuu VUTA-NKUVUTE
...naomba uutendee haki uzi huu kwa ku-edit hapo kwenye
"Wakili Msomi Wasonga" kwa kuondoa "Msomi" badala yake iwe "Mnywa-Maji",na sasa isomeke "Wakili Mnywa-Maji Wasonga"...
Usijali Mkuu Sabung'ori, hata kama amekosea na kushindwa kesi,bado anabakia kuwa Wakili Msomi Wasonga
 
Last edited by a moderator:
Kete pekee waliyoitegemea chama cha majangili(ccm),chama cha mateja(ccm),chama cha mafisadi(ccm) ni kubambikia kesi wapinzani na kufungua kesi za kupinga ubunge wa mashine za CHADEMA,sasa wafanyeje hawa wana chama cha magamba(ccm)?
 
Back
Top Bottom