Lissu kapata vyote;CCM yakosa kimoja

Lissu kapata vyote;CCM yakosa kimoja

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Katika kesi ya rufani ya kupinga ushindi wake alioupata Mahakama Kuu Dodoma,Wakili Msomi na Mbunge wa Singida Mashariki,Tundu Antipas Mughway Lissu ameibuka kidedea.

Kesi husika ilikuwa katika Mahakama ya Rufani iliyoketi Dodoma. Mahakama ya Rufani iliongozwa na Majaji watatu: Engela Kileo,Nathalia Kimaro na Salum Massati.

Siku nyingi kabla ya kesi hii kupangiwa tarehe ya kusikilizwa,yaani leo,Warufani wawili walijitoa rasmi katika kesi husika kwa kutumia Viapo. Wakili Msomi aliyekuwa akiwaongoza,Wakili Msomi Wasonga,alijua. Akakaa kimya. Ilimpasa atoe taarifa rasmi ya kisheria Mahakamani ili kesi husika isipangiwe hata tarehe ya kusikilizwa seuse kuwekewa pingamizi la awali.

Mahakama ya Rufani imesema leo kuwa kesi haiweza kuondolewa ikiwa tayari kuna mapingamizi ya awali yaliyosubiri kutolewa uamuzi. Ifahamike kuwa,kwakuwa tangu mwanzo wa kesi hii Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa upande wa Lissu(kama Mlalamikiwa wa pili),leo ameendelea kuwa hivyo. Katika kulinda weledi wake,Mwanasheria wa Serikali leo alikubaliana na kila hoja ya Lissu aliyoitoa Mahakamani hapo.

Jambo lingine la kuelewa ni kuwa Wakili Msomi Lissu alijiwakilisha mwenyewe katika kesi hii wakati ikiwa Mahakama Kuu kanda ya Dodoma. Akashinda. Leo,pamoja na kuwa Wakili Msomi Lissu alitegemea kuwepo kwa Wakili Msomi Method Kimomogoro,alijiwakilisha mwenyewe tena. Ifahamike kuwa Wakili Msomi Lissu leo hakuwa Wakili.Alijiwakilisha kama Mjibu Rufani. Ndiyo maana,hakuvaa kama Mawakili wengine waliokuwepo hapo.

Wakili Msomi Wasonga leo ameadhibiwa na kutojali kwake.Kutotoa taarifa.Kujaribu kuichezea Mahakama.Alisahau kuwa hii ilikuwa ni Mahakama ya Rufani ya Tanzania;mahakama ya juu na ya mwisho hapa nchini.Mahakama imelinda hadhi yake. Imekataa kuchezewa.

Wakili Msomi Wasonga tangu mwanzo wa kesi leo alisisitiza kutaka kuiondoa kesi kwakuwa Warufani wamejiondoa na hivyo hana wa kumwakilisha. Lissu na Mwanasheria wa Serikali wakakataa.Wakasema kuwa kesi,kutokana na kuwepo na mapingamizi pamoja na kujitoa kwa Warufani halafu taarifa isifikishwe Mahakamani,haiwezi kuondolewa. Hivyo,wakaomba itupiliwe mbali na gharama za kesi zilipwe kwa Lissu. Wamefanikiwa.

Wakili Msomi Wasonga sasa yu njia panda. Nani ampelekee uamuzi huu? Lakini mwenyewe anamjua.Akishindwa kumjua hata kwa kumburuta MAHAKAMANI,basi itampasa awajibike mwenyewe.Kazi ni kwake!

Wakili Msomi Lissu amepata vyote.Amelinda Ubunge wake,heshima yake,weledi wake,fidia na heshima ya MAHAKAMA. CCM wao (kwakuwa Warufani ni wa-CCM) wamekosa kitu kimoja tu walichokuwa wakikihitaji kwa udi na uvumba. Kitu ambacho wangekipata,leo hapa Lumumba kungekuwa na sherehe.Kesho tungefanya maandamano ya kuiunga mkono Mahakama ya Rufani. CCM wameukosa Ubunge wa Lissu.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Pole sana mzee tupatupa unaonyesha unakerwa na umbumbumbu wa wenzio hivi kwanini hawawapi nyie hata mda kidogo wa kuwashauri? jitahidini kuwashauri wambieni ulimwengu wa sasa sio ule wa miaka ya 47 najua wanavichwa vigumu ila juhudi zenu zitasaidia
 
ccm mzima sijaona mtu ambaye anaweza kum challenge Lissu kisheria ,wanachokifanya magamba chini ya ushauri wa mlevi wa madaraka Nchemba na Jungle master Kinana ni upotevu wa muda,fedha za walipa ushuru bila kusahau kuipa promo chadema ...!Mwigulu Nchemba oyee....... asante sana kwa kuipa promo CDM baada ya 4-0 promo nyingine hiyooooooo
 
aibu sana tulisha sema hapa kuwa kuna wa kuwachezea ila siyo Lissu.

Sasa hizo gharama watamtafuta aliyewatuma asaidie kulipa. Sidhani kama Makamba anahusika au ni kiti kiti alicho kuwa anakalia

buku 7 project watakosa mgao wao hii itafanya wapote jamvini.
 
hongera sana kamanda umethihirisha uweledi wako na kulinda heshima ya chama ...mapambano yanaendelea big up!!!
 
Wakili Msomi Wasonga sasa yu njia panda. Nani ampelekee uamuzi huu? Lakini mwenyewe anamjua.Akishindwa kumjua hata kwa kumburuta MAHAKAMANI,basi itampasa awajibike mwenyewe.Kazi ni kwake!
Waliomtuma wapo, awapelekee....mzee wa tembo au mropokaji Nape Nnauye.Ikishindikana hata savimbi si linamhusu pia?
 
Last edited by a moderator:
Yu wapi Absalom Kibanda; mwanahabari mwandamizi, mwandishi mweledi na mchambuzi yakinifu, yu wapi mwana wa Kibanda Aje hapa jamvini atupe maelezo ya kutosha kuhusu Kesi hii ya Abdrahaman Kinana; katibu mkuu wa CCM mweledi ambaye Absalom Kibanda muda mfupi kabla hajadhuriwa na wahuni alijaribu sana kutushawishi kwamba AB Kinana ni mtu matata sana ambaye angeweza kuvivuruga vyama vya siasa hususani CDM.
Je hizi kesi za kulazimisha ndio kielelezo cha ukabambe na weledi wa Ab. Kinana? je kwa mwendo huu Kinana atauweza muziki wa CDM, CUF na NCCR ambao kwa udhaifu wa kufikiri CCM wamezindua ari mpya ya kuimaliza CCM.

Uko wapi Absalom Kibanda??!! you went off the blocks too early before the gun!!
 
Kwan si alikuwepo mahakaman huyo wakili? Tena alikuwa akijitetea kesi ifutwe,alibaki mwenyew tu,si mwigulu,si kinana,si nepi aliemsaidia wala pinda,alibaki mwewnyewe...
 
Lumumba team mbona hawagusi hapa? Wanachungulia kwa mbali tu. Pa-moto kwao nini? Kamanda Lissu anawakimbiza ile mbaya na bado.
 
hahaaa hivi hawa CCM wana mwenyekiti kweli hawa ...mbona kama ni chama cha mateja tu
 
Sawa Kaka Vuta Nikuvute, ni vizuri tujitahidi kujenga siasa za kidemokrasia, hivi ni kwa nini Tume ya Uchaguzi isiwe inaandaa uchaguzi Huru na Haki ili tusipotezee watu muda wao wa kukata rufaa na ku-appear mahakamani?
 
Hongera mheshimiwa lisu,hongereni makamanda wote wa cdm taifa,mkoa,wilaya,kata,tarafa ,vitongoji na vijiji.
 
kinana hamjui vizuri TL,Angemuuliza JK habari za huyu jamaa.
werema mwenyewe huwa anaufyata
 
Lumumba team mbona hawagusi hapa? Wanachungulia kwa mbali tu. Pa-moto kwao nini? Kamanda Lissu anawakimbiza ile mbaya na bado.
Taarifa:Lumumba Project itasitishwa kwa muda ili kulipia gharama za kesi-by mzzee wa calorite
 
kwan si alikuwepo mahakaman huyo wakili? Tena alikuwa akijitetea kesi ifutwe,alibaki mwenyew tu,si mwigulu,si kinana,si nepi aliemsaidia wala pinda,alibaki mwewnyewe...

chadema yatosha nyinyiemu majangaaaa
 
Back
Top Bottom