GE2025 Lissu chini ya ulinzi mkali afikishwa Mahakamani

GE2025 Lissu chini ya ulinzi mkali afikishwa Mahakamani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Siku ya nne mfululizo, Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam inaendelea kusikiliza mapingamizi ya kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu, mapingamizi yaliyowekwa na mshtakiwa mwenyewe

Leo, Alhamisi Septemba 11.2025 Mahakama inaendelea kusikiliza hoja za mshtakiwa kwenye mapingamizi hayo, leo akitarajiwa kujibu hoja zilizoibuliwa na upande wa Jamhuri unaopinga mapingamizi hayo

Kutoka Mahakamani hapo, tunakusogezea kuona namna Tundu Lissu alivyofikishwa mapema leo akiwa chini ya ulinzi mkali.

Chanzo: Jambo Tv
 
Huo ulinzi ni vitisho kwa wananchi na chadema au wanalinda nini hapo?

Lisu aliisha kuwa mlemavu kukimbia hawezi, watu hawaruhusiwi hata kusogelea eneo la mahakama zaidi ya walio ruhusiwa ndani.

Sasa analindwa au wanamtisha au ni utaratibu kisheria kwa watuhumiwa wa uhaini kulindwa hivyo?
 
Rais wangu bora kabisa huyu kuwahi kutokea nchini.
Lissu na watanzania watalipa gharama kubwa sana kwa upumbavu wa kudharau viongozi wazalendo kipindi cha JPM ....tukitumia akili mtajua kuwa Lissu ana uwezo mdogo sana wa kuona mbele, tujiulize je Nyerere angekuwa hai angempinga JPM ? ...Tumtizame mtu kama Mtikila alivyo kuwa anaichukia CCM ila alimuunga mkono JPM kabla hata ajawa Rais ...hii inamaana kuwa Mtikila alikuwa na AKILI NZURI YA KUTAMBUA KIONGOZI NA UZALENDO
 
Huo ulinzi ni vitisho kwa wananchi na chadema au wanalinda nini hapo?

Lisu aliisha kuwa mlemavu kukimbia hawezi, watu hawaruhusiwi hata kusogelea eneo la mahakama zaidi ya walio ruhusiwa ndani.

Sasa analindwa au wanamtisha au ni utaratibu kisheria kwa watuhumiwa wa uhaini kulindwa hivyo?
Ulinzi wa mtuhumiwa siyo kwaajili ya yeye kutoroka tu analindwa ili asidhuriwe pia, akipata madhara hapo utakuja tena kuuliza kwanini hakuwekewa ulinzi
 
Lissu na watanzania watalipa gharama kubwa sana kwa upumbavu wa kudharau viongozi wazalendo kipindi cha JPM ....tukitumia akili mtajua kuwa Lissu ana uwezo mdogo sana wa kuona mbele, tujiulize je Nyerere angekuwa hai angempinga JPM ? ...Tumtizame mtu kama Mtikila alivyo kuwa anaichukia CCM ila alimuunga mkono JPM kabla hata ajawa Rais ...hii inamaana kuwa Mtikila alikuwa na AKILI NZURI YA KUTAMBUA KIONGOZI NA UZALENDO
Kipindi cha utawala wa mzalendo wako magufuli ndo kipindi lisu alipigwa risasi, ndg ungekua wewe ungempenda mtu kama huyo?
 
Kipindi cha utawala wa mzalendo wako magufuli ndo kipindi lisu alipigwa risasi, ndg ungekua wewe ungempenda mtu kama huyo?
Hilo swali ...jibu tayari Lissu analo na anajutia upumbavu wake wa kuwaletea wanamtandao hadi kupigwa risasi ...lisu ana uchungu sana na walio mtumia hadi akapigwa risasi na hao hao leo ndiyo wamemtua jela .. samia alitoka mbio kumtizama kibaraka wao kule Nairobi baada ya kuchapwa shaba leo Samia ndiyo kamtupa jela tofauti hata na JPM maana wakati wa JPM LISSU ALIFANYA KAMPENI NCHI NZIMA BILA YA BUGUDHA
 
Yani kuzungukwa kote huko wanaogopa atakimbia au watu wasio Julikqna wata mpiga risasi
 
anajutia upumbavu wake wa kuwaletea wanamtandao hadi kupigwa risasi ..
Kawatetea lini na wapi? Mbona unaongea upumbavu. Lissu hajawahi kutumika, yeye alimpinga JPM sababu ya udikteta wake wala sio kingine.

Hata kipindi mbowe anaanza maridhiano alipinga, sasa mtu wa mtandao anaweza kataa maridhiano na Samia?
 
Lissu ni mtu na nusu, anapewa pressure kubwa lakini bado yuko imara kabisa...hapo anaenda kutoa darasa la sheria kwa mawakili vilaza wa serikali!.
Hii kesi serikali
itanyoosha mikono tu! Lakini kubwa nililojifunza ni kuwa wachangiaji wengi wanayo elimu ndogo sana kuhusu uendeshaji wa mashauri na utetezi mahakamani. Ujinga! Hata kisichohusu sheria watu wanashangilia "ETI MWALIMU WA SHERIA" wakati ni mabishano ya kawaida kuhusu kilichotokea tu! Hata huku machawa ni wengi sana siyo kijani peke yake! Tunayo safari ndefu UJINGA bado ni mwingi Tanganyika. Maskini Tangamyila!
 
Back
Top Bottom