Lissu anapotosha watu

Lissu anapotosha watu

JIBU HIZI HOJA ZA LISU

1. Rais sio mzanzibar?

2. Bandari hazijauzwa?

3. Wamasai hawajahamishwa?

4. Mtanganyika anaweza kumiliki ardh zanzibar?

5. Mtanganyika anaweza kupata nafasi ya uongozi zanzibar?

6. Mtanganyika anaweza kupiga kura zanzibar?
Hizi ni hoja za kipuuzi zinazoungwa mkono na Wajinga.
 
..Watz hawawezi kufanya hiyo biashara ya blue carbon mpaka tuletewe Waarabu?

..Yaani hata kilimo Watz tumeshindwa tunawaleta Waarabu?
Kuna Halmashauri 3 tu Tanzania ndiyo zinajishughulisha. Ofisi inayo coordinate miradi ya Carbon iko SUA, Morogoro.

Hakuna Mtanzania anayekatazwa, tatizo Watanzania wanataka biashara zinazokupa faida hapo kwa hapo ndiyo maana hawaioni.
 
Hii topic ni distraction. Mimi nilitaka kuandika kuhusu jambo lingine.
Lakini 1964,kama TFL ilivunjwa ni kwa sababu iliunga mkono maasi ya Colito Barracks.
Lakini ni kweli anavyosema Tundu Lissu. Samia Suluhu BADO hajachaguliwa na Watanzania kuwa rais. Isipokuwa,Inshallah,anatumaini kuchaguliwa 2025.
Na kwa vile "Rais" Samia hajachaguliwa na watu,anavyouza ardhi ya Watanganyika ni kufuru.
Rais Samia ni kama Lyndon Johnson alivyokula kiapo ndani ya helicopter.
Lyndon Johnson alisubiri baadaye,alipochaguliwa,ndipo akaanza kufanya mambo yake.
Siku ile ile aliyoapishwa akaanza kuihamisha dhahabu ya Fort Knox. Malori ya US Army yakaanza kuiondoa ile dhahabu yakiongozwa na Linda Bird. (Huyu ndiye mke wake Johnson).
Halafu ipo hii Kampuni ya Blue Carbon ya Dubai( ruling family). Inanunua ardhi nyingi sana Afrika,katika nchi tano: Zimbabwe( ambako wamenunua ten percent of the country's land,na Tanzania na Cameroon,and two other countries. Hii Blue Carbon inapigiwa kelele na African Diaspora. Wanauliza kwa nini ndugu zetu wanaiuza Afrika?
Kama Joe Biden,kwa mfano,akigombea urais na kumchagua Kamala Harris kuwa mgombea mwenza,hapo Wamarekani wakimpigia kura Joe Biden itakuwa wanaiona probability( uwezekano mkubwa) wa Kamala Harris kuwa rais.
Sasa wewe ndiye umepotoshwa na wenzako halafu ukaenda kichwakichwa kutaka upingane na Lissu.
Wewe umetoshwa kiai kwamba ingependeza kama ungeitwa MPOTO kwa jindi ulivyo POTOKA.
 
JIBU HIZI HOJA ZA LISU

1. Rais sio mzanzibar?

2. Bandari hazijauzwa?

3. Wamasai hawajahamishwa?

4. Mtanganyika anaweza kumiliki ardh zanzibar?

5. Mtanganyika anaweza kupata nafasi ya uongozi zanzibar?

6. Mtanganyika anaweza kupiga kura zanzibar?
Hizi hoja wanaccm hasa ambao sio machawa wanatakiwa kuzijibu kwa utulivu na bahati Mbaya azijibiki maana ni kweli sasa wakae kwa kutulia ,hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza beza hoja hizi ni kweli na kama sio kweli wajitokeze kueleza umma ukweli ni upi basi,

Matokeo yake wanajificha kwenye hoja nyepesi tu , na kutuma watu wepesi kujibu hoja ngum

Nimtake Pro kabudi ajitokeze kujibu hoja hizi, ila wenda hanajua ukweli kwa iyo ni ngum kujitokeza
 
Blue Carbon hawanunui hawanunui ardhi ya Africa, instead Blue Carbon wanafanya trading kwenye Carbon credit business ndani ya Africa.

Wanakuja wanapanda misitu na kui-maintain ili kufidia Carbon emissions inayofanywa na UAE. Wafaidika ni sisi Watanzania kwa kufanyiwa maboresho ya kupandiwa miti hivyo kuboresha mazingira.

Mbona biashara ya Carbon credit iko wazi tu. Kuna Halmashauri tatu nchini zimekuwa zikipata Mabilioni ya Tsh kutokana mfuko wa Carbon duniani ikiwapo wilaya ya Tanganyika huko mkoa wa Katavi
Hiyo carbon credit ni njia ya mabeberu kukwepa kuchukua hatua ya kupunguza gesi chafu za viwanda vyao, badala yake wametutwisha sisi huo mzigo....
 
Hiyo carbon credit ni njia ya mabeberu kukwepa kuchukua hatua ya kupunguza gesi chafu za viwanda vyao, badala yake wametutwisha sisi huo mzigo....
Ni kweli lakini angalao wamejali baada ya kugundua hawawezi kufunga viwanda kuepusha hiyo carbon emissions. Kila nchi yenye viwanda imepangiwa kiwango cha carbon cha kupunguza, sasa kama huyo beberu anaweza kutengeneza oxygen kwa kupanda miti Tanzania ambayo itafidia kiwango cha carbon anachopaswa kukikata, ubaya uko wapi.
 
Tatizo wanakwepa kuwajibika kwa athari mbaya za mabadiliko ya tabia nchi......waathirika wakubwa wa uchafuzi wao ni sisi nchi zinazoendelea.

Uwajibikaji unaotakiwa ni wao kupunguza kiwango cha uchafuzi wa gesi chafu na kuchangia mfuko wa kufadhili na kukabiliana na athari za huo uchafuzi bila kukwepa.

Kutuanzishia Carbon credit huku uchafuzi ukiendelea ni uhuni tu
 
Huyu uandishi wake ndivyo ulivyo. Hoja zake huwa hazina logical sequence/coherence/conclusion. Hoja zake huwa zina hang. Kwa hiyo hapo inabidi ujiongeze ili kumwelewa. Kuna baadhi humu wanamwita "genius".
Ana Ubongo wa thamani sana.
 
Tatizo wanakwepa kuwajibika kwa athari mbaya za mabadiliko ya tabia nchi......waathirika wakubwa wa uchafuzi wao ni sisi nchi zinazoendelea.

Uwajibikaji unaotakiwa ni wao kupunguza kiwango cha uchafuzi wa gesi chafu na kuchangia mfuko wa kufadhili na kukabiliana na athari za huo uchafuzi bila kukwepa.

Kutuanzishia Carbon credit huku uchafuzi ukiendelea ni uhuni tu
Je wewe nchi changa unaweza kuwawajibisha mataifa makubwa kwa uchafuzi wa mazingira?
 
JIBU HIZI HOJA ZA LISU

1. Rais sio mzanzibar?

2. Bandari hazijauzwa?

3. Wamasai hawajahamishwa?

4. Mtanganyika anaweza kumiliki ardh zanzibar?

5. Mtanganyika anaweza kupata nafasi ya uongozi zanzibar?

6. Mtanganyika anaweza kupiga kura zanzibar?
Mtanganyika anaingia kwenye bunge la Zanzibar?
 
UAE. Wafaidika ni sisi Watanzania kwa kufanyiwa maboresho ya kupandiwa miti hivyo kuboresha mazingira.
Inasikitisha na kuudhi kwa pamoja.
Yaani hili nalo unasubiri kuwaleta UAE wakupandie miti nchini kwako?
Hizi akili mbovu zimetoka wapi sijui.
Mnatumia kila aina ya ulaghai kuvuruga mawazo ya watu huku mkiiuza nchi rejareja.

Eti tufaidike kwa kuja kupandiwa misitu! Sisi hapa hatujawahi kupanda misitu?
 
Je wewe nchi changa unaweza kuwawajibisha mataifa makubwa kwa uchafuzi wa mazingira?
Ingekuwa mantiki ni hiyo, ukoloni na biashara za utumwa zingekuwa zinashamiri hadi leo hii.
 
Bandari haijauzwa, ni propaganda ya wafuatao:1: Wenye kampuni za miaka zaid ya 30 za clearing and forwarding agent:2:Karamagi na kampuni yake ya TX kwa, ajili ya kuondolewa pale:4:Waliokuwa, wananufaika na mfumo mbovu wa, bandarini.

Hawa ndio wanapiga kelele kuwa bandari imeuzwa.

Lakin, bandari imeletwa kampuni ya ki technology na kimataifa kuliko TX. Itakayonufaisha nchi na wananchi.
Mimi si mmoja wa hao, lakini nalalamika kwa nchi kama Tanzania kutoweza kuendesha bandari kwa ufanisi, miaka 60 baada ya uhuru.
Kwa hiyo, wewe unatumia tu mwanya wa kuwataja matapeli hao ku'justify' jambo bovu kabisa linalofanywa na serikali.

Sisi kama nchi tutakuwa na uwezo lini wa kuendesha bandari?
Ngoja nikuongezee na hili kukufurahisha: mbona tunayo serikali yenye uwezo, angalau hata wa kutafuta hayo makampuni kuja kufanya kazi hapa? Hii serikali na wao tuwaondoe tutafute wenye uwezo zaidi yao toka nje?
 
Inasikitisha na kuudhi kwa pamoja.
Yaani hili nalo unasubiri kuwaleta UAE wakupandie miti nchini kwako?
Hizi akili mbovu zimetoka wapi sijui.
Mnatumia kila aina ya ulaghai kuvuruga mawazo ya watu huku mkiiuza nchi rejareja.

Eti tufaidike kwa kuja kupandiwa misitu! Sisi hapa hatujawahi kupanda misitu?
Je wewe bunafsi una miti mingapi umepanda na iko wapi?

Watanzania ndiyo tulivyo. Hatuna uthubutu na ubunifu ila tunapenda kulalamika.

Mitaa yetu ni michafu na kuna makampuni ya wazabuni wa kuzoa uchafu lakini hawafanyi kazi yao. Leo akija kampuni toka DUBAI akasema atakusanya taka na tumlipe bado TUTALALAMIKA
 
Uoga uoga wa kijinga unasababisha vijana wa tanganyika wanakosa ajira nafasi zetu baadhi zimechukuliwa na wazanzibar ilihali tukienda kwao hatuzipati
Kama muungano hautakuwa na usawa Bora uvunjwe tu
 
Back
Top Bottom