Lissu aingia matatani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lissu aingia matatani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OSOKONI, Aug 9, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  MNADHIMU wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu ameshtakiwa kwenye Kamati ya Kinga, Haki na Maadili ya Bunge kutokana na kauli yake kuwa baadhi ya wabunge waliokuwa kwenye Kamati ya Nishati na Madini wana mgongano wa kimasilahi.

  Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na mbunge aliyefungua malalamiko hayo, Charles Mwijage (Muleba Kaskazini-CCM), zinasema kuwa mbunge huyo wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chadema, alimkashifu.

  Hivi karibuni, Tundu Lissu alizungumza na waandishi wa habari bungeni na kuwataja wabunge saba kuwa wana mgongano wa kimasilahi kwenye Kamati ya Nishati na Madini.

  Wabunge hao wote kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni Sara Msafiri (Viti Maalumu), Mariam Kisangi (Viti Maalumu), Christopher Ole Sendeka (Simanjiro), Vicky Kamata (Viti Maalumu), Yusuph Nassir (Korogwe Mjini), Charles6 Mwijage (Muleba Kaskazini) na Munde Tambwe (Viti Maalumu).

  Akizungumza na Mwananchi juzi, Mwijage alikiri kumwandikia Spika wa Bunge, Anne Makinda kumlalamikia kuhusu Lissu.

  "Ni kweli nimemwandikia barua Spika na nimeshaikabidhi, nataka shauri letu lisikilizwe na nitendewe haki," alisema.

  Alisema kutokana na matamshi ya Lissu, vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ilimwandika kuwa ni mla rushwa na kuathiri hadhi yake.

  Mwijage pia amelilalamikia gazeti la Tanzania Daima kuwa liliandika habari hiyo kwa kumtaja kuwa ni mla rushwa na baadaye likasambazwa jimboni kwake kwa masilahi ya kisiasa.

  Kwa upande wake, Lissu alisema hajaitwa na Kamati ya Bunge kuhusu suala hilo lakini alikiri kupata taarifa hizo kutoka kwa Mwijage.

  "Nimekutana na Mwijage akaniambia amenishtaki na mimi nimemuuliza ‘unajua nilichokisema?' na yeye akaniuliza kwani ulisema nini? Nimemweleza kuwa mimi nawajibika kwa maneno yangu kuwa yeye ana mgomgano wa kimasilahi kwa kuwa consultant (mshauri) wa kampuni ya Puma. Siwezi kumwita mtu mla rushwa kwa kuwa sina ushahidi na hilo," alisema
   
 2. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Matata yapi?

  Mgongano wa kimaslahi si matusi wala kashfa.
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  anawewesekatu Lisu habari nyingine kwanza inaonyesha hajui hata maneno aliyoyasema lisu neno mgongano wa masilahi.
   
 4. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  Lissu ni lawyer anajua sana kuchagua maneno ya kuongea
   
 5. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Lissu ndo yuko matatani au Mwijage?
   
 6. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Mwijage muaaache Tundu Lissu,Jeikei kamshindwa utamuweza wewe? TL anasimamia hoja yake kwamba wewe una maslahi na tanesco so haufai kuwa humo fullstop.
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Kumbe ni hatari kukimbilia kauli za wanasheria! Lissu aliitisha kikao na waandishi wa habari huku kukiwa na sakata la wabunge kutuhumiwa kula rushwa huko TANESCO. Akawataja wabunge kadhaa tukadhani ametaja waliokula rushwa lakini leo anasema hakusema kuwa Mwijage (Aliyetajwa) amekula rushwa. Anasema alichokisema ni kuwa Mwijage ana mgongano wa masilahi kwa kuwa ni mshauri wa Puma! Patamu hapo.
   
 8. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,916
  Likes Received: 2,342
  Trophy Points: 280
  Tundu Lissu aangalie sana asijekuwa ngoma inayotaka kupasuka.
  Mdomo uliponza kichwa.
   
 9. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,728
  Likes Received: 12,795
  Trophy Points: 280
  Sasa nani hapo yuko matatani kati ya mwijage na lissu?

  Yan habari hile hile ya kila siku!
  Lissu aliwataja watu wenye mgongano wa kimaslai na Tanesco.

  Tunajua mmeshaanza kutapatapa ili kamati iwasafishe.
   
 10. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  magazeti hutia chumvi ili wauze nakala nyingi!
   
 11. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,728
  Likes Received: 12,795
  Trophy Points: 280
  Lissu anajua alicho kifanya.
  Labda muunde zengwe kujisafisha!

  Lakini kamwe lissu hakukurupuki.

   
 12. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mtoa hoja hivi kweli anajua maana ya kuingia matatani au ameamua kujiandikia tu? Huwezi kutoa dai ambalo ni haki kisheria ukaingia matatani vinginevyo neno matata lina maana nyingine tofauti na tunayojua. Yaelekea mtoa hoja ameamua kuingia mtego wa ushabiki na kutofikiri kiasi cha kuandika kitu ambacho hakifanani na kichwa cha habari. Lissu hajaingia matatani. Kama kuna utata si mwingine bali uelewa wa mtoa hoja ambaye kwa mujibu wa michango hapa ameingia matatani mwenyewe kwa kuzusha.
   
 13. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #13
  Aug 9, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  'TL: Unajua nilichokisema?
  Mwijage: Kwani ulisema nini?'

  Sasa mh Mwijage kama hujui alichokisema umeshitaki nini?
   
 14. m

  manucho JF-Expert Member

  #14
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,410
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hili suala si lipo kwenye uchunguzi sasa unaweza ukalizungumzia au kumshitaki mtu wakati uchunguzi wa kamati haujamalizika au inakuwaje hapa
   
 15. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #15
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,081
  Likes Received: 6,544
  Trophy Points: 280
  Kwani Lissu kakosea nini hapo,
  unataka kusema hakuna mgongano wa kimaslahi tanesco.
  tena hawa wezi wametuletea balaa hata sisi wateja na kusababisha tunalipa bili
  kubwa kwa matumizi kidogo, tena tanesco ni wizi mtupu.
   
 16. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #16
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Lissu amesema ni Mgongano wa Kimaslahi lakini tunachojua sisi yeye na wenzake ni Wezi na Mafisadi wakubwa ambao wameliletea hili taifa hasara kubwa
   
 17. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #17
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  I will not comment maana si haki swala liko kwenye kamati tunakatazwa kulisemea .hehehhe Tanzania bwana
   
 18. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #18
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,861
  Likes Received: 2,786
  Trophy Points: 280
  Hapo hakuna matata yoyote kwa Lisu, labda yeye Mwijage ana kesi ya kujibu kwa kufungua kesi bila kujua shitaka lenyewe! Kwani ulisemaje? Sasa umeshitaki nini tumb..f wewe? Wabungo wa Mwabwepande siku zote wanatumia RIBUSAMA kufikri. Nani wa kumweza Tundu Lisu? Mwulizeni Nkapa habari ya Lisu!
   
 19. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #19
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye red ni kichekesho! Ameshaki kutokana na maneno ya kwenye magazeti na mtandaoni au ameshtaki kwa maneno aliyoyasikia mtaani? Maana inaonekana hajui alichokisema Lissu!
   
 20. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #20
  Aug 9, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  aaah wapi,Lissu ni mjanja hata J.K analijua hilo na kumwogopa juu
   
Loading...