Lissu aingia matatani

Kauli ya Lissu kisheria hambani, ila kwa kuwa waandishi wa magezeti ni vihio na hawajui kutafsiri kauli za kisheria ndo wameandika kuwa Lissu kasema hao aliowataja ni wala rushwa, huyu ni mwanasheria aliyebobea ndo maana hata watakapo muita atashinda tu na kuwaumbua.
 
Kumbe ni hatari kukimbilia kauli za wanasheria! Lissu aliitisha kikao na waandishi wa habari huku kukiwa na sakata la wabunge kutuhumiwa kula rushwa huko TANESCO. Akawataja wabunge kadhaa tukadhani ametaja waliokula rushwa lakini leo anasema hakusema kuwa Mwijage (Aliyetajwa) amekula rushwa. Anasema alichokisema ni kuwa Mwijage ana mgongano wa masilahi kwa kuwa ni mshauri wa Puma! Patamu hapo.

Pole. Maana wewe na Mwijage wala hamna tofauti. Wote hamjui Tundu Lissu alisema nini hasa. Mtaendelea kuingizwa kingi. Suala la msingi ambalo ungeweza kuhoji hapa, ni kwa nini kwenye habari za tv hayakusikika hayo maneno ambayo yaliandikwa kwenye 'headlines' za baadhi ya magazeti kesho yake!

Nikupatie kitu kidogo tu hivi; siku hiyo ya habari hizo zikiwa zimepamba vyombo vya habari, nilikuwa najadiliana na mwanahabari mwenzangu mmoja hivi. Nikamwuliza mbona umeandika maneno mengine tofauti na yale aliyosema Lissu, akajibu "sasa unafikiri wananchi wataelewa nini ukiandika mgongano wa maslahi, hilo wasomaji hawajui, unawaandikia kile wanachojua." Nilitamani kulia.

Kila la heri Mwijage na hawa akina Kimbunga.
 
Wenye mgongano wa kimaslahi ndio wapo matatani sio mh.tundu lissu............................
 
'TL: Unajua nilichokisema?
Mwijage: Kwani ulisema nini?'

Sasa mh Mwijage kama hujui alichokisema umeshitaki nini?

Ha ha haaa!!! hii taaamu kwelikweli. huyu mwijage anaweweseka kwa sababu puma ndo watu wake na walikosa tenda mara kwanza baada ya kwenda na bei ya 1900. kuona hivyo wakazunguka mbuyu nyumanyuma wakaenda wakalegeza mpaka 1450. inawezekana mwijage ndo aliratibu hizi za sarakasi za gizani nje ya meza, halafu wakaja public na shangwe nyingi eti tumeokoa bilion 3 kwa wiki mbili sawa na bilion 6 kwa mwezi!! SASA CHA KUJIULIZA, NI KAMA KWELI NIA YAO ILIKUWA NJEMA, KWA NINI WALIANZA NA BEI AMBAYO KIMSNGI ILIKUWA NI KUTUMALIZA KABISA??? NA KWA NINI WALISHUSHA BEI NA KUKUBALIWA BILA KUPTIA PPRA??? hawa wakina mwijage sio wema hawa, ina hajui kama puma walizunguka mbuyu??? na kama anajua yeye kama kiongozi mwadilifu kama anavyotaka tumwamini ameshatoa tamko gani la kulaani hicho klitendo cha watu wake hao wa PUMA??? huyu bwana ana jambo, si ajabu ANAWEWESEKA.
 
TL is a very smart lawyer of our time.
TL huwa hakurupuki wala haropoki hata siku moja. TL akitamka au kusema neno amelifanyia kazi na anajua anachokizungumza na kukisimamia!

Kinachoonekana hapa ni ubabaishaji wa Wabunge wa CCM ambao walitajwa na TL kwenye sakata la TANESCO kwamba baadhi yao walihongwa na Makampuni ya mafuta yanayoiuzia TANESCO mafuta mazito kwa ajili ya kufua umeme na wengine wanafanya biashara hiyo hiyo ya kuuza mafuta kwa TANESCO!

Tumesikia kutoka kwa Bi Mkora Anne Makinda juu ya kuundwa kwa Kamati ya kuchunguza sakata hilo Bungeni inayoongozwa na Mhe. Ngwilizi na kwamba TL atakuwa ni mtu wa kwanza kuhojiwa kama shahidi! Ninatilia mashaka sana juu ya umakini wa Bi Anne Makinda na hiyo Kamati yake. Picha inayojaribu kujengwa hapa ni kutaka KUWASAFISHA WABUNGE WA CCM WANAOTUHUMIWA KWENYE SAKATA HILI.

Mimi sioni mantiki ya kudai eti TL ndiye akatoe au kuleta ushahidi kwenye Kamati hii ilhali kuna TAKUKURU na POLISI wanaotakiwa kuwakamata na kuwahoji watuhumiwa na hatimaye kuwafikisha Mahakamani. Hii Kamati ni kiini macho tu,mwisho wa siku tutasikia kwamba tuhuma hizo dhidi ya Wabunge wa CCM si za kweli baali ni za uzushi mtupu na Tundu Lissu ameshindwa kuithibitishia Kamati kama wale Wabunge walikuwa na mgongano wa Kimaslahi na iwapo kama walipokea mlungura kutoka kwa Makampuni hayo ya mafuta!!!

Tunajua CCM wanavyolindana linapokuja swala la Rushwa na Ufisadi! Tusubiri hizo wiki 2 tuone Kamati itakuja na matokeo gani. I predict that many Tanzanians will be very dissappointed by the findings of the Ngwilizi Committee!

Period.
 
Pole. Maana wewe na Mwijage wala hamna tofauti. Wote hamjui Tundu Lissu alisema nini hasa. Mtaendelea kuingizwa kingi. Suala la msingi ambalo ungeweza kuhoji hapa, ni kwa nini kwenye habari za tv hayakusikika hayo maneno ambayo yaliandikwa kwenye 'headlines' za baadhi ya magazeti kesho yake!

Nikupatie kitu kidogo tu hivi; siku hiyo ya habari hizo zikiwa zimepamba vyombo vya habari, nilikuwa najadiliana na mwanahabari mwenzangu mmoja hivi. Nikamwuliza mbona umeandika maneno mengine tofauti na yale aliyosema Lissu, akajibu "sasa unafikiri wananchi wataelewa nini ukiandika mgongano wa maslahi, hilo wasomaji hawajui, unawaandikia kile wanachojua." Nilitamani kulia.

Kila la heri Mwijage na hawa akina Kimbunga.

Mkuu Tumaini Makene naona unasoma kinyumenyume! Hukunielewa hata kidogo umeruka tu na kupiga chogo chemba huku umevaa msuli! Mantiki ya post yangu ni kwamba ni vizuri kuwa makini na wanasheria kwa kuwa wao ni makini. Watu walikimbilia kuandika kuwa ametaja wala rushwa lakini akiwa kama mwanasheria anajua madhara yake hivyo siyo kwamba aliwataja wala rushwa kama Mwijage bali alisema Mwijage ana mgongano wa kimaslahi; hapo si kumtaja kuwa anakula rushwa. Lakini kwa kuwa wakati huo kulikuwa na sakata la wabunge kuambiwa wamekula basi waandishi kama wewe wakakurupuka na kuandika kilichokuwa vichwani mwao na wala si kauli ya mtoa kauli. Nawajua wanasheria na najua kauli zao si za kukurupuka wako makini hasa katika kauli.

Mkuu usikimbie kujibu bila kusoma chini ya mstari.
 
Last edited by a moderator:
Inaonekana wewe ni Gamba na kada harufu wa Chama cha mabwepande na nadhani wewe ni wassira na msura wako wakifisadi ule Lisu ni mpiganaji wa uhakika na tunategemea awe Tz prezoo wa 2020 baada ya slaa!Gamba we!
Bwana mdogo kama huna pointi ya kuandika waachie wenye akili wakuandikie.
Kwa kawaida upuuzi wa kijinga kama huu unatolewa na watu wenye ubongo wa chekechea.
 
We Jamaa una usingizi nini ??..Matata yapi mbona kila kitu kimejijibu.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Nimekutana na Mwijage akaniambia amenishtaki na mimi nimemuuliza ‘unajua nilichokisema?' na yeye akaniuliza kwani ulisema nini? Nimemweleza kuwa mimi nawajibika kwa maneno yangu kuwa yeye ana mgomgano wa kimasilahi kwa kuwa consultant (mshauri) wa kampuni ya Puma. Siwezi kumwita mtu mla rushwa kwa kuwa sina ushahidi na hilo," alisema
Habari za mujini zinaanza kufika Bungeni.. saafiiii.....
 
Back
Top Bottom