Uchaguzi 2020 Lissu aahidi kufumua madudu ya Magufuli

Haya ndiyo tunayoyataka Watanzania siyo kunyanyaswa, kudhalilishwa, kubambikiwa kesi etc utadhani tuko Afrika Kusini ya MAKABURU.
Watanzania wengi wameumizwa ndani ya nchi yao kuliko Makaburu walivyowaumiza watu wa Afrika Kusini ya kipindi kile cha Apatheid Rule.Inasikitisha sana kwa watawala wetu kuamua kuteka,kutesa,kuua,kubambikia kesi na kuwafilisi raia wenzao ndani ya nchi huru.Mambo haya yanatakiwa kukomeshwa mara moja.
Watanzania Twendeni na Mh.Lissu uchaguzi huu ili tuitengeneze upya mifumo yetu ya Utawala kwa kuandika Katiba mpya mara baada ya Uchaguzi Mkuu 2020 kuanzia pale ilipokomea Tume ya Mbadiliko ya Katiba ya Jaji Warioba.Hilo tu ndiyo dawa ya kutibia vidonda vyote vilivyosababishwa na tawala zilizotangulia.Wakati ni Sasa!
 
Kumwelewa Lisu ni lazima uwe na akili.

Kama mtu hujui umuhimu wa sheria katika maebdeleo, ni dhahiri una kasoro kichwani.

Nimekuwepo kwenye taasisi za kimataifa tukifanya ranking ya mataifa yote Duniani kwenye favorability ya investment environment. Item ya kwanza ni mfumo wa sheria wa nchi husika, pili ni mfumo wa kodi wa nchi husika, baada ya hapo ndiyo vinafuata vitu vingine.

Nchi yenye mfumo mbaya wa sheria na/au mfumo mbaya wa kodi, huua na hufukuza uwekezaji. Na bila uwekezaji hakuna maendeleo.

Mfano dhahiri ni huu wa Taifa letu. Kutokana na sheria nyingi mbaya na mfumo wa mahakama tegemezi, na mfumo mbaya wa kodi, kufuatia mabadiliko mbalimbali yaliyofanywa awamu hii, ukuaji wa uwekezaji wa nchi yetu umeanguka toka 28% mpaka 4%. Na hiyo ndiyo sababu inayomfanya Magufuli asiongelee kabisa juu ya uchumi wa viwanda. Kwenye uwekezaji, awamu hii imeanguka vibaya mno. Na uwekezaji ni mama ya maendeleo. Uwekezaji ndio hutrngeneza ajira, uwekezaji hukuza technolojia, uwekezaji huhuisha mzunguko wa fedha, uwekezaji huongeza makusanyo halisi ya serikali, n.k. Awamu hii imeshindwa vibaya kwenye uwekezaji, na kusababisha kushindwa katika mambo mengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama huu ndo ufahamu wako, ni halali kumshabikia Lissu. Uwekezaji una maana gani? Watu kutoka nje kuja kuweka ivestments? Kama ni hivyo nchi ipi duniani iliwahi kuendelea kwa uwekezaji wa aina hiyo? Eti unaamini uwekezaji unakuza teknolojia, unajua maana ya teknolojia au uko chuoni bado unajifunza? Naomba ukomae na shule, boss! Maneno kama sheria nyingi; Nyingi ni namba ipi dunia hii? Mabadiliko mbalimbali; mbalimbali ni mangapi?
Pole!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom