Uchaguzi 2020 Lissu aahidi kufumua madudu ya Magufuli

Hapana. Na Lissu ndiye mwenye rekodi dhidi ya ubeberu wa kunyonya wanyonge kupitia kupitia migodi. Rejea harakati zake na maandiko yake toka miaka ya 90. Sisi akina fulani tunataja ubeberu kama fasheni tu.
Mbona tulipo leta hiyomikataba mibovu, huko bungenii kwa ajiri ya marekebisho lisu alitusaliti na kutetea mabeberu tena aka akasema kwa sautii kuu akiwtisha watanzania eti tukigusa mikataba ya madinii tutanyolewa nywelee bila majiii. Kama aliandika vitabu vinguu juu ya unyonyaji wa madini, alishindwa nini kuuungana na wazalendo ilikujadili kipi kifanyike juuu ya kupigania mali zetuu??
 
Too good to be true,

Hakuna nchi ya aina hiyo duniani.

Huu ni utapeli mchana kweupe.

Ni bora ushindwe kufikia lengo kuliko kulenga kunyamazisha watanzania na kuwatisha hadi kwenye kampeni mtu anasema kabisa kama hatachaguliwa hatapeleka maendeleo hivi huyo si anatakiwa kuenguliwa kwenye ugombea
 
Mgombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu ameahidi kuwa akishinda nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu, Serikali atakayoiongoza itafuta sheria zote zinazominya uhuru wa habari na haki za kiraia zinazotumiwa na Serikali iliyopo madarakani kukandamiza watu.

Mgombea huyo ametoa ahadi hiyo Septemba 26, 2020 wakati wa mkutano kati yake na Wahariri na Waandishi wa habari waandamizi uliofanyika jijini Mwanza, Kaskazini Magharibi mwa Tanzania.

Uhuru wa maoni na utawala wa sheria

Mgombea huyo ambaye mikutano yake ya kampeni inahudhuriwa na umati wa wananchi ametaja miongoni mwa sheria zitakazopitiwa upya, kubadilishwa nap engine kufutwa ni ile inayounda Idara ya Habari Maelezo na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambayo kiuhalisia ina chembechembe za ukoloni kwa sababu zinaminya uhuru wa maoni, mawazo, kujieleza, kutafuta na kupata habari.

“Chini ya Serikali itakayoongozwa na Chadema uhuru wa maoni, kujieleza, kutafuta na kupata habari utatekelezwa bila kuwekewa vizingiti kama inavyotakiwa kwa mujibu wa Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977,” anasema Lissu ambaye ni mwanasheria na wakili mahiri nchini Tanzania

Anaongeza; “Taratibu zitakuwa kama ilivyo nchini Ghana ambako siyo tu mtu haitaji usajili kuanzisha chombo cha habari, bali pia hakuna udhibiti wa vyombo vvya habari.”

Wakati akiahidi kulivunja Idara ya Habari Maelezo, mgombea huyo pia ameahidi kuinyang’anya TCRA nguvu ya kupiga faini na kufungia vyombo vya kielektroniki, badala yake itakuwa kuvisajili kwa ajili ya kumbukumbu za kiofisi.

Kuhusu utawala wa sheria, mgombea huyo amesema Serikali itakomesha maamuzi na vitendo vya kibabe vya viongozi wa ngazi zote akitolea mfano agizo la Rais John Magufuli la kuwabomolea nyumba wakazi wa eneo la Kimara, jijini Dar es Salaam licha ya kuwepo zuio la Mahakama.

“Kwa ajili ya kuweka misingi ya kuwazuia wengine watakaoongoza Taifa hili kuonea watu, Serikali chini ya Chadema itawalipa fidia wananchi wote waliovunjiwa nyumba na mali zao zingine kuharibiwa bila kulipwa fidia,” anasema

Kundi lingine litakalofidiwa ni lile la watu waliokamatwa, kuswekwa rumande, kufunguliwa kesi, kufilisiwa au kufungwa kwa uonevu.
“Ni bahati mbaya hiyo bili itakuwa kubwa, lakini tutatafuta fedha hizo. La msingi kwanza tukubaliane kuwa wana haki ya kulipwa kwa mujibu wa sheria,” anasema Lissu

Apangua propaganda ya ubeberu
Akijibu swali kuhusu tuhuma kuwa wanaopigania na kutetea uhuru wa maoni na haki kwa makundi yote ya kijamii wanatumiwa na mabeberu, mgombea huyo amesema hoja hiyo hutumiwa na waliofilisika kisiasa kwa sababu kiuhalisia uhuru wa maoni, demokrasia na maendeleo ya watu ni masuala ya msingi na asili ya binadamu.

Ameahidi kuwa Serikali atakayoongoza itajenga na kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Mataifa mengine bila kusahau taasisi na mashirika ya kimataifa ambao ni wadau muhimu wa maendeleo.

“Tanzania haiwezi kuendelea bila kutengeneza mahusiano na nchi zote marafiki, wahisani, taasisi na mashirika ya kimataifa, asasi za kiraia na wadau wengine wa maendeleo ili kuvutia mitaji na teknolojia kutoka nje,” anasema na kuongeza

“Hatuwezi kuendelea bila kushirikiana na wengine. Hutuwezi kullima na kula korosho zetu wenyewe, Dhahabu, almasi na madini mengine na hata mbuga na hifadhi zetu zinategemea soko na wageni kutoka nje kwenye hizo nchi zinazoitwa za mabeberu.”

Pamoja na kuboresha mahusiano kimataifa, Lissu pia ameahidi kuweka mazingira mazuri yatakayovutia uwekeza na biashara ndani na nje ya nchi na hatimaye kuongeza kipato cha wananchi na Serikali na hatimaye uwezo wa kutekeleza miradi ya maendeleo.

“Kukuza uchumi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kunahitaji muunganiko na ushirikiano wa kidunia. Hatuwezi kujitenganisha na dunia,” anasisitiza Lissu

Amesema hata Serikali ya CCM inayoeneza propaganda ya ubeberu nayo inategemea na kushirikiana mataifa na taasisi za nje kutekeleza miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo sekta ya ujenzi wa barabara.

Ametumia mkutano huo kuahidi kuondoa ubaguzi uliopo hivi sasa katika mikopo ya elimu ya juu ambapo wanafunzi waliosoma shule binafsi za msingi na sekondari wananyimwa au kupewa asilimia ndogo ya mkopo ikiamini kuwa wazazi au walezi wao wana uwezo kiuchumi, jambo ambalo si sahihi.

“Tutaondoa ubaguzi huo na kushusha kiwango cha riba ya mikopo ya elimu ya juu kutoka asilimia 15 za sasa hadi kiwango cha awali kabida cha asilimia tatu ambayo itaanza kulipwa baada ya aliyekopa kupata ajira au kipato halali ndani au nje ya nchi,” anasema

CCM wahaha kuhujumu msafara wake
“Mgombea wa CCM hakupata mapokezi mazuri alipokwenda mkoani Kagera, sasa walipoona mapokezi yetu wakaamua kuwaanda vijana kuvuruga msafara wetu kwa kuturushia mawe wakiwa kwenye jengo la CCM,” anafichua Llissu

Hata hivyo, mgombea huyo anawapongeza askari polisi waliokuwa wakiongoza msafara wake kwa kulidhibiti kundi hilo.
Anasema hali kama hiyo pia ilijitokeza mkoani Geita ambako kundi la vijana walipanga mawe kuzuia msafara wake kupita kwenye barabara inayopita jirani na ofisi za CCM.

“Kwa mara nyingine polisi waliwadhibiti na kwa Geita walitawanywa kwa mabomu ya machozi. Hata hivyo, nimesikitika kupata taarifa kuwa, RPC na OCD wa Geita nao wamehamishwa kosa lao likiwa ni kuwapiga mabaomu wana CCM,” anasema kwa masikitiko

Anasema hata mkoani Songwe pia amepata taarifa za mkuu wa upelelezi wa mkoa huo kuhamishwa baada ya kukataa amri haramu ya kuwakamata viongozi wa wagombea wa Chadema wakati wa ziara yake.

Pamoja na viongozi hao wa polisi kukumbwa na madhila hayo, Lissu amewapongeza askari wa jeshi hilo kwa kufanya kazi kwa weledi tangu kampeni za uchaguzi mkuu zilipoanza Agosti 26, mwaka huu.
Vyombo vya usalama vinafanyakazi kwa weledi wa hali ya juu katika kampeni zinazoendelea bila kujali Chama cha siasa chini ya Dr. John Pombe Joseph Magufuli, Lissu mwenyewe karidhia ukitangulia kuliona jua na ukakubali kufungua macho yako utakuwa msaada kwa kila Mmoja ambaye kafuata nyuma yako kuliona jua, Hamna mtanzania mzalendo anayeshindwa kung'amua kiongozi sahihi kati ya JPM na TAL.
 
Pumbavu kwelikweli.Utadhani atachaguliwa kweli.
Mkuu uko Dunia ipi?? Unajua hivi sasa ccm ina hali gani au uko huku mitandaoni huoni hali halisi?? Unafahamu Jiwe kakatiza kampeni zake? Je sababu unafahamu?

Siasa hazilazimishwi kwa mtutu wa bunduki wala lugha za vitisho. Bali kwa lugha nyepesi ktk ushawishi wa kisera.
 
Acheni kulinganisha lissu na vitu vya ajahu ajabu. Kilicho baki ji kuiba kura.. hata mkishinda cha moto mmekipata.
Mtavuna porojo zenu Oct 28.Watu wajinga pekee ndio watakao piga kura kwa Lissu. Watanzania tuna macho ya kuona na masikio ya kusikia.Magufuli kafanya kazi kubwa mno, ambayo hata robo yake saccos yenu isingeweza.
 
Miaka 5 tu kajenga mahoteli na uwanja wa ndege kijijini kwake akipewa 10 si atahamishia hazina yetu kwao. Mtu msafi aogopi demokrasia, mtu msafi uweka Mambo wazi, why Siri juu ya mikataba ya miradi kwa Kodi zetu. Sisi tulipe Kodi wao kazi yao Ni kuzitafuna tumekuwa vibarua wao.
 
Kweli... Hawa wakoloni weusi ccm tumewachoka, tunawapumzisha rasmi 28/10/2020
Toka lini mtu mweusi akawamkolonii?? Soma historian zotee. Sisi tunajua tunaekwenda kumgalagaza October , siio nyie chadema, sisi tutakaye mgalagaza October ni beberu lililoko nyuma yenuu.
 
Toka lini mtu mweusi akawamkolonii?? Soma historian zotee. Sisi tunajua tunaekwenda kumgalagaza October , siio nyie chadema, sisi tutakaye mgalagaza October ni beberu lililoko nyuma yenuu.
Mkuu usijihangaishe nao wamejaa mitandaoni kupeana moyo wanadhani kushinda uchaguzi ni kazi rahisi. Hawataamini kitakachowakuta mwezi ujao. Uzuri siku zinaenda fasta. November 1 wote humu watakuwa wamenywea.
 
Mkuu usijihangaishe nao wamejaa mitandaoni kupeana moyo wanadhani kushinda uchaguzi ni kazi rahisi. Hawataamini kitakachowakuta mwezi ujao. Uzuri siku zinaenda fasta. November 1 wote humu watakuwa wamenywea.
Hata lisu mbona analifaham saaanaa.
 
Kazi kupora tu ardhi za wanyonge maccm ni hatari Sana kwa maendeleo ya watanzania
IMG_20200926_232608.jpg
IMG_20200926_232604.jpg
IMG_20200926_232602.jpg
IMG_20200926_232558.jpg
 
A
Huyo jamaa yenu siyo intelligent man, anasahau kama kuna kesho pia, muache aendelee kulikoroga baada ya oktoba 28 ndiyo ataijua CCM
Amelikoroga wapi? Mimi ni mwana CCM lakini akili yangu haijafungiwa Kwenye box. Huyu jamaa ana hoja, tujikite kujibu hoja zake. Mimi nimeshindwa kuzipangua maana kila anachozungumza kina akisi hali halisi iliyopo.
 
Toka lini mtu mweusi akawamkolonii?? Soma historian zotee. Sisi tunajua tunaekwenda kumgalagaza October , siio nyie chadema, sisi tutakaye mgalagaza October ni beberu lililoko nyuma yenuu.
Ukoloni siyo rangi, bali ni utawala haramu wa kimabavu unaotekelezwa na kikundu Cha wachache kwa hila, kinyume na matakwa ya wananchi/watawaliwa
 
Musitufanye kama nchi nzima ni mali ya CCM na CHADEMA. Hadi muda huu hujagundua kwamba Lissu siyo mtu wa kuwa rais?
Angalia madudu unayoandika, hayo ndo yamfanye apewe kura? Yaani yeye atakuwa rais wa kurekebisha na kutunga sheria tu, ili iweje? Tangu lini sheria zikaleta maendeleo. Wapi alikoona? Huko Ubelgiji? Na tena kwa ulimbukeni wake na wazungu , na kunyoa kiduku ktk umri wa zaidi ya miaka 50, mwambie akatibiwe tena. Kichwa kina kasoro hicho!
Kumwelewa Lisu ni lazima uwe na akili.

Kama mtu hujui umuhimu wa sheria katika maebdeleo, ni dhahiri una kasoro kichwani.

Nimekuwepo kwenye taasisi za kimataifa tukifanya ranking ya mataifa yote Duniani kwenye favorability ya investment environment. Item ya kwanza ni mfumo wa sheria wa nchi husika, pili ni mfumo wa kodi wa nchi husika, baada ya hapo ndiyo vinafuata vitu vingine.

Nchi yenye mfumo mbaya wa sheria na/au mfumo mbaya wa kodi, huua na hufukuza uwekezaji. Na bila uwekezaji hakuna maendeleo.

Mfano dhahiri ni huu wa Taifa letu. Kutokana na sheria nyingi mbaya na mfumo wa mahakama tegemezi, na mfumo mbaya wa kodi, kufuatia mabadiliko mbalimbali yaliyofanywa awamu hii, ukuaji wa uwekezaji wa nchi yetu umeanguka toka 28% mpaka 4%. Na hiyo ndiyo sababu inayomfanya Magufuli asiongelee kabisa juu ya uchumi wa viwanda. Kwenye uwekezaji, awamu hii imeanguka vibaya mno. Na uwekezaji ni mama ya maendeleo. Uwekezaji ndio hutrngeneza ajira, uwekezaji hukuza technolojia, uwekezaji huhuisha mzunguko wa fedha, uwekezaji huongeza makusanyo halisi ya serikali, n.k. Awamu hii imeshindwa vibaya kwenye uwekezaji, na kusababisha kushindwa katika mambo mengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom