Lipumba, unalipeleka wapi taifa hili?

Lipumba, unalipeleka wapi taifa hili?

Unapotaka kushughurika na watu wa Mtwara usitumie propaganda mahitaji yao yapo wazi WANASIASA siyo tatizo pale
 
mkuu kwa nini tusijadili maendeleo ya mtwara kwa kina na kwa mantiki ya kutatua matatizo ya mtwara na siyo kutatua kwa vurugu kama unavyofikili wewe,na unafikiri vurugu na mandamano ndiyo yataleta maendeleo.

nikukumbushe tu kuwa Maendeleo yaliyoletwa na Gaddafi kule Libya yalitokana na Mapinduzi, Rwanda ya leo haishikiki kimaendeleo kwa sababu watawala wanajua nini kitatokea wakifanya fyongo makusudi, China ya leo iko vile unajua source yake, hebu angalia Cuba ya Fiedel Casto uone. Target ni maendeleo, njia ilosaidia kupatikana kwake does not make any difference, kikubwa ujue hakuna machafuko ya kudai haki yalodumu milele na yote yalipomalizika maendeleo yamekuwepo

Umeshawahi kujiuliza dunia ya leo ingekuwaje kama Hiltler asingetolewa na vita ya pili ya dunia? Marekani ingekuwa wapi kama siyo mapinduzi ya 1770's, ingekuwa wapi ufaransa ya leo, Mkwawa je, angeishi miaka 100 ka bi Kidude kama asingepapana na wajerumani?

Yuko wapi Steven Bicco, wapi Lumumba, au unajua sababu ya mapinduzi Zanzibar?
 
mkuu dua la kuku halimpati mwewe unaweza kutangulia ukamwacha jk kwa sabu mungu siyo athumani kaka؛

Hizi ni methali tu za kiswahili na hazina ukweli wowote. No scietific proof
 
AGRRECO Wameacha kuzalisha umeme na sasa wanafanya biashara ya mafuta?

mkuu, hivi ulikuwa hujui? unafikiri yale mafuta waliyokuwa wanatumia kuendeshea mitambo yao yalikuwa yanatoka wapi? ingawa wanazalisha umeme lakini pia wana wanaendesha biashara ya mafuta kwa kutumia kampuni ya..........
 
Tujiulize pia kama wananchi wanaojitambua wanahitaji kuchochewa ili kudai haki zao?
 
halafu AGGRECO inawauma sana kuona tatizo la umeme linaisha nchini. wanafurahia matatizo haya ili wao waendelee kutuuzia umeme kwa bei kubwa na waiuzie tanesco mafuta kwa bei kubwa kupitia hayo makampuni yao ya mafuta
 
nikukumbushe tu kuwa Maendeleo yaliyoletwa na Gaddafi kule Libya yalitokana na Mapinduzi, Rwanda ya leo haishikiki kimaendeleo kwa sababu watawala wanajua nini kitatokea wakifanya fyongo makusudi, China ya leo iko vile unajua source yake, hebu angalia Cuba ya Fiedel Casto uone. Target ni maendeleo, njia ilosaidia kupatikana kwake does not make any difference, kikubwa ujue hakuna machafuko ya kudai haki yalodumu milele na yote yalipomalizika maendeleo yamekuwepo

Umeshawahi kujiuliza dunia ya leo ingekuwaje kama Hiltler asingetolewa na vita ya pili ya dunia? Marekani ingekuwa wapi kama siyo mapinduzi ya 1770's, ingekuwa wapi ufaransa ya leo, Mkwawa je, angeishi miaka 100 ka bi Kidude kama asingepapana na wajerumani?

Yuko wapi Steven Bicco, wapi Lumumba, au unajua sababu ya mapinduzi Zanzibar?

umeisoma vizuri american revolution na umeweza kujiuliza wamarekani wakati wanafanya mapinduzi ya kilimo walitumia method gani na umejaribu kujiuliza kwa nini yale makampuni ya mafuta yanapambana gesi isifanye kazi na unafikiri kwa nini libya imerudi kulekule na unakubuka wakati wa vita ya 1 na 2 ujeruman ilikuwa the reading power na unakumbuka kwa nini german ilipigwa gape na marekani.
 
halafu AGGRECO inawauma sana kuona tatizo la umeme linaisha nchini. wanafurahia matatizo haya ili wao waendelee kutuuzia umeme kwa bei kubwa na waiuzie tanesco mafuta kwa bei kubwa kupitia hayo makampuni yao ya mafuta

Nani aliyewaleta Aggreco? Nani aliwapa mkataba wa kuuza mafuta kwa bei chafu?
 
Lipumba ni mzarendo anataka Mali asili iwanufaishe wananchi moja kwa moja waendelee kukaza watu Wa mtwara mpaka kuendesha wamechoka kuzurumiwa au wewe ni bepari
 
Huyu mleta mada anaonekana anaposti ili kupata buku 7000 lumumba........................,hovyooo haelewi mambo eti Mtwara-mafuta, mara aggreco............................acha ujinga jipange. Inaonekana wewe si msomaji wa vitabu na ripoti............na hata shule unategemea vi-summary kwenye makaratasi kujiandaa na mitihani.........GAMBA wewe
 
mkuu, tamaa za madaraka na fedha ndo zinawaponza

Wewe Lizaboni ndiyo unatumika. Tatizo la CCM siku hizi ikishindwa aidha kuwashawishi wananchi kwa HOJA au kutekeleza ahadi zake inatafuta WITCH HUNTING. Na siku hizi ni vyama vya UPINZANI hasa CDM.

Tamko la Wana Mtwara liliwekwa hapa, wakaeleza nini wanataka wafanyie kabla ya gesi kupelekwa Kinyerezi na Bagamoyo. Badala yake Pinda akaenda Mtwara akajipindua pindua na kudanganya umma kwamba ame solve tatizo la gasi Mtwara.

Ngoma sasa imekuwa zinto, CCM kwa kufahamu kwamba Mtwara CUF ina ushawishi mkubwa kuliko CDM, sasa wamehamishia matatizo ya gesi Mtwara kwa hizo blaaah blaaah kama ulivyoaandika.

Hebu CCM tekelezeni hayo madai ya Wana Mtwara tuone kama kutakuwa na FUJO huko Mtwara. Nayo ni Kujenga kiwanda cha mbolea, kujenga viwanda vya kuchakata gesi Mtwara, sio Bagamoyo na DSM, Kujenga mitambo ya kuzalisha umeme wa gasi Mtwara na baadaye kuuiingiza kwenye gridi ya Taifa, Kupanua bandarini ya Mtwara etc.

Badala ya Serikali ku -address hayo madai ya wana Mtwara sasa imerukia Prof. Lipumba na CUF na hizo propaganda za kuhongwa na makampuni ya mafuta.

Wananchi wa Mtwara hawatazubaishwa na hizo propaganda zenu za mwaka 47
 
Jaman Tz cjui wanakupeleka wap. Ni longolongo 2 kla kona. Maneno mengiii. Lait kama watz 2ngefunga miaka miwl kutumikia nch ye2, 2ngewazd hata hao super powers. Hz siasa znatuulia nch. Ninaona ni bora atokee dictator 1 mzalendo na mweny akil kulko hz demcrasia za kulaumiana na kupelelezana 2
 
Shida yangu mimi na hizi harakati za Mtwara ni aina ya vipaumbele vilivyowekwa na hao wanaojiita wanaharakati. Kwanza tukubaliane ni ujinga kuamini kwamba kila kinachofanywa na CCM ni kibaya.

Hiyo moja, mbili: watu wa Mtwara wamepata mwalimu wa hovyo. Mambo ya msingi wameyaacha badala yake wanadai mambo ya kijinga. Maslahi ya Mtwara yanaambatana na watu wa Mtwara kukubali mabadiliko na sio tabia zile zile za kale zitegemewe kuleta maendeleo.

Tunapaswa kuwa makini na mambo tunayofanya ikiwa hatutapenda kuonekana wajinga huko mbele. CCM wanafurahi tunapofanya fujo za kijinga
 
Hebu CCM tekelezeni hayo madai ya Wana Mtwara tuone kama kutakuwa na FUJO huko Mtwara. Nayo ni Kujenga kiwanda cha mbolea, kujenga viwanda vya kuchakata gesi Mtwara, sio Bagamoyo na DSM, Kujenga mitambo ya kuzalisha umeme wa gasi Mtwara na baadaye kuuiingiza kwenye gridi ya Taifa, Kupanua bandarini ya Mtwara etc.

Wananchi wa Mtwara hawatazubaishwa na hizo propaganda zenu za mwaka 47

Na haya ndio madai yenyewe ya kipuuzi.
 
Nyie magamba mna matatizo, mbona mlipofunga ndoa na cuf hamkutushirikisha, leo ndo mnataka kutuaminisha eti lipumba mbaya, kwani hiyo gesi ina faida gani kwa watz mbona dhahabu haina faida yoyote?? Bado hatujawaelewa mkajipange upya
 
Ni bora umesema chanzo cha habari ni wewe mwenyewe. Kama ulimsikiliza vizuri Prof.Lipumba kwenye mkutano na waandishi wa habari, kauli yake kuhusu rais kikwete kuongezewa mda wa kukaa madarakani haikuwa final and conclusive. Nilivyomwelewa ni kwamba yeye alikuwa anatoa maoni yake kwenye dira ya mchakato wa katiba mpya. Ndio maana alisema kuwa hajui kama rais kikwete anaweza kuongezewa mda wa kukaa madarakani, lakini endapo kuna watu watamshauri hivyo akatae kabisa.<br><br>
 
Huyu jamaa mpuuzi sana pamoja na elimu yake ya uprofesa
 
Back
Top Bottom