Lipumba; ubunge si size yangu.

asahau? Kivipi?
asahau kwani hawezi kuupata, kagombea mara 3 , zote kakosa na still anauwaza, just lime most of the comments above suggests , ata ujumbe hawampi, kama anapenda kuinua uchumi aombe kazi BENKI kuu , kazi ya kiutendaji , sio SIASA
 
Hapo ndipo unaweza kujua kama Prof ni mwanasiasa mwenye malengo au ni mshereheshaji katika Siasa za Bongo.
 
Asiponde kwa kuseam jimbo ni sehemu ndogo sana... Anatakiwa akagombee ubunge na kushinda.. Maana haiingii akilini tangu 1995 yeye anagombea tu na kushindwa..

Jamani ni aibu iliyoje kudharau uwakilishi wa jimbo wakati tumeona jinsi gani wabunge wa upinzani wanavyoweza japo kwa uchache wao kusimamia maslahi ya taifa letu kupitia uwakilishi waoe. Hawa wengine ni kuwasamehe bure ashafilisika atunze vvzr vyeti vyake au navyo ni vya kughushi coz haviendsni na presentantion zake. Rip CUF.
 
akiongea katika kipindi cha baragumu cha chanel ten leo asubuhi akijibu swali, amesema hafikirii kugombea ubunge ambao si size yake, kwa kuwa lengo lake ni kusimamia uchumi wa kitaifa si wa jimbo, jimbo ni sehemu ndogo kwanu, alisema mchumi huyo.

Mwenye hekima mmoja alipata kutamka kuwa "kitu pekee kinachoanzia juu ni kaburi" urais anaoutaka sana prof.lipumba ni kaburi lake la kisiasa.Kwani hawezi kutaka apande ngazi ya kisiasa kwa kuanzia juu itakula kwaketu.Siku moja nipo Mbeya kikazi nakumbuka ilikuwa ni kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu 2010,siku hiyo JK ndo yupo Mbeya mjini,nikiwa ndani ya gari nasikiliza Clouds FM,Prof akawekwa hewani alichoongea kikanifanya niwasikitikie wana CUF,Prof aliulizwa mbona umekuwa ukigombea mara zote lakini mara zote umeshindwa huoni kama ni wkt upishe wengine nao wajaribu? Swali liliulizwa kwa kinamna hiyo samahani kama nitakuwa sijalikumbuka swali vizuri na jibu lake ambalo alilijibu nkwa style hii,"Mimi nafuata nyendo za Rais wa Senegal wkt huo Abdoulaye Wade ambaye kwa miaka ishirini alikuwa akigombea tu mpaka akashinda huo mwaka 2000" Hapo nikaona democracy ndani ya cuf itakuwa at stake kama imebahatika kupata chairperson mwenye misimamo ya hivi,sikukaa sawa mara Prof.Safari nje,Mara Hamad Rashid nje.Hii ni hatari sana na ni attitude hii hii inayong'ang'ania urais wakati hatujaona anawezaje kuinua uchumi wa jimbo.Urais kwa Lipumba ni ndoto za Alinacha,na ndilo litakuwa kaburi lake kisiasa.Atangoja sana na tutamzika akingoja.
 
Huyu mzee wangu naye hata hajui kupima upepo! Wenzake woote ukianza na Mzee Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Dr. Slaa, Lowassa, Sitta, Dr Shein, Membe wameanza na uwakilishi. Sasa yeye anaposema ubunge si size yake kiasi flani nakuwa namshangaaa, anataka tupime vipi utendaji wake kisiasa? Sometime unatakiwa ujifanyie assessment na unaweza ukaanza hata na udiwani uonyeshe utumishi uliotukuka then wananchi wakuombe ugombee nafasi zingine za juu zaidi. Asijipandishe sana aache wananchi wampandishe. Arejee kauli yake ya kuwa Dr. Slaa ni kichuguu na yeye ni mlima kilimanjaro matokeo yake yeye ndiyo akawa kichuguu na Slaa akawa Mlima Meru!
 
Nilishawahi kuuliza kwenye uzi mmoja humu humu.. Nchi gani ambayo wana raisi mwenye hadhi ya u-professor nikatajiwa Malawi kwa maana ya Marehemu Bingwa.. Jibu ambalo ckulipata ni kwamba ni Professor wa fani gani na jee hali ya nchini kwake ikoje mpaka anapata umauti.. Ciku zote ninaamini wagombea urais ni wale wenye elimu za degree ya kwanza au ya pili.. Prof. Lipumba angeachana na siasa na kujikita katika utendaji wa fani yake.. kung'ang'ania kugombea uraisi ni kudhalilisha usomi wake na kutoitendea haki..
 
Back
Top Bottom