nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
Wednesday, 16 March 2011 00:11
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba
TAMKO lililotolewa hivi karibuni na Chadema kuwa hakiwezi kushirikiana na vyama vingine vya upinzani bungeni kwa sababu, vimeungana na CUF ambayo imefunga ndoa na CCM na kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, lilikuwa mwiba mchungu wa CUF.
Katibu Mkuu Chadema, Dk Willibrod Slaa, anasema Kamati Kuu ya Chadema, imeona chama hicho hakiwezi kuwa na ushirikiano wenye tija na vyama hivyo bungeni, na kumwagiza kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, kuunda baraza kivuli la mawaziri la wabunge wa Chadema pekee.

Dk Slaa alikaririwa akisema Kamati Kuu imezingatia kuwa, CUF na CCM wamejiunga kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar na kwa kuwa, sheria inayoruhusu uwepo wa vyama vya siasa inahusu pande zote za Muungano, inaamini CCM na CUF ni wamoja hata Bara.
Tamko hilo liliibua mvutano mkubwa wa kisiasa kati ya CUF na Chadema na kuwafanya viongozi mbalimbali wa CUF kuitupia lawama Chadema kwa madai kuwa haikutenda haki ya kidemokrasia.
Hivi karibuni, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba wakati anazungumza kuhusu masuala ya Uchumi, siasa na Usalama anasema Chadema inaendesha siasa zinazoweza kuibua vurugu nchini.
Kitendo cha Chadema kuibeza serikali ya umoja wa kitaifa ya Zanzibar ni kuwadharau Wazanzibari na kuwatakia shari, Zanzibar ni sehemu moja kati ya mbili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chuki za Chadema haziutakii mema muungano wetu, anasema Profesa Lipumba.
Profesa Lipumba ambaye tangu mwaka 1995 mpaka sasa amekuwa akiwania urais kwa tiketi ya chama hicho anasema kitendo cha Chadema kuifananisha CUF na CCM B kwa sababu ya kushiriki katika serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar ni dharau kwa Wazanzibari.
Anasema kabla ya kura ya maoni ya Wazanzibari, Kituo cha Demokrasia Nchini (TCD), chini ya uwenyekiti wa Chadema kiliandaa tamasha visiwani Zanzibar kuwahamashisha Wazanzibari kupiga kura ya ndiyo ili kuwepo na mabadiliko ya katiba yatakayoleta Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Serikali ya Umoja wa Kitaifa inatokana na kura ya Wazanzibari iliyoungwa mkono na Chadema. Katiba ya Zanzibar inaelekeza kuwa chama chochote cha siasa kitakachopata asilimia 5 au zaidi ya kura zote kitakuwa na haki na wajibu wa kushiriki katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa, anasema Profesa Lipumba.
Anasema Chadema ilishiriki katika uchaguzi wa Zanzibar ikielewa wazi katiba ya Zanzibar.
Kama ingepata alau asilimia 5 za kura, wawakilishi wao wangeshiriki katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa, sasa wanapobeza serikali hii ni kuwadharau Wazanzibari na kuwatakia shari, anasisitiza Profesa Lipumba.
Anasema serikali hiyo imeleta amani katika siasa za Zanzibar na kwamba kauli za Chadema kuidhalilisha Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar haiitakii amani Zanzibar inalenga kuuvuruga Muungano.
Watanzania wote wanaopenda amani wanastahiki kulaani kauli za Chadema, anasema.
Anasema katika mfumo wa vyama vingi na nchi yenye serikali katika ngazi mbalimbali ni jambo la kawaida kwa chama kushirikiana katika ngazi moja wakati vyama hivyo hivyo vinapingana katika ngazi nyingine.
CUF ilipokuwa na wabunge wengi ilishirikiana na Chadema, Chadema imekataa kushirikiana na CUF na vyama vingine vya upinzani. Hii inaonyesha kuwa Chadema haina lengo la kujenga umoja wa Watanzania, anasema Profesa Lipumba.
Anasema kauli za viongozi wa Chadema katika mikutano ya hadhara mkoani Mwanza ambapo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alionya kama Rais Kikwete hatachukua hatua kuinusuru taifa yaliyotokea nchini Misri, Libya na Tunisia yanaweza kutokea Tanzania, ni kauli ambazo zinaweza kuchochea vurugu za kisiasa.
Pamoja na mapungufu ya katiba na Tume huru ya uchaguzi, uhuru wa kisiasa uliopo Tanzania ni mkubwa kuliko hali ilivyokuwa Tunisia, Misri na Libya, anasema Lipumba.
Anasema kufanya maandamano kwa malengo ya kuifanya nchi isitawalike hakusaidii kujenga misingi ya demokrasia.
Anasema wanaotaka kuingia madarakani kwa kuiangusha serikali kupitia maandamano hawana nia ya kuwakomboa Watanzania na kujenga msingi imara ya demokrasia.
Hawa wanahitaji kuwatumia wananchi kuingia madarakani na wakishapata madaraka hawatakuwa na lengo la kujenga demokrasia ya kweli na hawatakubali kungolewa kwa kura, anasema Lipumba.Anasema wanasiasa wenye malengo halisi ya kujenga demokrasia wanastahiki kujikita katika kudai Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.
Anasema Rais Kikwete amekubali kuanzisha mchakato wa kupata katiba mpya hivyo ni wakati wa vyama vya siasa kutoa mapendekezo ya mambo ya kuzingatiwa katika mswada wa sheria utakaopelekwa bungeni kwa lengo la kuanzisha mchakato wa kupata katiba mpya ikijumuisha kuundwa kwa tume ya kuongoza mchakato huo.
Ni wakati wa kuandaa na kupeleka serikalini hadidu rejea za Tume itakayosimamia mchakato wa kupata katiba mpya, anasema Lipumba.
Anaongeza, Ni wajibu wa viongozi makini kumuunga mkono Rais Kikwete katika jambo hili jema na kushiriki kikamilifu kuhakikisha tunapata katiba mpya. Hatuwezi kupata katiba yenye misingi ya demokrasia ikiwa Chadema watafanikiwa kuifanya nchi isitawalike.
Anasema kuandaa vyema uchaguzi mkuu 2015 kunahitaji kuwepo kwa Tume huru yenye mfumo unaofika kwenye majimbo ya uchaguzi.Anasema serikali inapoonekana kuyumba, wanaotaka nchi isitawalike watapata fursa ya kufanikisha malengo yao.Mvutano wa vyama vya upinzani ni mzito, ni ndoto kwa vyama hivi kuweza kushirikiana kama Watanzania wengi wanavyoota kila kukicha.
Nchini Kenya vyama vingi vilipoanzishwa havikufua dafu kwa chama tawala (KANU).
Baada ya chaguzi mbili za vyama vingi, vyama vya upinzani vikaamua kuungana kwa mujibu wa sheria ya nchi yao na hatimaye wakapata rais mpya aliyetokea upinzani, ndiyo ukawa mwisho wa chama tawala.
Pamoja na hayo, kukazuka mgogoro wa chama hiki kudai kuwa kimepewa mawaziri wachache, kile kikidai kunyimwa wizara nyeti, hiki kikidai makubaliano yamekiukwa mpaka wakagombana.
Walisambaratika na kumlazimisha rais aliyetokana na upinzani kuanzisha ushirikiano mpya na rais aliyeondoka madarakani na hivyo kufifisha vita dhidi ya ufisadi na kusababisha serikali iliyokuwa madarakani ionekane ya ufisadi sawa na ile serikali iliyokuwa imepita. Je, Huo ndiyo ushirikiano wa vyama vya upinzani unaotafutwa na Watanzania?