Lipumba azungumzia Katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lipumba azungumzia Katiba mpya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Mwiba, Mar 2, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Lipumba azungumzia katiba mpya
  Salim Said

  CHAMA cha Wananchi (CUF), kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kuhakikisha kuwa anasimamia rasimu ya katiba mpya yenye misingi ya kidemokrasia.

  Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kutambulisha safu mpya ya uongozi wa chama hicho kwenye Uwanja cha Kidongo Chekundu jijini hapa, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema katiba mpya yenye misingi ya kidemokrasia ndio itakayomjengea heshima Rais Kikwete.

  Alifafanua kuwa rasimu ya katiba hiyo iko kwa wadau kushughulikiwa na akamtaka rais kusimamia kupitishwa kwa rasimu hiyo baada ya kutoka kwa wadau ili iwe sheria kamili.

  Akizungumza wakati wa kumkaribisha mwenyekiti, katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad alisema CCM lazima iondoke madarakani kwenye uchaguzi wa mwaka 2010.

  "Ndugu zangu udhalilishaji na manyanyaso yaliyopo kwa Watanzania ni kwa sababu ya Serikali ya CCM... imechoka na lazima iondoke 2010," alisema nana huku wananchi wakimshangilia kwa kusema yes we can.

  Maalim Seif aliongezea "CCM Ikubali kutunga katiba mpya au isikubali, lazima itaondoka; ikubali kuunda tume huru ya uchaguzi au isikubali lazima itangÂ’oka tu. Kipimo tutakiona katika uchaguzi mdogo wa jimbo la uwakilishi la Magogoni Zanzibar. Ni jimbo letu ila tuliporwa kwa vifaru na magari ya kumwaga maji ya kuwasha."


  ___________________
  Hiki kipande cha mwisho ni siasa au ni mtego kwa CCM kwa anaejua siasa katika hali ya leo,hapo ni dhahiri kuna mtego kwa CCM ,nawashauri CCM bora hilo jimbo wawaachie CCM kuliko kutaka kufanya ubabe.Kwani CCM wakifanya hila hapo basi wajue ndio wamekwisha kabisa.
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kama kuna Magogoni kule Pemba, lazima watashinda tu!
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Unajua mapaparazi wa CCM hapa JF mpo wengi kwa ufupi ,mmeivamia JF ,nimeangalia sana na kuona kuna hitilafu katika uchangiaji aidha wapinzani inaonekana wamezidiwa nguvu na mapaparazi wa CCM au wanausalama kama wanavyojiita kisheria, usalama mkubwa wa kuilinda CCM isiondolewe madarakani ,mpaka sasa kuna mvutano kati ya Slaa na Zitto ,sijui kama mnaelewa kuwa hivi sasa mambo si sawa kati ya Zitto na Slaa.

  Ila ndio walivyo mara nyingi mamluki huona mmoja kapewa kidogo au kalipwa kidogo au mmoja anapemndelewa.

  Ila CUF dau lake ni jingine ,CUF wanasema huu si wakati wa kushughulika na mafisadi ,huu ni wakati wa kumkomboa Mtanzania kutoka katika mauza uza na ubabaishaji wa CCM ,si unakumbuka yale maudhui ya Mbutolwe mwana wa Umma ,nenda kasome uone namna watu wanavyopigania haki,haki haitapatikana kwa kumsakama Lowasa na Karamagi au yule mfanya biashara wa Ikulu. Haki itapatikana kwa kuisakama CCM nzima kama chama ambacho hakina na kimepoteza sifa ya kuwa viongozi wanaoheshimika ndani ya jamii.

  CUF inakwambia moja kwa moja kuwa CCM haifai kuongoza nchi hii ,na sio Lowasa au Kikwete ,CCM nzima imeoza ,wameua maalbino mpaka wamechoka sasa wanawambia wananchi wapige kura kuchagua nani muuwaji ,hapa CCM wameniwacha hoi maana kwa kimombo tunasemea wamemake my day !!! :D
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Tatizo CUF wamekosa mwelekeo... yaani sasa wapo sawa na nyani jangwani... hana amani atapata wapi mti wa kupanda?
   
 5. M

  Mama JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2009
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  CCM is there to rule Tanzania kwa miongo kadhaa ijayo kwa sababu vyama m-badala vimedorora, mdebwedo so to say.
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mwiba,
  CUF wanakosea kama wanafikiri si wakati muafaka wa kushughulikia ufisadi. Bila ufisadi kuondolewa Tanzania njema haitawezekana.
   
 7. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  CUF hamna jipya hadithi tu zile zile za Seif na Lipumba tangi 1992!

  Ni kwa nini hamna mawazo mapya?
   
 8. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Nimeshangaa kuona wamewarudisha wale wale kwenye madaraka....hivi lipumba na usomi wake ulio tukuka....anafikiri katika kuiongoza tanzania one day?Maalim seif aliye kimbia wafuasi wake mwaka 2001 wakati wanapata kipigo cha polisi leo wanamchagua kwa kishido?Kesho anasema kikwete kaiba kula mwaka 2005?Tuamini vipi yeye haibi?
  Ina maana hakuna wao faa uko kwenye CUF?CCM will be here forever kama vyama vya siasa havita amua kubadili Uongozi na mengine mengi..toka 1995 tunawasikia hao hao.Huyu lipumba aende akafanye research,za uchumi mwisho wa siku aje na proposal nzuri awape vijana waitete..sio kutaka kuwa mwenyekiti kila wakati...ni msomi anaye hitaji muda wake kufanya yaliyo ya maaana.
   
 9. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  Sasa na wewe tukuite Paparazi wa Chama cha 'Wananchi' (CUF) ama?????
   
 10. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #10
  Mar 2, 2009
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwa sehemu naikubali CUF kama moja ya vyama vya upinzani v nyenye wabunge wengi ingawaje wanatoka visiwani zaidi (wote wa majimbo wametoka Pemba tu)

  Ninajipa wakati mgumu kuamini kuwa CUF ni chama makini chenye nia thabiti ya kupambana na umasikini, rushwa/ufisadi, maradhi na ujinga.
  CUF haioni kuwa CCM ndiye adui wa jamii. CUF inahangaika sana kuhakikisha kuwa inasurvive hata kama ni kwa kupambana na wapinzani wenye miale mikali ya kupambana na Jibwana la Ufisadi CCM.

  Hii naona kama hatari kubwa sana.

  Sioni mahali ambako CUF itajirekebishia na kuwa chama kinacholenga kuondoa umangimeza wa CCM.

  CUF??? Sijui
   
 11. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Yap kuna point ndani yake
   
 12. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kuna kitu kimoja ambacho nadhani wengi hawakioni (hasa wanansiasa wa Upinzani). Nacho ni ukweli kwamba hakuna uwezekano wowote wa chama chochote cha upinzani kuishinda na kuiondoa CCM madarakani kwa sasa. Ukweli huo (mkali na usiopendwa na wengi) unatokana na misingi ya uanzishwaji wa vyama vingi vya siasa nchini 1992.

  Ikumbukwe kwamba, serikali na hasa CCM haikupenda kuwepo kwa vyama vya upinzani nchini (mapambano na waliokuwa na mawazo ya uhuru wa kisiasa yanaweza kutumika kuthibitisha hivyo. Mapalala, Fundikira, Seif n.k). Hayati Baba wa Taifa ndie alieishinikiza CCM kukubal na kupitisha ruhusa ya upinzani kuwepo na kupewa fursa ya kushiriki katika siasa Tanzania kisheria, baada ya kutishia viongozi wa CCM kuhusu kupotea kwa amani endapo watazuia mahitaji hayo ya wananchi. Pamoja na yote hayo, Katiba ya nchi haikutoa fursa kamili ya upinzani kushiriki kwa usawa katika siasa na hivyo kuipa CCM uhakika wa kushinda uchaguzi wa Rais na Wabunge (wengi) kila mara kutakapokuwa na uchaguzi. CCM inatoa nafasi ya wabunge wachache kushinda, nao hawana nguvu zozote za kuiyumbisha CCM.

  Nadhani serikali ya CCM inapenda/inafurahia hali hii ya wabunge wachache kutoka upinzani na wengi kutoka CCM. Wanaipenda hali hiyo kwasababu inadhihirisha/inatoa taswira ya demokrasia nchini (hasa kwa international community).

  Bila Katiba kubadilika, nyimbo hizi za kuiangusha CCM hazitakuwa na mchezaji kwa miaka mingi sana. Tutaimba tu, halafu itafika siku tutasahau hata chorus yake ikoje.

  Wanasiasa hasa wa upinzani wanatakiwa kushinikiza Katiba mpya. Na katiba mpya haitakiwi kutungwa na watu wachache katika hotel moja Jijini Dar halafu ikaitwa Katiba ya nchi. Kufanya hivyo kutakuwa ni sawa na mchezo wa watoto kutengeneza magari ya kuchezea na kudhani kuwa ni magari ya kweli. Kwa tafsiri nyingine, ni sawa na kuchezea muda na rasilimali chache walizonazo tu. Kufanya hivyo ni kupotofu kuliko hata kuwepo kwa Katiba ya sasa, iliyotungwa na waTanzania wachache (WaBunge) kupitia Bunge halali, japokuwa ina mapungufu mengi na ya makusudi.

  Katiba ya nchi inatakiwa itungwe kutokana na mapendekezo ya wananchi karibu wote wa Tanzania. Ingefaa itokane na mapendekezo ya watu wasiopungua asilimia 10 (10%)ya waTanzania wote, wenye akili timamu. Hiyo ndio itakayoweza kuwa Katiba sahihi ya nchi, na itakuwa na mapungufu machache zaidi ya ile inayotungwa na kikundi fulani cha watu kwa maslahi yao binafsi.
   
 13. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu una uhakika ama kuna moto mgeni unauwasha hapa?
   
 14. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nakubaliana nawe kabisa. Lakini kwa magogoni hii tunayoijua sisi, hashindi asilani-hata akichangiwa na wale wanaoishi katika majumba ya kale ya Mji Mkongwe, wanachama wa CCM na wapenzi wa CCM ni wengi katika eneo hilo kulinganisha na wafuasi wa CUF.
   
 15. D

  David Nkulu Member

  #15
  Mar 3, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ikiwa lengo ni kubadilisha katiba, kwa nini inaonekana kuwa rais ndiye mhusika mkuu?
  Ninavyoona mimi, rais ndiyo tatizo kubwa ktk jitihada za kubadilisha katiba. Ukweli ni kuwa JK na watanzania wote tumerithi katiba ambayo ilitengenezwa wakati wa JKN. Katiba hii, inampa madaraka makubwa sana rais bila kujali kuwa yeye pia ni mtu kama wengine, na inabidi awekewe breki za kisheria ili pasiwe na dictatorship ndani ya demokrasi.
  Jitihada hizi lazima zianzie bungeni au wananchi wahamasishwe (signed petition) kutaka iwe ni moja ya mabadiliko ambayo lazima yatokee ili tuweze kukabili matatizo ambayo kama nchi tunashindwa kuyakabili tangu tufukuze wakoloni!!
   
 16. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ndio kabisa ,kwanza kabla sijaendela nimezidi kuwaona wanausalama ambao wamo humu JF ,kwa ufupi wote wamenasa tena vibaya sana ,maana wameshindwa angalau kujificha ,natumai wamekurupushwa huko kazini mbona kuna Mwiba unakwaruza kwaruza hapo JF ,ajabu awamekuja na hoja hazina miguu wala kichwa ,ila niwawache maana wapo kazini hawawezi kuonyesha hisia za usambaratishaji wa Taifa hili unaofanywa na CCM.Pia inawezekana hawajui watendalo. :D

  Kwa yeyote yule ambae atasema CUF haina nguvu hapa Tanganyika huyo atakuwa anajidanganya tena anajidanganya wakati kuna muangaza na mchana aidha atakuwa amehadaika na kiza akafanya haja njiani.

  CUF ,Chama Cha Wananchi kina asili ya kupendwa na hata watoto wadogo ambao wakiitamka tu ile CUF unawaona wamejaa matumaini juu ya Chama wanachokitamka ,yaani wanakuwa wenye furaha na kuchangamka kabisa ,huu ni ukweli ,si wakiristo si waislamu CUF ina mvuto wa aina yake ,sijui kwanini labda naweza kusema ni siri ya Mungu Mwenyewe.

  Tofauti na vyama vingine hapa Tanganyika na Zanzibar ,kimekuwa Chama tishio kwa CCM na wenyewe CCM wanalijua hilo kwamba hakuna Chama kinachotishia utawala wao kama CUF ,CCM wanajua kama uchaguzi utakuwa wa haki na sawa usiokuwa na mizengwe basi wataachwa mbali sana na CUF kwa idadi ya kura.

  Mtikiso ambao unatayarishwa na CUF kwa kipindi hiki ni kuiangalia KATIBA ya Tanzania na kuibadilisha ili kukidhi mahitaji ya Taifa hili chini ya mfumo wa vyama vingi ,jambo ambalo ndicho kiini cha kumalizika kwa Utawala wa Kisultani wa CCM ,maana tukitaka tusitake Sultani wa Nchi hizi ni CCM ,hivyo kiti cha Usultani kinakaliwa na watoto wa Sultani ambao ni magogo ya CCM waliojimilikisha hatamu za nchi hizi ,ulinzi usalama upolisi ujeshi umahakama utume yote hayo yanaongozwa na Ukoo wa Sultani huyu CCM.

  Ni kweli kabisa kama alivyosema mmoja wetu hapa bila ya WaTanzania kuibadili katiba iendane na wakati itatugharimu mapinduzi kuuangusha utawala wa Sultani CCM. Wakulima na wafanyakazi pamoja na wachungaji itawabidi waikatae Serikali ya Sultani CCM kwa nguvu na si vinginevyo ikiwa Sultani huyu kila anavyoshauriwa hataki wala hakubali.

  Wananchi wameweza kuziangusha Serikali za Kisultani wa aina hii ambazo zilikuwa na nguvu kuliko huyu Sultani wetu.Na kwa kweli si jambo kubwa sana mara tu wananchi walio wengi watakapokubaliana kuwa sasa Sultani CCM anavuka mipaka na ameshakata kamba haambiliki ,hakataziki wala hasikii la mwengine basi ni kuamua tu kumzingira kila kona na kumwambia hatukutaki katika utawala wa nchi hizi.

  CUF imeamua kushika usukani katika kuwaamsha tena wananchi kuwa maendeleo hayatafikiwa kwa miaka ya karibu au haytafikiwa kabisa ikiwa Usultani wa CCM hautaondolewa kwa njia za kuibadili Katiba na kama hawataki itabidi kuungana kwa umoja na kukana Usultani wao.
   
Loading...